Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Pham Dinh Quan (watatu kushoto), akikabidhi hundi ya
shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda, kwaajili ya kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa katika kuboresha
sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu 402 zilizoko jijini hapa katika hafla fupi iliyofanyika katika shule ya
msingi Mapinduzi jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Pham Dinh Quan, , (kushoto), akizungumza
na waandishi wa habari pamoja na viongozi mbalimbali wa kamati ya ujenzi wa ofisi
402 za walimu alipokwenda kukabidhi hundi ya shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwaajili ya kuunga mkono jitihada za
serikali ya Mkoa katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa
ofisi za walimu 402 zilizoko jijini hapa
katika hafla fupi iliyofanyika katika
shule ya msingi Mapinduzi jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya
Halotel Mhina Semwenda, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari pamoja na
viongozi mbalimbali wa kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu wakati kampuni
hiyo ilipo kwenda kukabidhi hundi ya shilingi milioni Hamsini
(50,000,000) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwaajili ya kuunga
mkono jitihada za serikali ya Mkoa katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania,Picha na Brian Peter
Dar es Salaam, Januari 22 2018…………… Katika kuunga mkono jitihada
za serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, kampuni ya simu za
mkononi ya Halotel imetoa mchango wa fedha taslim Shilingi milioni Hamsini
(50,000,000) kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni moja ya
utekelezaji wa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali na ofisi
hiyo katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za
walimu kwa shule 402 kati ya hizo shule 295 ni za elimu ya awali/msingi na
shule 107 ni za sekondari zilizoko mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mchango huo
kwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda, Mkurugenzi mkuu wa
Kampuni ya Halotel, Le Van Dai amesema mchango huo ni sehemu tu ya jitihada
kubwa zinazofanywa na kampuni hiyo katika kusaidia na kuinua sekta ya elimu
nchini ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali
katika kuboresha maendeleo ya nchi hasa kupitia sekta ya elimu ambayo ni
muhimili wa maendeleo ya kila nchi duniani.
“Tunatambua kuwa, huduma bora ya elimu kwa wanafunzi na waalimu
ni moja ya msingi imara katika kukuza sekta ya elimu nchini, kwa kuzingatia
hili tumeamua kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa
mchango wetu wa kifedha ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa ofisi za waalimu
ikiwa ni sambamba na kuboresha mazingira utendaji kazi kwa waalimu ya kazi na
kurahishisha ufanisi wao katika kuwafunza wanafunzi ambao ni taifa la leo na
kesho” alisema Dai.
“ Halotel tumekuwa mstari wa mbele tukishirikiana na serikali
katika kuboresha sekta ya elimu kupitia teknolojia, kwa mfano tumekuwa
tukitekeleza mradi wa kuunganisha shule zaidi ya 400 nchi nzima na huduma ya
intaneti ni ya kipekee sana, tumeendelea kuhakikisha sisi kama kampuni
tunausimamia na kuhakikisha unaleta mabadiliko na tija kwa elimu yetu.”
Alisema.
“Katika kuhakikisha mradi huo wa intanenti unawanufaisha waalimu
na wanafunzi katika kuboresha uelewa na ufaulu wa masomo yao, Halotel kwa
ushirikiano na Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) cha Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tumeunda jukwaa (Mfumo) wa kujisomea kupitia
mtandao wenye masomo ya Sayansi na Hisababati kwa kufuata Mtaala uliokubaliwa
na serikali, ambalo unawawezesha waalimu na wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza
(I) mpaka cha nne (IV) nchini kote kusoma masomo hayo. Mfumo huu unaoitwa
Halostudy, na linapatikana kupitia tovuti
(http://www.halostudy.ac.tz/). Jukwaa hili ni Tofauti na majukwaa mengine yanayofanana, kwa
maana maudhui yaliyotengenezwa yameunganishwa na vipengele vya multimedia kama
vile video, sauti, na michoro katika maeneo maalum ambapo maudhui mengine ni
vigumu kuelewa kutumia maandishi pekee:” Aliongeza Dai.
Kampuni ya simu za mikononi ya Halotel imekuwa mstari wa mbele
katika kushirikiana na serikali na itaendelea kufanya hivyo katika kuboresha
sekta ya mawasiliano nchini, pamoja na sekta nyingine ikiwa ni utekelezaji wa
kuboresha maisha ya watanzania kupitia uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni
hiyo nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment