Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kibenki kwa
njia ya Mitandao wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), John Mhina (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary
Advance’ ambayo wateja
wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi
nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine
kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji
Biashara na Masoko, Valence Luteganya na Meneja Masoko wa benki hiyo, Rahma Ngassa.
Mkuu wa Kitengo
cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Mwalimu
Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa tatu kushoto), akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya
‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja
wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi
nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine
kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa
njia ya Mitandao, John Mhina na Meneja Masoko, Rahma Ngassa.
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo
mbalimbali vya habari wakirekodi tukio la uzinduzi wa huduma ya ‘MCB Salary
Advance’ ambayo wateja
wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi
nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura jana katika
ukumbi wa tawi la benki hiyo Barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment