Benki ya TPB yasaini mkataba wa mahusiano na taasisi ya Tanzania skauti association lengo ikiwa ni kuweza kusaidiana katika kuijenga Taasisi hiyo ya skauti.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshindi amesema lengo la kusaidia kuijenga Tanzania skauti association na kusaidia kutengeneza data za kuwatambua wanachama wao waliopo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa kadi za kisasa kwa ajili ya wanachama wao
Amesema katika kutengeneza mahusiano yao kutawasaidia kutoa elimu kwa Vijana namna ya kuweka akiba kwa manufaa yao na kizazi kijacho pia.
"Niwashukuru Sana Tanzania skauti association walivyokuja na wazo hili kwani kutasaidia kuelimisha na kutoa elimu kwa Vijana ya namna ya kuweka akiba kwani Vijana wengi hawajui njia za kuweka akiba yao ya mbeleni. "Alisema Mkurugenzi wa TPB
Aidha amesema wataweza kuwasaidia Tanzania skauti association kukusanya mapato yao kwani watakuwa tayari wamefahamu wanachama wao kutokana na ladies zitakazotolewa.
Kwa upande wake kamishna Wa chama cha skauti Tanzania Abdulkarim Shah, meishukuru Benki ya TPB kwa kukubali kusiani mkataba wa mahusiano na kuweza kupata kadi zitakazotambulisha wanachama,ambapo amesema itasaidi kuwatambulisha na kufahamu wanachama wa skauti anapopatikana.
0 comments:
Post a Comment