Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Mwalimu Commercial Plc, (MCB) Ronald Manongi (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
wakati wa uzinduzi rasmi ya akaunti mpya ya ‘Tukutane Januari’ yenye lengo la
kuhamasisha moyo wa ujiwekea akiba kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndongole, Mkuu wa
Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Lutegenya na Meneja Mahusiano
kwa Wateja, Charles Shadrack. Akaunti hii itakuwa mkombozi kwa wateja kuweza
kujiwekea akiba itakayowawezesha kumudu mahitaji muhimu yanayojitokeza mwanzoni mwa mwaka.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa
Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa pili kulia),
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi
ya akaunti mpya ya ‘Tukutane Januari’ yenye lengo la kuhamasisha moyo wa
kujiwekea akiba kwa wateja wake na kwa watanzania kwa ujumla. Wengine kutoka
kushoto ni, Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndongole, Ofisa Mtendaji Mkuu wa
MCB, Ronald Manongi, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence
Lutegenya na Meneja Mahusiano kwa Wateja, Charles Shadrack. Akaunti hii itakuwa
mkombozi kwa wateja kuweza kujiwekea akiba itakayowawezesha kumudu mahitaji
muhimu yanayojitokeza mwanzoni mwa
mwaka.
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya
habari wakirekodi tuki la uzinduzi wa akaunti mpya ya Tukutane Januari ya Benki
ya Mwalimu Commercial Plc jijini Dar es Salaam leo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC
YAZINDUA BIDHAA KWA AJILI YA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA.
15 JANUARI 2018, Dar es
Salaam – Mwalimu Commercial Bank PLC
(MCB) imezindua bidhaa iitwayo Tukutane Januari Akaunti, ikiwa ni moja
ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Akizungumzia Kuhusu akaunti hii
mpya ya akiba ya ‘Tukutane Januari’, Mkurugenzi Mkuu wa MCB, Bwana
Ronald Manongi alisema, mteja ataweza kujiwekea akiba kidogo kidogo wakati
wowote katika kipindi chote cha hadi kufikia Januari. Akaunti hii ina riba ya
kuvutia ambayo mteja wetu atalipwa kila robo ya mwaka.
Vilevile inamuwezesha mteja
wetu kupata mkopo wa hadi asilimia 30 ya amana yake katika kipindi cha mwaka
husika. Hivyo Mteja atakapoweka akiba zaidi atafaidika zaidi, na atakuwa na
uwezo wa kukopa kiasi kikubwa kulingana na akiba ya akaunti yake.
Akaunti hii ya akiba
itamuwezesha mteja kujiondolea usumbufu wa kutatua mahitaji muhimu ya kipesa
kipindi cha mwanzo wa mwaka husika ikiwa ni pamoja na ada za shule na vyuo na
manunuzi mengine ya vifaa vya shule, pia kodi za nyumba hivyo kuondokana na
dhana ya Januari kuwa ni mwezi mgumu.
Mkurugenzi huyo pia aliwaasa
watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba mara kwa mara kwani husaidia sana
kutatua matatizo mengi yanayoikabili familia na jamii kwa ujumla. “Mara nyingi
watu wamejikuta wakiingia katika madeni makubwa na fedheha pale wanaposhindwa
kulipa madeni hayo”, alisema Ndugu Manongi. Akiendelea Ndg Manongi alisema
“Hivyo benki hii ya biashara ya Mwalimu imebuni mkakati huu kuisaidia jamii
kuazimia kupunguza na/ama kuondokana na fedheha, adha na madhara yanayotokana
na kuwa na majukumu mazito mwezi huo wa kwanza wa mwaka”.
Naye Mkuu wa kitengo cha
Biashara na Masoko aliongeza kwa kusema “Uzinduzi wa huduma hii mwanzoni mwa
mwaka 2018 ni moja ya ishara kuwa Benki ya Mwalimu imejipanga vyema katika
kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka
huu kuwa wa neema kwa wateja wetu. Hivyo tunakaribisha Watanzania wote kuja
kufungua akaunti na kuweza kufaidi huduma na bidhaa zetu.
MWISHO.
Kwa taarifa zaidi wasiliana
kwa:
Mwalimu Commercial Bank Plc
(MCB).
Mlimani Tower - Mezzanine
Floor, Sam Nujoma Road
P.O. Box 61002, Dar es Salaam
Telephone: 022-2772954/7 and
+255 629 331 151
Email; info@mcb.co.tz
0 comments:
Post a Comment