Kampuni ya UmojaSwitch leo imechezaesha droo yake ya bahati nasibu ya Shinda na Umoja kwa wateja wake zaidi ya 32,222 waliotumia kadi za UmojaSwitch kati ya tarehe 1- 8 Januari mwaka huu ambapo zaidi ya wateja 25 wameibuka washindi katika droo ya leo.
UmojaSwitch ilianzisha bahati nasibu hiyo ya Shinda na Umoja mwezi Desemba mwaka jana kwa lengo la kutoa hamasa kwa wateja wao kupitia kampeni yao ya kubadili kadi za UmojaSwitch kutoka kwenye mfumo wa zamani na kwenda kwenye mfumo mpya wa ‘Microchip’
Katika makundi matatu yaliyo chezeshwa leo kundi la kwanza limetoa washindi 25 waliojishindia T-Shirt za UmojaSwitch,
Mzunguruko wa pili umetoa washindi wa tano wa Simu za Mkononi (Smart Phone), mzunguruko wa tatu umepata washindi wawili wa fedha taslimu mara mbili ya fedha walizokuwa wanatoa kwenye Akaunt zao kupitia kadi za UmojaSwitch na Mzunguzuro wa nne umepata mshindi mmoja aliejishindia kiasi cha Shilingi Milioni Moja Taslimu.
Akiendesha Droo hiyo Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Bi BeatriceEmmanuel Chini ya Mkaguzi wa Bodi ya Michezo yakubahatisha Bakari Maggid amewapongeza washindi wa zawadi hizo na kudai kuwa watafanya mawasiliano na Benki husika wanazotumia washindi wao ili kuweza kuwapatia zawadi zao muda mchache kuanzia leo.
Aidha Beaterice amewataka wateja ambao bado hawajabadilisha kadi zao za awali kufika kwenye Benki husika ili kubadili kadi zao na kuwea kuingia katika bahati nasibu hiyo ya Shinda na UmojaSwitch kwenye droo inayofuata.
Kampuni ya UmojaSwitch inaunganisha mabenki zaidi ya 27 Tanzania kwa lengo la kushirikiana kutoa fedha kwa njia ya kilectronic ya ATMs
Afisa Masoko wa UmojaSwitch Beatrice Emmanuel (kushoto) akibonyeza kitufe kuashiria kuchezesha droo ya bahati nasibu ya Shinda na Umoja kwa wateja wake zaidi ya 32,222 waliotumia kadi za UmojaSwitch kati ya tarehe 1- 8 Januari mwaka huu ambapo zaidi ya wateja 25 wameibuka washindi katika droo hiyo hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika katika ofizi zao jijini Dar es Salaam leo (kulia) ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo yakubahatisha Bakari Maggid
Afisa Masoko wa UmojaSwitch Beatrice Emmanuel akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment