Meneja Huduma Mbadala za Benki wa Benki ya Equity Magreth Mwasumbi (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mfumo wa kadi za kutoa fedha za kigeni (Visa debit card) ambapo mteja akiwa na kadi hiyo anauwezo wakufanya malipo katika maduka makubwa na madogo, Migahawa,Hospital, Vituo vya mafuta Mahotelini na huduma nyengine nyingi Hafla hiyo imefanyika leo katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam wengine pichani kushoto ni Meneja Diaspora wa Benki ya Equity Doreen Raphael pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Malipo na IT Keneth Wakati.
Meneja Huduma Mbadala za Benki wa Benki ya Equity Magreth Mwasumbi (kushoto) Meneja Diaspora wa Benki ya Equity Doreen Raphael (katikati) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Malipo na IT Keneth Wakati wakionesha mfano wakadi hizo mara baada ya kuzindua.
DAR ES SALAAM, Disemba 2, 2020 | Taasisi inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kifedha Equity Bank Limited, leo imezindua kadi mpya ya kisasa ya Visa inayotumia mfumo wa sarafu ya Dola ya Kimarekani ‘VISA USD Debit Card’ kwaajili ya matumizi ya wateja wake nchini Tanzania.
Kadi hiyo iliyotengenezwa kwa kiwango cha dhahabu ni ya kwanza na ya kipekee ikiwa na malengo ya kutoa urahisi na upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, ambao wanataka kufanya manunuzi kupitia mtandaoni au kufanya biashara kwa kutumia sarafu ya Dola ya Kimarekani.
Kadi hiyo inampa mteja fursa ya kulipia bidhaa na huduma mbalimbali kwa sarafu ya Dola ya Kimarekani pasipo na nyongeza ya malipo yoyote ya ziada. Itamsaidia mteja kufanya miamala pasipo kuvuruga bajeti yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania Limited, Robert Kiboti, anasema kuwa kadi hiyo ni nafuu, inatoa suluhisho la bei, ni rahisi na salama kwa mteja na itamsaidia sana mteja katika kurahisisha huduma kwa wakati sahihi lakini pia kuchochea ukuaji wa biashara ya mtandaoni.
“Kadi ya Visa Gold Debit inaruhusu wateja kulipia bidhaa au huduma kwa Dola za Kimarekani kwa viwango vilivyoonyeshwa kwa wakati huo. Hii inamaanisha kuwa ikiwa unalipa bidhaa inayouzwa Dola 10 za Kimarekani, hiyo ndiyo inayokatwa katika akaunti yako- hakuna malipo mengine,” anasema Kiboti.
“VISA USD Debit Card inatumia mfumo wa PayWave ambapo pia mtumiaji ana uwezo wa kufanya manunuzi madogomadogo,” Mkurugenzi Mkuu, Bw Kiboti, anafafanua zaidi.
Visa PayWave ni teknolojia ya malipo isiyohusisha mawasiliano ya moja kwa moja isipokuwa kupitia mawasiliano ya kimtandao kwa kutumia chip maalumu yenye ili mtumiaji kupokea malipo.
“Kadi hii inatumia mfumo wa chip na neno la siri kwaajili ya usalama na ubora kwa mtumiaji,” Mkuu huyo wa Kitengo cha Malipo anaelezea zaidi.
Uzinduzi huo unakuja kufuatia mwenendo wa mabadiliko ya biashara ya kielektroniki, wakati ambao biashara nyingi zinahamia katika mtandao, ikiwa ni mojawapo ya madhara ya mlipuko wa Covid-19.
Dondoo Muhimu
- Pamoja na kutumika katika mashine mbalimbali za kutolea fedha (ATM), wateja wataweza kufanya manunuzi katika duka lolote linalotumia kadi hiyo ya Visa, kama vile Maduka makubwa ya bidhaa (supermarkets), migahawa, hoteli, sehemu za hosptali na vituo vya mafuta, maduka ya kawaida n.k
- Wateja watafanya manunuzi kupitia mtandaoni pasipo na gharama yoyote ya ziada.
- VISA USD Debit Card itampa mteja fursa ya kufanya manunuzi kwa sarafu ya Dola ya Kimarekani bila kuingia gharama yoyote za ziada
- Kadi hii ni ya kwanza na ya kipekee katika soko nchini Tanzania
- Inatumia mfumo wa chip na neno la siri kwaajili ya usalama na ubora kwa mtumiaji
- Kadi hii inatumia mfumo PayWave unaompa mtumiaji fursa ya kufanya miamala ya manunuzi madogomadogo wakati wote
0 comments:
Post a Comment