Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Haba na Haba Hununua Smarta’ iliyofanyika jana. Kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kununua simu aina ya Smarta kwa kulipa kidogo kidogo kuanzia Shilingi elfu moja kupitia akaunti ya Ezypesa. Kushoto kwake ni Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga.
Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga akionesha namna ya kufanya malipo kidogo kidogo kupitia akaunti ya Ezypesa ili kununua simu aina ya Smarta wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ijulikanayo kama ‘Haba na Haba Hununua Smarta’. Kushoto ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa.
Na Mwandishi Wetu | Zanzibar | Kwa kulipa kidogo kidogo kuanzia Shiling elfu moja, wateja wa Zantel wanaweza kununua simu aina ya Smarta ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni kuwawezesha watu wengi zaidi kunufaika na huduma za kidigitali.
Huduma hiyo imezinduliwa chini ya kampeni ijulikanayo kama ‘Haba na Haba Hununua Smarta’ itawawezesha wateja wa Zantel kutunza fedha kidogo kidogo kuanzia shilingi elfu moja (1,000/-) kwenye akaunti za Ezypesa na pale mteja anapofikisha kiwango cha 39,999/- ataweza kukitumia kununua simu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa alisema kama kampuni ya kidigitali imeona kuna haja ya kuja na suluhisho litakalowawezesha wateja kumiliki simu janja bila kuathiri bajeti au matumizi muhimu kwa kulipa kidogo kidogo.
“Tunatambua kwamba siyo watu wote wana uwezo wa kununua simu kwa kulipa pesa taslimu (Cash) na ndiyo maana tumekuja na huduma hii ili kuwawezesha wateja kulipa kidogo kidogo na kuwapunguzia mzigo wa kulipa kwa mara moja,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga alisema mbali na kutunza pesa kwa njia ya Ezypesa, kupitia huduma hii wateja wanaweza kuchangiana kwa kumuingizia kiasi cha fedha kwenye akaunti yake ya Ezypesa ili kumuwezesha mmoja wao kumiliki simu janja aina ya Smarta.
“Azma yetu ni kuhakikisha kila mtu anafikiwa na huduma za kidigitali na anufaike na fursa zake ikiwamo kujumuika na ndugu jamaa na marafiki lakini pia kufanya shughuli za uchumi.Kupitia huduma hii tumerahisisha zaidi upatikanaji wa simu janja bila kujali kipato cha mteja wetu,” alisema Muga.
Ili kupata huduma hii mteja wa Zantek atatakiwa kupiga *149*15# kisha 0 na kufuata maelekezo.Wateja watakaofanikiwa kufikisha kiwango wataweza kununua simu za Smarta kupitia maduka ya Zantel yaliyopo nchi nzima.
Simu za Smarta ni simu za bei nafuu zaidi sokoni hivi sasa zenye uwezo wa 4G na zinakuja na application mbalimbali ikiwamo YouTube, Google, Facebook na WhatsApp zinazomuwezesha mtumiaji kufurahia huduma mbalimbali za kidigitali.
Kuhusu Zantel:
Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.
Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment