Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea Ugeni wa wafanyabiashra/wawekezaji kutoka Nchini Uturuki na umejumuisha Makampuni matano. Ugeni huo ukiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof. Elizabeth Kiondo ugeni huo umefika chini ili kukutana na wadau mbalimbali wanaohusika na kuwezesha uwekezaji nchini.
Vilevile imebainika kwamba ugeni huo umefika nchini kutokana na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji yanayosimamiwa na Kituo cha Uwekezaji kwa wawekezaji Tanzania TIC ambapo muwekezaji anaweza kupatiwa ardhi, usajili wa kampuni, vibali na ushauri wa kimazingira.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mhe.Prof. Kiondo ameeleza kwamba ujgeni huo unawakilisha sekta za kilimo na zana za kilimo, viwanda vya nguo, viwanda vya kutengeneza pampas za watoto na watu wazima, vifaa tiba na dawa na viwanda vya kuunganisha vifaa vya kilimo.
Pamoja na mambo mengine, ugeni huo umefika ili kueleza nia yao ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. Wawakilishi wa Taasisi zenye jukumu la kusaidia wawekezaji, wameeleza kwamba maeneo wanayokusudia kuwekeza ni miongoni mwa kipaumbele cha Serikali.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Taasisi ambayo inahamasisha na kuvutia uwekezaji nchini, imetumia fursa hiyo kuelezea maeneo ambayo nchi inakaribisha wawekezaji hususan eneo la kuongeza thamani bidhaa za kilimo, uvuvi, madini, ufugaji, vifaa tiba, na katika eneo la utalii.
Naye mmoja ya wageni hao akizungumza na waandiahi wa habari ameeleza kwamba wamekuja Tanzania kwa kuwa wameshafanya uchunguzi na kubaini kuwa Tanzania inakwenda na kasi ya Uchumi wa viwanda hivyo wamefanya maamuzi ya kuweka kiwanda cha kutengeneza pampas na vifaa tiba ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, katika sekta ya uchumi wa Viwanda. .
Tayari tuna wawekezaji nchini kutoka Uturuki ambao wamewekeza kwenye sekta ya viwanda, elimu, ujenzi, kilimo na madini.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na wawakilishi kutoka TPSF, EPZA, SIDO, TCCIA na TNBC ambapo taasisi zote zimeonesha utayari wa kushirikiana na kampuni hizo katika kufanilisha uwekezaji wao hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment