Meneja Masoko na Mawailiano wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (kushoto), akikabidhi zawadi ya flat screen televisheni ya ukubwa wa inchi 40 kwa mshindi wa kampeni ya’fanya miamala ushinde’ ya benki hiyo, Darius Tebuka, jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni maofisa wa Barclays, Theresia Robert na Emmanuel Wangwe
WATANZANIA wametakiwa kutumia
mifumo ya kibenki kwa njia za kidigitali badala ya fedha taslimu katika kufanya
manunuzi hususani katika msimu huu wa sikukuu ili kujiepusha na vitengo vya
wizi na unyang’aji.
Hayo yalisemwa na Meneja Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera jijini Dar es Salaam
jana, wakati wakikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili wa kampeni iitwayo ‘fanya
miamala ushinde’ inayoendeshwa na benki hiyo.
Kampeni hiyo ya miezi mitatu
inahamasidha wateja wa benki hiyo katika kutumia huduma za kidigitali kama vile
ATM, na kupitia simu za mkononi ili kufanya malipo mbalimbali
kama vile, luku, bili za maji, ving’amuzi, kodi mbalimbali ama kuhamisha fedha
kutoka katika akaunti ama kutoka kwenye akaunti kwenda katika mitandano ya simu
za mkononi hivyo pia kupunguza muda wa kwenda katika matawi ya benki.
“Natoa hamasa kwa wateja wetu na
kwa watanzania kuondokana na tabia ya kutembea na lundo la fedha mfukoni bali
watumie huduma za Barclays za njia ya kidigitali kwani ni salama na za
uhakika”, alisema.
Katika hafla hiyo, Darius Tebuka
alikabidhiwa zawadi ya flat screen television yenye ukubwa inchi 40 aliwashauri
watu kutokuwa na wasiwasi na matumizi ya huduma za kibenki kwa njia za
kidigitali hapa nchini kwani ni salama na zinasaidia kuwapa muda wa kufanya
shughuli nyingine za uzalishaji mali.
0 comments:
Post a Comment