A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, December 14, 2018

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Singida imetupilia mbali kesi ya rushwa iliyokuwa ikimkabili mfanyabiashara, Haidar Hussein Gulamali.


Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Consolata Singano ambapo amesema amezingatia ushahidi wa mashahidi 9 wa upande wa jamuhuri waliofika mahakamani hapo.

Katika uamuzi huo, Hakimu Singano amesema hakuna ushahidi unaomgusa Gulamali moja kwa moja.

Katika kesi hiyo ambapo  Mawakili wa Gulamali walikuwa Godfrey Wasonga, amesema moja ya sababu ni kutofautiana kwa mashahidi watatu kuhusu bahasha iliyobeba fedha. 

Katika ushahidi wao kila shahidi ametaja rangi tofauti ambapo mmoja ametaja Kaki, mwingine nyeupe, huku wa mwisho akitaja Brown jambo ambalo mahakama imeshindwa kuelewa  bahasha ipi ilibeba fedha.

Pia amesema hata mchakato wa ukamataji haupo vizuri kwani hakuna mahali iliyoonyesha Pesa ziliwahi kutaifishwa hadi zilipofikishwa mahakamani, pia namna zilivyotunzwa mpaka kuletwa kama ushahidi.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Singano amesema anatupilia mbali kesi hiyo na kumfanya Gulamali kuwa huru.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive