A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Sunday, December 16, 2018

NBC yatoa elimu ya kifedha kwa mama na baba lishe soko la feri

Mkurugenzi wa wateja wadogo wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko, Sarah Laiser (kushoto), na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Alina Maria Kimaryo wakikabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa Mtendaji wa Soko la Samaki la Kivukoni, Mkuu Chanje (kulia), ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. Katika hafla hiyo iliyofanyika sokoni hapo juzi, NBC ilikabidhi pia tanki la maji vizibao kwa ajili ya baba na mama lishe na watoza ushuru pamoja pamoja na kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa wafanyabiashara sokoni hapo.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam juzi  ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao. 

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (wa tatu kushoto), akikabidhi msaada wa tanki la maji kwa Mtendaji wa Soko la Samaki la Kivukoni, Mkuu Chanje katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia vizibao kwa baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru sokoni hapo, Dar es Salaam juzi pamoja na vifaa vya kufanyia usafi, ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Nguli Wa masuala ya elimu za biashara na ujasiariamali, James Mwang’amba (kushoto), akizungumza na baadhi ya baba na mama lishe na wafanyabiashara wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanyabiashara hao sokoni hapo. 

Baadhi ya baba na mama lishe na wachuuzi wengine katika Soko la Samaki la Kivukoni, wakifungua akaunti  kujiunga na Benki ya NBC kupitia huduma yao ya kufunguliwa akaunti mahali alipo mteja. NBC pia sokoni hao, Dar es Salaam, ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao pamoja na kuwapa msaada wa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na tanki la maji, vizibao na vifaa vya kufanyia usafi.

Mama lishe wa Soko la Kivukoni wakibeba pia la kuwekea takataka muda mfupi baada ya kukabidhiwa na benki ya NBC sokoni hapo juzi.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive