Mshindi wa kwanza Kilomita 21 Mbio za Yas Half international Marathon kwa upande wa wanaume Mtanzania, Inyasi Sule, akimaliza mbio hizo ktika mashindano Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro
Hatimaye watanzania wamefanikiwa kung'ara kwenye mashindano ya mbio za Kili marathon 2025, zilizofanyika Jana Moshi mkoani Kilimanjaro.
.jpg)
Katika mbio hizo mtanzania Suleiman Inyasi aliibuka Mshindi wa kwanza wanaume kwenye mbio za km 21.
Ambapo nafasi nyingine 3 zilishikwa na watanzania wengine wa 4 huku nafasi ya 5 ikuenda Kenya kwa Bernard Kiplagat ambaye amemshinda,shumeli Said WA Tanzania na Theophile Rugamba wa Rwanda.
Inyasi amefuatiwa na Watanzania wenzake, Samhenda Sombi na Peter Mwangi huku washindani wawili kutoka nchi za Kenya na Rwanda wakiambulia kuingia kumi bora.
Mbio za Kili International Marathon zinazoshirikisha wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni ambapo kipengele cha km 21 maarufu kama Nusu Marathon kinadhaminiwa na Kampuni ya mtandao wa simu ya Yas kwa mwaka wa kumi sasa.Kwa mwaka huu 2025 washiriki zaidi ya 2000 wameshiriki mbio za Yas Marathon.
Yas imekuwa mdhamini wa mashindano ya Kili marathon kwa mwaka WA 10 sasa ambapo awali yalikuwa yakidhaminiwa na chapa ya Tigo kabla ya kubadirika kuwa Yas
Mapema hapo Jana Serikali ikishirikiana na kampuni ya Yas iliendesha kampeni maalum ya upandaji miti, ikumbukwe kwa hizi ni mbio maalum kwa ajili ya wanariadha Kutoka mataifa kadhaa hususani Yale ya afrika mashariki ambao nchi kama Kenya, Rwanda, Uganda na wenyeji Tanzania zilimeshiriki mbio hizo
0 comments:
Post a Comment