Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB)imewazawadia washindi wawili safari ya kwenda Zanzibar na malazi waliofanya miamala mingi katika msimu wa wapendanao kupitia kampeni iliyoendeshwa na benki hiyo ijulikanayo kwa jina la Mahaba Kisiwani.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Adam Mihayo, Mkurugenzi wa Biashara za Wateja Wadogo na Kati, Lilian Mtali amesema TCB imefanikiwa kukuza uelewa na matumizi ya bidhaa zake za kidijitali kwa kuwazawadia wateja hao waliofanya miamala mingi katika msimu wa wapendanao.
Amesema kampeni ya Mahaba Kisiwani inadhihirisha malengo ya kimkakati ya TCB kutumia teknolojia kukuza matumizi ya njia za kidijitali katika kufanya malipo.
Mtali amesema mbali na kuwakabidhi zawadi hizo washindi hao pia TCB inaadhimisha hatua muhimu ya miaka 100 ya huduma na ubora wa benki tangu kuanzishwa kwake.
Amewapongeza wafanyakazi wa benki hiyo kwa juhudi na mchango wao katika mafanikio ya benki hiyo. “Mafanikio ya benki yetu katika kipindi cha miaka 100 iliyopita ni matokeo ya juhudi na bidii za kila mmoja wetu.
“Tunadhamiria kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ambayo kila mmoja anathaminiwa, anaungwa mkono na kuwezeshwa tunapoendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu,”amesema
Amesema TCB inaendelea kuahidi kuwekeza katika uvumbuzi wa kidijitali na kuongeza ubora kwa wafanyakazi wake ili kuhakikisha mustakabali wenye mafanikio kwa wateja pamoja na wafanyakazi wake
'HomeHabariTCB yawazawadia washindi wa kampeni ‘Mahaba Kisiwani.'
0 comments:
Post a Comment