Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka madiwani Manispaa ya Ilala kusimamia na kupitisha shuguli za Miradi ya maendeleo bila kukwamisha wala kuichelewesha kwa kuendekeza mivutano kwani lengo la miradi Ni kutatua kero zinazowakabili wananchi.
Rc Makonda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kudai kuwa kumekuwa naucheleweshaji wa miradi kwa maslahi binafsi na kuelekeza ofisi ya Katibu tawala mkoa kuhamisha watumishi na wakuu wa Idara wanao kwamisha kazi hizo.
Aidha amepongeza kwa kuanza kwa ujenzi wa soko la Kisutu na machinjio ya kisasa ya Vingunguti baada ya kukwama.
"Miradi hii ya kimkakati tumepewa fedha, naomba tuisimamieipasavyo ili tutatue kero zilizopo Katika halmashauri zetu" Amesema Makonda.
Amewataka madiwani hao kuacha mivutano na kuongeza bidii ya kusimamia miradi ilikuokoa fedha za walipakodi na kumuagiza Mkurugezi kufanya maamuzi ya kumpa kazi ya kujenga mifereji ya Maji ya mvua Mkandarasi ambaye atafanya ujenzi haraka iwezekanavyo.
"Jambo lingine ambalo linatukwamisha pia ni kutoaminiana naomba tuaminiane ili mambo yaende naomba kama mtakwama nipo muda wote nipigieni simu wala haihitaji kutuma barua"Amesema.
Aidha amesema wakuu wa Idara wanaokwamisha maendeleo Hadi kufika May 30, mwaka huu,wawe wamamishwa ili kuepusha migongano na mivutano inayotokea hivyo amewataka kuelekeza nguvu kwa Pamoja ili kuhakikisha miradi haichelewi Tena.
0 comments:
Post a Comment