Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo, wakimsikiliza DMO Manispaa ya Temeke Dr. Gwamala Mwabulambo (kulia) akitoa maelekezo ya mradi wa Afya Katika manispaa hiyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kukagua miradi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akizungumza Katika Ziara hiyo
Amesema haiwezekani kuona Kilomita Moja ya Barabara ya DMDP Wilaya ya Kinondoni inajengwa kwa Shilingi Billion 2.7 wakati kwa Wilaya ya Temeke barabara kama hiyo inajengwa kwa shilingi Milioni 900.
RC Makonda amebaini madudu hayo wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kupitia fedha zinazotoka Serikali Kuu, Halmashau na pesa za wahisani ambapo amekwazwa na matumizi mabaya ya fedha za mkopo kutoka Bank ya dunia.
Aidha amesema kuwa Barabara za DMDP zimekuwa zikijengwa kwa kiasi kikubwa cha pesa kuliko zile za TANROAD ambazo kwanza zina ubora mkubwa, uwezo wa kubeba mzigo mkubwa na pia ni Pana.
Katika ziara hiyo ametembelea miradi ya Ujenzi wa Barabara,Hospital na Shule ambapo ameipongeza Manispaa ya Temeke kwa kusimamia vizuri miradi ya Maendeleo na kuwataka kuongeza kasi.
0 comments:
Post a Comment