A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, April 23, 2019

RC MAKONDA KUHAMISHIA ZIARA YAKE WILAYA YA ILALA

 Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam PAUL MAKONDA na Mkuu wa Wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA (katikati) wakiwa Katika Ziara ya Ukaguzi was miradi mkakati ya kimaendeleo Katika Wilaya hiyo  (kushoto) Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto


  Ujenzi was soko la kisasa kisutu ukiendelea

MKUU wa Mkoa wa Dar es  Salaam, Paul Makonda,amempongeza Kasi ya Ujenzi wa hospitali ya Kivule iliyopo Katika Wilaya ya Ilala.

RC Makonda amefikia hatua hiyo Mara baada ya kufanya Ziara Katika Wilaya hiyo na kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ambapo amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa kivule, Ujenzi wa Soko la kisasa kisutu, Hospitali ya Buguruni, Barabara ya Kiwalani Pamoja na Barabara ya Gerezani ambayo ni miradi mkakati.

Amesema mradi wa Ujenzi wa hospitali ya Wilaya inategemewa kukamilika mwezi June mwaka huu ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kukahakikisha anaendelea kuusimamia vyema.

" Kwanza kabisaa nampongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa kusimamia vyema ujenzi wa hospitali hi ya Kivule Kasi wanayoenda nayo Ni nzuri na matumaini yangu Hadi kufikia June 30, mwaka huu utakuwa umeisha" Amesema Makonda.

 Ameongeza kuwa miradi yote hiyo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwa lengo la kuwasaidia wanyonge ambao Ni wananchi wa hali ya chini.



Amesisitiza kwamba Rais John Magufuli anataka kuona huduma zinamfuata mwananchi na siyo mwananchi anaifuata huduma na kuongeza kwamba hospitali hiyo itatumika kwa wananchi wote ambao walikuwa wakienda  kufuata huduma katika Hospitali  ya Amana ambao wanaoshi maeneo hayo.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo  amesema watu waache dhana kwamba Kuna watu wanaotumia wanyonge kwa manufaa yao binafsi kwani Katika Serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya kuwainua na kuwatetea wananchi wanyonge.
Share:

Udhamini wa NBC wang’arisha shindano la Shika Ndinga jijini Dodoma

Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kati, James Ndimbo, akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa mkazi wa Dodoma, Twaha Saleh aliyojishindia katika kampeni ya Shika Ndinga inayodhaminiwa na benki hiyo na kuandaliwa na kituo cha redio cha EFM. hafla hiyo ilifanyika jijini Dodoma hivi karibuni. 
Washiriki wa Shindano a Shika Ndinga Upande wanaume wakichuana ili kumpata mshindi wa shindano hil lililodhaminiwa na Benki ya NBC na kufanyika mjini Dodoma hivi karibuni. Twaha Saleh alishinda na kuzawadiwa zawadi ya pikipiki.
Washiriki wa Shindano a Shika Ndinga Upande wanawake wakichuana ili kumpata mshindi wa shindano hil lililodhaminiwa na Benki ya NBC na kufanyika mjini Dodoma hivi karibuni. Sarah Ntenga  alishinda na kuzawadiwa zawadi ya pikipiki.
Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliohudhuria katika shindano la Shika Ndinga wakimsiliza mfanyakazi wa NBC kitengo cha mauzo akiwaeleza kuhusu huduma za kibenki zitolewazo na benki hiyo na jinsi wanavyoweza kufungua akaunti ya Fasta ya NBC kwa gharama za kuanzia shs 5000 na kupewa kadi ya ATM aina ya Visa papo hapo.
Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kati, James Ndimbo, akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa mkazi wa Dodoma, Sarah Ntenga aliyojishindia katika kampeni ya Shika Ndinga inayodhaminiwa na benki hiyo. hafla hiyo ikifanyika jijini Dodoma hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kati, James Ndimbo, akiungumza na umati wa watu uliojitokeza katika shindano la Shika Ndinga linalodhaminiwa na benki hiyo mjini Dodoma hivi karibuni.
Share:

Thursday, April 18, 2019

RC MAKONDA awataka watumishi wa Serikali kuacha Uzembe, pamoja na fitina kazini




RC Makonda akishiriki Katika ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza Ukonga zinazomaliziwa na  SUMA JKT .


Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam Paul Makonda akimsikiliza Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi  la Magereza  Julius Ntambala, wakati wa hafla ya Mkuu wa Mkoa kwenda kutembelea majengo yanayojengwa kwaajili ya makazi ya askari magereza katika Gereza la Ukonga  jijini Dar  es Salaam, (kulia) ni  Brigedia Jenerali, Charles Mbuge, kutoka Makao Makuu ya JKT,  ambae pia ni Mkuu wa mradi  wa ujenzi wa nyumba za askari magereza  na maofisa wengine kutoka jkt na magereza 



Baadhi ya Majengo yanayojegwa na  Jkt


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka watumishi wote wa Serikali kuacha majungu Pamoja na fitina na badala yake kufanya kazi kwa bidii ili waweze kupandishwa madaraja.

Akizungumza Leo na waandishi wa habari Katika mwendelezo wa Ziara yake Katika mkoa huo  RC Makonda ametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Askari Magereza  Pamoja na maafisa Ukonga yanayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili,ambapo ujenzi huo walipewa SUMA JKT baada ya kampuni ya TPA kusuasua katika kujenga Nyumba hizo.


"Watumishi wa Serikali tunapasawa kuacha uzembe ,Tuache majungu tufanye kazi tukiacha hayo na kufanya kazi tutafika mbali hata ukitaka kupandishwa cheo fanya kazi kwahiyo Kama Kuna mtumishi yeyote anatamani kupanda daraja ndani ya serikali afanye kazi na kazi yake itamsemea" Amesema Makonda.

Amesema watumishi wengi wa Serikali wamekuwa na fitina na uzembe Katika kazi Jambo linalopelekea kuchelewa kwa maendeleo Katika nchi na hata wengine kushindwa kupanda madaraja.

Aidha ametoa pongezi kwa Mkuu wa Oparetion ya ujenzi huo Bregidia Mbuge kwa kusimamia vyema ujenzi huo ambao unaenda vizuri ambapo Amesema mradi huo utakuwa ni chachu  ya kuongeza kazi nyingine zaidi  kwa SUMA JKT.

Pia RC Makonda amesema lengo la Ziara hiyo Ni kuona maendeleo ya Miradi na kuhamasisha zaidi na mpango kabambe unaochelewesha maendeleo ya wananchi hivyo amezitaka kampuni nyingine kujifunza kutoka kwa wanajeshi ili kufikia malengo ya serikali kukuza maendeleo Katika nchi.


Katika hatua nyingine RC Makonda amemwomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuangalia kwa jicho la tatu mradi wa NSSF  uliopo kata ya Toangoma Wilaya ya Temeke,ambao umekaa kwa muda mrefu bila kuendelezwa hivyo ameomba Majengo hayo yakabidhiwe kwa Suma Jkt ili yaweze kuendelezwa.

"Katika Ziara yangu hii nimeweza kuona Majengo ya NSSF yaliyojengwa  tokea 2004  nitumie fursa hii kumwomba Mhe. Rais awakabidhi wanajeshi kwani huu Ni mradi mkubwa ulioachwa kwa takribani miaka 15 Sasa bila kufanyiwa kazi yoyote na kuonekana kutokuwa na tija yoyote kwa taifa" Amesema Makonda.

Amebainisha kuwa Majengo Yale yanaweza kusaidia watumishi, na wanaweza kulipa hata gharama kidogo na kuweza kuchangia Pato la taifa kwa kupitia Kodi hivyo amemwomba Mhe. Rais aweze kufanya linalowezekana kuhusu Majengo hayo.
Share:

Wednesday, April 17, 2019

RC MAKONDA AIPAISHA WILAYA YA TEMEKE KWA KUFANYA VIZURI KATIKA UJENZI WA MIRADI

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makinda akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo (kulia) wakiwa kwenye Ziara Katika Manispaa hiyo ya Ukaguzi maendeleo ya Miradi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva,  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Chaurembo,  wakimsikiliza DMO Manispaa ya Temeke Dr. Gwamala  Mwabulambo (kulia) akitoa maelekezo ya mradi wa Afya Katika manispaa hiyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kukagua miradi mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akizungumza Katika Ziara hiyo


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amemuagiza Mkurugenzi wa TAKUKURU Mkoa huo kufanya uchunguzi wa utaratibu wa upatikanaji wa tenda kwenye miradi ya DMDP baada ya kubaini matumizi mabaya ya fedha za serikali katika miradi hiyo.

Amesema haiwezekani kuona Kilomita Moja ya Barabara ya DMDP Wilaya ya Kinondoni inajengwa kwa Shilingi Billion 2.7 wakati kwa Wilaya ya Temeke barabara kama hiyo inajengwa kwa shilingi Milioni 900.  

RC Makonda amebaini madudu hayo wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kupitia fedha zinazotoka Serikali Kuu, Halmashau na pesa za wahisani ambapo amekwazwa na matumizi mabaya ya fedha za mkopo kutoka Bank ya dunia.

Aidha amesema kuwa Barabara  za DMDP zimekuwa zikijengwa kwa kiasi kikubwa cha pesa kuliko zile za TANROAD ambazo kwanza zina ubora mkubwa, uwezo wa kubeba mzigo mkubwa na pia ni Pana.

Katika ziara hiyo  ametembelea miradi ya Ujenzi wa Barabara,Hospital na Shule ambapo ameipongeza Manispaa ya Temeke kwa kusimamia vizuri miradi ya Maendeleo na kuwataka kuongeza kasi.
Share:

Legal Services Facility Appoints a New CEO

The Legal Services Facility (LSF) yesterday announced the appointment of Ms.Lulu Ng’wanakilala as its new Chief Executive Officer. In assuming this role, she replaces Kees Groenendijk who led the organization since its inception in 2011.
Ng’wanakilala, who holds a Masters’ Degree in International Law and Human Rights from the University of Liverpool in the United Kingdom and a Bachelor of Law from the University of Dar es Salaam, will among other things oversee ongoing institutional reforms at LSF designed to broaden legal aid provision in order to continue to enable millions of poor women and men in Tanzania to access legal aid services.
She assumes leadership of the non-profit organization that to date has facilitated the active presence of paralegals who work to provide free legal aid and education in all districts of mainland Tanzania and Zanzibar while also financially and technically supporting regional mentor organizations that provide oversight to the paralegals, as well as a variety of other implementing partners.
In anticipation of the new CEO and reflecting on LSF’s work over the last eight years, Groenendijk, the outgoing CEO, said: “From its very start with enabling support of development partners DANIDA and DfID and the government, LSF’s mission has been to establish an environment where access to legal services for poor people, particularly women, is both easy and reliable. To achieve this, we have created a large network of around 3,000 active paralegals across the country whose commitment interprets into visible positive changes to the lives of marginalized people. Of equal importance is that LSF works with many civil society organizations and the government to effect policy and law reforms to ensure that justice remains a paramount attribute of everyday lives of Tanzanians. The new CEO will find a vibrant, focused organization that pursues its vision with vigor and resolve”.
“Ng’wanakilala brings into LSF fresh impetus in terms of innovative and inspirational leadership, as well as broad experience and knowledge in vital disciplines and capacities that are crucial for moving this organization forward,which makes her the ideal person to occupy the helm of LSF”, Groenendijk added.
In welcoming the new CEO, LSF’s Board Chairperson Dr. Benson Bana pointed to the dynamic environment of the provision of legal aid services around the country saying: “Guaranteeing sustainable legal aid services is at the core of what defines LSF’s mission. Over these few years this organization has transformed the lives of countless ordinary citizens while putting emphasis on uplifting women who are traditionally less advantaged. LSF through active cooperation from the government continues to ensure the availability of legal aid services to everyday, ordinary people free of charge. Our incoming CEO will connect with these people and her wealth of experience will help steer LSF to expand opportunities for even more people to benefit from our dedication to access to justice”. 
Prior to her appointment to LSF, Ng’wanakilala served in various capacities including as Chairperson of the White Ribbon Alliance for Safe Motherhood in Tanzania (WRATZ), Steering Committee Member of the Leading Safe Choices Project (LSC), Board Director of Tanzania Women of Achievement (TWA) and Founder and Board Member of Tanzania Centre for Communication and Development (TCDC). She has played a vital role in policy reforms and technical working groups at the coordination, facilitation and participatory levels including in the National Poverty Reduction Strategy (MKUKUTA). Ng’wanakilala is also a member of the Tanganyika Law Society (TLS).
Ng’wanakilala’s appointment formally commences on 1st May, 2019.
Share:

Tuesday, April 16, 2019

RC MAKONDA AWATAKA MADIWANI KUFANYA KAZI KWA UZALENDO.




Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka madiwani Manispaa ya Ilala kusimamia na kupitisha shuguli za Miradi ya maendeleo bila kukwamisha wala kuichelewesha kwa kuendekeza mivutano kwani lengo la miradi Ni kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Rc Makonda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kudai kuwa kumekuwa naucheleweshaji wa miradi kwa maslahi  binafsi na kuelekeza ofisi ya Katibu tawala mkoa kuhamisha watumishi na wakuu wa Idara wanao kwamisha kazi hizo.

Aidha amepongeza kwa kuanza kwa ujenzi wa soko la Kisutu na machinjio ya kisasa ya Vingunguti baada ya kukwama.

"Miradi hii ya kimkakati tumepewa fedha, naomba tuisimamieipasavyo ili tutatue kero zilizopo Katika halmashauri zetu" Amesema Makonda.

Amewataka  madiwani hao kuacha mivutano  na kuongeza bidii ya kusimamia miradi ilikuokoa fedha za walipakodi na kumuagiza Mkurugezi kufanya maamuzi ya kumpa kazi ya kujenga mifereji ya Maji ya mvua Mkandarasi ambaye atafanya ujenzi haraka iwezekanavyo.

"Jambo lingine ambalo linatukwamisha pia ni kutoaminiana naomba tuaminiane ili mambo yaende naomba kama mtakwama nipo muda wote nipigieni  simu wala haihitaji kutuma barua"Amesema.

Aidha amesema wakuu wa Idara wanaokwamisha maendeleo Hadi kufika May 30, mwaka huu,wawe wamamishwa ili kuepusha migongano na mivutano inayotokea hivyo amewataka kuelekeza nguvu kwa Pamoja ili kuhakikisha miradi haichelewi Tena.
Share:

Monday, April 15, 2019

RC MAKONDA AKAGUA MIRADI MBALIMBALI KINONDONI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda(Katikati) Pamoja na watendaji wa Wilaya ya Kinondoni wakiwa Katika Ziara ya Ukaguzi wa miradi mbalimbali Katika Wilaya hiyo.


 RC Makonda akikagua mitaro ya maji inayojenga Tandale 






 Baadhi ya mafundi wakiendelea na Ujenzi wa Soko la Magomeni Usalama Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Paul Makonda amefurahishwa na Kasi ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Katika Wilaya ya kinondoni ambapo mpaka kufikia Sasa utekelezaji wake unaenda vizuri.

Ikiwa Ni mwendelezo wa Ziara yake, Leo April 15, RC Makonda ametembelea miradi mbalimbali Katika Manispaa ya Kinondoni ambapo lengo la Ziara hiyo Ni kuona Kasi ya utekelezwaji wa ujenzi Katika miradi hiyo ambayo ni miradi Katika sekta ya Afya, Barabara ambayo imetolewa fedha kutoka Katika Serikali.


RC  Makonda ametembelea ujenzi wa Soko la Magomeni,ujenzi wa kituo Cha Afya kigogo ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibunii, Soko la Sinza, Pamoja na ujenzi wa Barabara ya Barafu Mbulahati,  ambapo amewataka wakandarasi kufanya kazi zao kwa kuzingatia ueledi.

Amesema wakandarasi wamekuwa wakifanya kazi bila kuzingatia viwango Jambo linalopelekea barabara kuwa mbovu baada ya muda mchache, ambapo amesema wapo waliofungiwa kufanya kazi Katika mkoa huo, na wengine kutakiwa kurudia ujenzi wa barabara kwa fedha zao wenyewe.


Aidha amemtaka Mkuu wa Wilaya ya hiyo kuhakikisha anaendelea kusimamia kikamilifu miradi yote ili iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa na kuweza kutatua kero na adha zinazowakumba wananchi.

Pia amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kushughulikia changamoto za malipo kwa wa Vibarua rwanaofanya kazi katika miradi hiyo huku akiweka sawa mailpo halali wanayotakiwa kulipwa kuwa ni kiasi cha shilingi 12,500 na si chini na hapo.
“Tuna matumaini makubwa sana kutokana na kasi wanayoenda nayo na nampongeza sana DC kwa kazi anayoifanya, barabara ya kituo cha simu 2000 pia inaendelea vizuri na kuna kipande cha mita 250 kimechukuliwa na TANROADS kwa jailli ya kuunganisha na ujenzi wa barabara ya Ubungo hivyo wananchi wakiona kinachelewa wasijiulize kwa Nini hii Ni kwamba tunataka kuunganisha na ujenzi wa barabara ya juu inayojengwa ya Ubungo" Amesema Rc Makonda.
Ziara ya kukagua miradi ndani ya Mkoa huo bado zinaendelea ambapo siku ya kesho RC Makonda ataendelea na ziara katika wilaya ya Kinondoni

Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive