A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, March 13, 2020

Wafanyakazi wanawake wa Jubilee Insurance na Jubilee Life insurance waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kutoa misaada Hospitali ya Mwananyamala

Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, Rose Musa (wa tatu kushoto), akipokea msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike vilivyotolewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance na Jubilee Life Insurance kwa kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana. 
Wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Bima ya Jubilee na Jubilee Life pamoja na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala wakionyesha ishara maalumu ya kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani 2020 isemayo ‘Wanawake katika Mshikamano Tutaendelea Mapambano’ wapolitembelea hospitalini hapo kutoa msaada  wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya matukio yao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
Ofisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Jubilee Insurance, Grace Tupa (kushoto), na mwenzake kutoka Jubilee Life Insurance, Doreen Offen Martin (kulia), wakikabidhi msaada wa shuka na vitu vingine kwa mmoja wa wazazi aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, Tatu Hashim wakati wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo wakitembelea hospitalini hapo kutoa msaada  wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi hiyo hospitali hapo ikiwa ni sehemu ya matukio yao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
Ofisa Utumishi na Utawala wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, Mansour Anchi (kushoto), akizungumza wakati wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance na Jubilee Life Insurance wapolitembelea hospitalini hapo kutoa msaada  wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya matukio yao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance, Angela Tungaraza (kushoto), na Ofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Baraka Mosha (kulia), wakikabidhi msaada wa shuka na vitu vingine kwa mmoja wa wazazi aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, Tatu Hashim wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo wakitembelea hospitalini hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi hiyo hospitali hapo ikiwa ni sehemu ya matukio yao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive