Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (katikati), akizungumzia maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo mbele ya waandishi wa habari na wageni wengine waalikwa. Katika hafla hiyo. Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilimtangaza msanii Diamond Platnumza kuwa Balozi mpya wa Coral Paints.
Balozi Mpya wa Rangi za Coral, Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz akiimba wimbo, maalum kuhamasisha matumizi ya rangi ya kampuni hiyo wakati Kampuni ya Insignia Ltd ikimtangaza kuwa balozi sambamba na maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (kushoto), na Balozi Mpya wa Rangi za Coral, Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz (kushoto kwake), wakishangilia katika hafla ambayo kampuni hiyo ilitangaza kuadhimisha miaka 30 tokea kuanzishwa kwake nchini na pia kumtangaza Diamond kama balozi wao. Wengine ni wawakilishi kutoka Coral Paint na Wasafi Media. Hafla hiyo ilifayika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (katikati), akizungumzia maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo mbele ya waandishi wa habari. Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilimtangaza msanii Diamond Platnumz kuwa Balozi mpya wa Coral Paints.
Na Mwandishi Wetu,
KAMPUNI ya rangi ya Coral Paints imeadhimisha miaka 30 tangu ilipoasisiwa huku ikijivunia ushirika wake katika kukuza uchumi wa wananchi na taifa zima kwa kuwainua mamia ya wajasiliamali nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Kishan Dhebar, alisema wengi miongoni mwa wajasirimali hao kwa sasa ni mawakala wakubwa wa Coral Paints ndani na nje ya nchi.
“Wapo ambao tulianza nao miaka 30 iliyopita na tumekuwa tukitumia takriban Sh. 100 milioni kila mwaka kwa ajili ya kuwainua wajasiriamali wa Tanzania. Hadi sasa tuna takriban mawakala 1,500 ndani na nje ya nchi,” alisema Dhebar.
Dhebar alisema Coral Paints katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Moshi ambako ndiko kampuni hiyo ilikozaliwa mwaka 1990, ikiasisiwa na Watanzania kabla ya kupanuka na kuwa kinara katika soko la rangi, ikichagizwa na kauli mbiu ya ‘Kupamba na Kusherehekea’.
Akizungumzia mafanikio ya kampuni kwa miaka yake 30, mmoja wa wafanyakazi, Amani Mosha, alisema iikuwa ni miaka ya kujivunia kutokana na ubora wa bidhaa wanazozalisha na kuziingiza sokoni.
“Bidhaa zeu ni bora na zenye mng’ao unaodumu kwa muda mrefu na kukidhi matakwa ya wateja ikionyesha thamani halisi ya nyumba au garii,” alisema Mosha.
Awali Dhebar alimtambulisha msanii maarufu nchini, Diamond Platinum kuwa Balozi wa Chapa ya Coral Paints, akisema kwa kuwa wao huzalisha bidhaa bora, ndio maana wamemchagua mtu bora kushirikiana nao.
Diamond, kwa upande wake aliahidi kutoiangusha kampuni hiyo na kwamba atatumia kipaji chake kusambaza ‘simulizi ya kila ukuta’ kama ilivyo kauli mbiu mpya ya Coral Paints.
“Nitaanza kwanza kwa kuipamba Tandale. Nyumba ambazo hazijapakwa rangi tutaipaka rangi za Coral ili baadate tusherehekee,” alisema Diamond.
0 comments:
Post a Comment