Na Mwandishi wetu,
Nabii Suguye wa Kanisa la Huduma ya Upatanisho (WRM) lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga, jijini Dar es salaam, jumapili ya leo amewafundisha maelfu ya waumini waliohudhuria Ibada ya leo kanisani hapo iliyokuwa maalumu kwaajili ya Unabii wa mtu mmoja mmoja na Maombi ya Mapatano juu ya Masharti ya kupelekea maombi yako kujibiwa na Mungu.
“Watu wa Mungu tumekuwa watu wa kuutafuta uso wa Mungu juu ya maitaji yetu lakini wengi wetu majibu yamekuwa hayapatikani na kuanza kujiuliza kama kweli Mungu yupo lakini siri ni kuwa wamefeli kufata kanuni za Mungu za Maombi”
“Ukitaka maombi yako yajibiwe yakupasa uwe na Imani ya Kiungu; Kuna Imani ya kibinadamu lakini pia kuna imani ya Kiungu.”
Alisema Nabii Suguye na kunukuu maandiko kutoka katika kitabu cha Warumi 4:17 “(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.”
“Imani ya Mungu ni kuyaleta mambo yasiyokuwepo kana kwamba yamekwisha kuwepo. Kama unaona umaskini imani ya Mungu inaona Utajiri, kama unaona haiwezekani Imani ya Mungu inaona kuwezekana.”
Nakuongeza kwa kunukuu neno kutoka kwenye waraka wa Waebrania 11:3 “Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.”
“Wengi wetu tunafeli kwakua tunashindwa kuifanyia mazoezi imani. Imani sio tu ya mdomoni kwa kusema namjua Mungu, imani inatakiwa itendewe kazi maandiko yanasema imani pasipo matendo imekufa ndani yake.”
Nabii Suguye aliendelea kusema “Ili maombi yako yajibiwe usiache KUOMBA. Neno linasema msijisumbue kwa lolote Bali kwa kusali na kuomba. Katika kuomba unatakiwa kutamka mambo ambayo unayataka bila kumwekea Mungu mipaka wala mashaka kwakua mashaka huzuia Maombi kufanikiwa.”
“Unapoomba usiombe kwa kumuwekea mipaka Bwana ya kukubariki na kukufanyia muujiza. Wengi tumekua hatujibiwi kwakua tunamwekea Bwana mipaka tunapokua tunaomba. Unapopokea majibu ya Daktari na Ukaanza kuomba usizitazame taarifa za daktari unapofanya maombi amini kuwa Mungu anauwezo wa kufanya zaidi ya wanachokiwaza wanadamu.” Alisema Nabii.
“Mashaka ni hatari katika maisha ya mwamini, Mungu anataka tuwe majasiri tuliojaa imani tunaojua wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea. Usikubali Mashaka ipoteze Baraka zako, simama na Mungu wakati wote mashaka isipate nafasi kwako.” Aliongeza Nabii Suguye.
Nabii Suguye aliendelea kusema kuwa “Unatakiwa kuamini kuwa Mungu yupo na humjibu kila amtafutaye, ndio Mungu huangalia imani yako hivyo unapoomba, kuwa na Imani ya kupokea.
0 comments:
Post a Comment