Catherine Kahuka (kushoto) na Gloria Wangeleja (kulia), wawakilishi kutoka taasisi ya PLPDF kupitia Shirika la Uhifadhi Mazingira Daniani (WWF), ofisi ya Tanzania wakipanda mtiti.
Na Asha Mwakyonde
SHIRIKA la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), ofisi ya Dar es Salaam Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Vodacom Tanzania imepanda miti mia moja na kuwatembelea akina mama waliojifungua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8, kila mwaka.
Upandaji miti huo ulienda sambamba na uchangiaji damu na utoaji zawadi kwa watoto waliozaliwa hospitalini hapo ikiwa ni kujumuika pamoja na akina mama hao katika siku hiyo ya wanawake duniani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hospitalini hapo mara baada ya kufanya shughuli hizo Meneja Mawasiliano wa WWF, Joan Tanisa amesema kuwa shirika la uhifadhi mazingira kupanda miti ni moja kati ya kazi zao za msingi.
Joan amesema mazingira yakiwa mazuri mama mwenye mzigo wa mkubwa wa kuilea familia yake anaweza kupata nafuu na kwamba miti inapopandwa na kustawi vizuri kutakuwa na upatikanaji wa maji ya kutosha na mama huyo hatapata shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Amesema kuwa mwanamke ni kiungo katika suala la uhifadhi wa mazingira kwani shughuli nyingi anazozifanya zinahusiana na mazingira na kwamba ana nafasi ya kubwa ya kuelimisha familia yake juu ya uhifadhi huo.
"Kwa wanawake wenzetu wa vijijini wabaolima, wanaokwenda kutafuta kuni na ndio wanaohudumia familia hivyo ndio mwalimu wa kwanza wa kuweza kutoa elimu ya uhifadhi mazingira,"amesema Joan.
Ameongeza kuwa wamepanda miti maeneo mbalimbali hapa nchini hivyo wameona wafanye kitu gani ambacho kitangusa mwanamke moja kwa moja katika yale ambayo anayafanya kila siku.
Naye Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Taasisi ya Vodacom Sandra Oswadi amesema taasisi hiyo ni ya kujitolea kwa jamii na kwamba wamejumuika na akina mama hao waliojifungua kwa kupanda miti na kutoa zawadi kwa watoto.
"Siku hii tumekuja kupanda miti ambayo imetokana na mkakati wetu wa miaka mitatu wa kutunza mazingira. Kwa mwaka wa kwanza tumedhamiria kupanda miti 70,000 ambao unaishia mwishoni mwa mwezi huu,"amessema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uunguzi na Ukunga kutoka hospitali ya Nuhimbili - Mloganzila Redemptha Matindi ametoa shukrani kwa WWF na taasisi ya Vodacom kwa kupanda miti na kuungana na wanawake waliojifungua na kulazwa hospitalini hapo.
0 comments:
Post a Comment