Nabii Nicolaus Suguye akisaini moja ya Kitambaa cha muumini wa Kanisa hilo
Na Mwandishi wetu,
KATIKA jambo lililowashangaza wengi, ndani ya Kanisa la WRM lillopo Kivule Matembele ya Pili, Ukonga, jijini Dar es Salaam, Kiongozi na Msimamizi Mkuu wa huduma hiyo, Nabii Nicolaus Suguye ameendesha Ibada ya kutia saini vitambaa vya maelfu ya waumini wa kanisa hilo.
Neno saini limetoholewa kutoka katika neno la kiingereza ‘sign’ ili lifanane na muundo wa Kiswahili na liwe ni neno kamili la Kiswahili na kutumika kama kitenzi na wakati mwengine kama nomino.
Nabii Suguye akionesha dhamiri ya dhati kuhakikisha kila aliyehudhuria Ibada hiyo anamsainia kitambaa chake.
Saini (kitenzi) ni kutoa idhini ili kitendo Fulani kitendeke au kipatikane. Matumizi yaliyozoeleka na kukubaliwa na wengi ni kutoa idhini au kuthibitisha kupatikana kwa kitu au jambo Fulani na mara nyinine ni kwa kuandika jina lako.
Tunatumia neno hili tunapotaka kuweka saini mahali fulani. Ni sahihi kusema kuweka saini na wala siyo kutia saini. Kutia lina maana ya kufanya kitu kiwemo ndani ya kitu kwa mfano nitilie chai badala ya kusema niwekee chai. Kuweka kitu maana yake ni kukitua kitu kama vile kuweka kitabu mezani au kuweka silaha chini.
Msururu wa Waumini ukisubiria kusainiwa Leso zao na Nabii Suguye
Neno sahihi (nomino) lina maana ya kuthibitisha au kuidhinisha kwa jambo kutendeka au kupatikana.
Awali nabii Suguye aliwafundisha maelfu ya waumini wa kanisa hilo umuhimu wa kuthibitishwa na Mungu, “Unapothibitishwa ni rahisi kwako kuomba lolote kwa Yule aliyekuthibitisha na akalifanya”
“Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.” Nabii alinukuu kutoka kwenye maandiko ya Biblia Injili ya Yohana 14:14
“Ninaposaini Leso ya kila mtu aliye hudhulia mahali hapa hii ni Saini ya USHINDI, ninapoisaini mahali hapa imesainiwa mbinguni na kupitishwa kuwa MSHINDI” alisema Nabii Suguye.
Nabii Suguye akiwahubiria maelfu ya waumini waliohudhuria Ibada hiyo
Akifundisha katika Ibada hiyo alisema kupitia tendo hilo la Imani iwe ni fahari kwao kujua kuwa, kuna umuhimu wa kujitakasa na kuwa katika mstari ule Neno la Mungu linatufundisha ili tupate kuthibitishwa nakuwa na hakika ya kupokea yale yote tuyaombayo kwa Mungu.
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Waebrania 11:1
“Kupitia saini hii nakutabiria ukafanikiwe katika kila kitu utakachokwenda kukifanya kwaajili ya Utukufu wa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo.” Alisema Nabii Suguye wakati wa Ibada hiyo.
0 comments:
Post a Comment