Diwani wa Kata ya Kimara Paschal Manota, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi wa kata hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa daraja katika mto Gide uliopo kimara ambapo Daraja hilo litagharimu takribani Shilingi za kitanzania milioni 321 ambapo katika hizo milioni 200 zimetoka kwenye mfuko wa Halmashauri ya Ubungo na hizo nyengine zimetolewa na Wakala wa Barabara za Mijini na VIjijini (TARURA)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi , Mpeha 2000 Ltd Never Black, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi wa kata ya kimara wakati alipokabidhiwa eneo kwaajili ya Ujenzi wa daraja katika mto Gide uliopo kimara ambapo Daraja hilo litagharimu takribani Shilingi za kitanzania milioni 321 ambapo katika hizo milioni 200 zimetoka kwenye mfuko wa Halmashauri ya Ubungo na hizo nyengine zimetolewa na Wakala za Barabara wa Mijini na VIjijini (TARURA)
Msimamizi wa Mradi kutoka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Ubungo Mhandisi Denis Charles akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi wa kata ya kimara wakati alipokabidhiwa eneo kwaajili ya Ujenzi wa daraja katika mto Gide uliopo kimara ambapo Daraja hilo litagharimu takribani Shilingi za kitanzania milioni 321 ambapo katika hizo milioni 200 zimetoka kwenye mfuko wa Halmashauri ya Ubungo na hizo nyengine zimetolewa na Wakala za Barabara wa Mijini na VIjijini (TARURA)
Mkazi wa kata hiyo Mwajuma Mungila, akitoa neno la shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwa kuwatatulia kero iliyodumu kwa muda mrefu zaidi ya miaka kumi.
Wanahabari wakiwajibika wakati wa hafla hiyo Picha zote na Brian Peter
Sasa Ujenzi wa daraja la mto Gide kuanza kujengwa jumatatu baada ya wakazi wa kata hiyo kupata shida ya kutumia njia hiyo kwa muda wa miaka kumi
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkandarasi anaetarajia kujenga daraja hilo Never black amezibitisha kuwa wanatarajia kuanza ujenzi huwo rasmi siku ya Jumatatu Tarehe 30 mwezi huu.
“Tunatarajia kuanza ujenzi haraka iwezekanavyo na tumepewa muda wa miezi mitatu yaani siku 90 lakini tunatarajia kufanya kazi kwa muda wa miezi miwili kama mvua itasimama kunyesha au haitonyesha kwa wingi.
“Daraja litakuwa na urefu wa mita kumi na moja na litakuwa la njia mbili ambalo lita ghalimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 321Daraja hilo litaweza kupitisha magari ya uzito wa tani kumi pamoja na njia ya watembea kwa miguu” anasema Black.
Kwa upande wa Diwani wa Kimara Baruti, Paschal Manota, anasema Halmashauri imetoa sh milioni 200, na Wakala wa barabara, TARURA imetoa milioni 100 kwaajili ya mchango wa ujenzi wa daraja hilo la mto Gide.
“Mkandarasi anatakiwa atoe kazi kwa wananchi wa eneo la baruti na makoka asipewe mtu wa kutoka mbali na eneo hili la ujenzi wa daraja ili lijenge kwa wakati.