A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, January 30, 2020

KAMPENI YA USAFI YA OMO NG’ARISHA YAZINDULIWA

Umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofurika katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam jana, kushuhudia uzinduzi rasmi wa Kampeni usafi ya OMO Ng'arisha Festival wakifuatilia matukio ya uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Unilever Tanzania, David Minja (wa nne kushoto), akikata utepe kuzindua kampeni ya kitaifa ya usafi wa iliyopewa jina la Omo Ng'arisha Festival katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam jana.
Wasichana wa promosheni wa Kampeni ya OMO Ng'arisha festival, wakishika mifuko yenye sabuni za Omo kunogesha uzinduzI rasmi wa kampeni ya miezi sita ya usafi iliyopewa jina la OMO Ng'arisha Festival katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Unilever Tanzania, David Minja, akizungumza na umati wa watu uliojitokesa katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam jana kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya usafi iliyopewa jina la OMO Ng'arisha familia katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa Jiji la Dar e Salaam wakichangamkia kununua sabuni za OMO wakati wa uzinduzi wa kampeni ya OMO Ng'arisha Festival jijini humo jana.
Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam akisikiliza maelezo kuhusu ubora wa sabuni ya OMO kutoka kwa wasichana wa mauzo wa bidhaa hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya OMO Ng'arisha Festival jijini Dar es Salaam jana.
Hapa wakionyesha jinsi ya ufuaji bora wa nguo kwa kutuma sabuni ya OMO ili kupata matokeo bora. Hapo ni katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam kwenye wa Kampeni ya OMO Ng'arisha Festival.
Balozi wa Kampeni ya OMO Ng'arisha Festival, msanii nguli wa muziki wa taarabu nchini Tanzania, Bi. Isha Mashauzi akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Msani mahiri wa muziki wa singeli, Seif Mwinjuma 'Sholo Mwamba' akikonga nyoyo za maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofurika katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Dar es Salaam jana kushuhudia uzinduzi rasmi wa Kampeni ya OMO Ng'arisha Festival.


UNILEVER TANZANIA Kampuni inayotengeneza bidhaa mbalimbali leo inazindua kampeni maalumu ya usafi kwa kipindi cha miezi sita iitwayo ‘OmoNg’arisha Festival’ itakayofanyika Tanzania nzima ikiwa na lengo la kuhamasisha faida, ubora na matumizi sahihi ya sabuni bora ya Omo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Jijini Dar es Salaam leo, Meneja Masoko wa bidhaa ya Omo, Bi. Upendo Mkusa alisema ni matumaini yao kwa kupitia kampeni hiyo jamii itatambua matumizi sahihi ili kupata matokeo yanayotarajiwa.

“Ni matumaini yetu watanzania watatumia sabuni ya Omo kwa usahihi kutokana na ukweli kuwa Omo Fast Action na Omo Extra Fresh ni bora katika kupambana na uchafu kwani ina nguvu zaidi ya mara 10 kuliko sabuni za kawaida na ni ukweli kuwa ukitumia Omo kufulia nguo za familia yako wewe na nguo za familia yako mtang’aa, nguo zako ziking’aa wewe na familia yako mtang’aa, pia tunataka kuona watanzania waking’aa,” alitanabaisha Bi. Upendo.

Akizungumza zaidi kuhusu kampeni hiyo, Bi.Upendo meneja masoko wa Omo alisema mara baada ya uzinduzi huo, kampeni hiyo itaendelea katika mikoa ya Dodoma, Dar, Mwanza, Arusha, Moshi na Mbeya. Kuifanya kampeni hii kuwa yenye bashasha na mvuto, Unilever Tanzania inamtangaza Msanii maarufu nchini Tanzania, Bi. Isha Mashauzi kuwa  Balozi wa Kampeni hii ya Omo Ng’arisha, ambaye atakayeshiriki katika matukio mbalimbali katika kampeni hii ikiwemo michezo ya kufurahisha na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Kampeni itashirikisha timu ya promosheni ya Omo kwa kupita mlango kwa mlango majumbani, kwenye maeneo ya wazi na katika sehemu za biashara kuijulisha jamii juu ya ubora, faida na matumizi sahihi ya OMO, ambayo ni moja ya bidhaa kubwa zaidi ya Unilever.

Bi. Upendo meneja huyo alisema pia, wameandaa zoezi maalumu la kuwatambua Wanawake Wajasiriamali 10 katika kila mkoa watakapofanya kampeni hiyo na kuwapa zawadi itakayowasaidia kuboresha biashara zao hivyo kuwafanya kung’aa.“Ni imani yetu wanawake hawa miongoni mwao kuna wenye biashara ndogondogo, tutawatambua na kuwapa zawadi. Ni matarajio yetu utambuzi huu utaleta tija na kuwa kichocheo katika utendaji wao na kukuza biashara zao’’, alimalizia Bi Upendo Mkusa. 

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Unilever Tanzania, Bw. David Minja, alisema “Unilever inatambua na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuendeleza uchumi wa viwanda na katika kuwaletea watu wake maendeleo na kwa kuonyesha uungaji wetu mkono, timu yetu ya kampeni katika mikoa hiyo tuliyoitaja itatembelea katika mahospitali ambako tutaonyesha moyo wa kujali kwa kutoa msaada wa sabuni za Omo kwenye hospitali ya mikoa hiyo tukiongozwa na balozi wetu wa Omo Bi. IshaMashauzi.

“Katika kuendelea kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali ya awamu ya tano, tutakuwa mstari wa mbele kuhimiza jamii na wananchi kufanya usafi wa mazingira yao, na nina furaha kwamba kupitia kampeni ya Omo Ng’arisha katika kila mkoa tutakaopitia, timu yetu ya Omo Ng’arisha itashiriki katika shughuli za usafi kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa huo,” aliongeza Bw.Minja.

Aidha Mkurugenzi Mkuu huyo alisema Unilever inatoa shukrani kubwa kwa ushirikiano inaoupata kutoka mamlaka mbalimbali za kibiashara na kiserikali hapa nchini. “Tunaipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuweka mazingira wezeshi na juhudi yake katika kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazoikabili jumuiya ya wafanyabiashara. Kwa upande wetu tunaahidi kuongeza ubora wa bidhaa zetu kuhakikisha zinakidhi mahitaji ya wateja wetu, tukifanya biashara kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote zilizopo huku tukiangalia namna bora zaidi ya kuinufaisha jamii ya watanzania,” alisema.    

Licha ya bidhaa ya Omo ikiwa na aina mbili za Omo Fast Action na Omo Extra Fresh yenye nguvu mara kumi zaidi, Unilever inazo bidhaa nyingine kama; Sunlight-sabuni ya unga, inayotakatisha vizuri, yenye manukato na kulainisha ngozi, mafuta ya mgando na losheni ya Vaseline yenye uwezo wa kutunza ngozi,Vim-sabuni ya kusafishia ambayo ni kiboko ya uchafu wa nyumbani,  AXE-sprei ya mwili kwa wanaume inayokuacha na harufu nzuri kwa zaidi ya masaa 48 na Royco mchuzi mix, kiungo cha chakula chenye viungo asilia 16 kwa kuongeza ladha murua ya chakula.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive