A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Tuesday, January 21, 2020

BILLION PAINTS YATOA NDOO 500 ZA RANGI KATIKA KUBORESHA ELIMU DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wanahabari wakati alipokwenda kutembelea kiwanda cha utengenezaji wa rangi cha Billion Paints
Meneja Masoko wa  kampuni ya utengenezaji wa Rangi cha Billion Paints Ruth Muruve, 
akizungumza na wanahabari wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alipokwenda kutembelea kiwanda hicho.
 
Januari 21 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepokea ndoo mia tano kutoka katika kampuni ya utengenezaji wa rangi cha Billion Paints ambazo zimeelekezwa katika shule jijini humo ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho na kukabidhiwa rangi hizo Makonda amesema kuwa kiwanda hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2017 na kijana mtanzania aliyeitikia wito wa Rais Magufuli katika suala la ujenzi wa viwanda matunda yameanza kuonekana na wamekuwa sehemu ya ushiriki wa shughuli za kijamii ikiwemo elimu.

Makonda amesema kuwa rangi hizo zitasaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 380 kwa uwiano wa wanafunzi 50 kwa darasa moja unaendelea katika Wilaya ya Temeke ambako wanafunzi 5970 wameshindwa kuanza masomo yao kutokana na ufinyu wa madarasa.

"Wanafunzi 5970 waliofaulu walikosa vyumba vya madarasa na kupitia waraka uliotolewa na Wizara ya elimu tunategemea kufikia Machi Mosi wanafunzi  wote watakuwa darasani wakiendelea na masomo, na tunawashukuru Billion Paints kwa mchango huu na kwa kutambua hili tutachora 'Billion' ili kutambua mchango huu" ameeleza.

Aidha Makonda amesema kuwa hadi kufikia sasa shule mpya nne zimeanzishwa, ujenzi wa madarasa na matundu ya choo unaendelea na hiyo ni pamoja na ukarabati wa miundombinu na madawati.

"Ninawaomba wadau na washiriki kama Billion wajitokeze na tushirikiane katika kuimarisha sekta hii adhimu na wazazi hawatachangishwa chochote elimu itatolewa bure kama Rais Dkt. John Joseph Magufuli alivyoelekeza" amesema Makonda.

Vilevile amewashauri vijana kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa imara kama mwanzilishi wa kiwanda hicho alivyothubutu na kuajiri vijana wengine arobaini.

Kwa upande wake Meneja masoko wa kiwanda hicho Ruth Muruve amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kuboresha sekta ya elimu nchini na wametoa rangi hizo ili kutengeneza mazingira bora ya ujifunzaji kwa wanafunzi.

Amesema kuwa kampuni hiyo ya wazawa inazalisha aina saba za rangi na inapatikana kwa gharama nafuu.


Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive