A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Sunday, March 24, 2019

WAKAZI WA MTWARA WAFURIKA TAMASHA LA SHIKA NDINGA

1
 Meneja wa Benki ya NBC,  Kanda ya Pwani, Daudi Mfalla (kushoto) akimkabidhi pikipiki mmoja wa washindi wa kampeni ya Shika Ndinga kwa upande wa wanawake, Mariamu Hamisi wakati wa kampeni hiyo  katika  Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mkoani Mtwara jana. Kulia ni Meneja wa Tawi la NBC Mtwara, Job Nshatsi. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo pamoja na kufahamishwa huduma nyingine za kibeni za benki hiyo.
2
 Meneja wa Benki ya NBC, Kanda ya Pwani, Daudi Mfalla (kulia) akimkabidhi pikipiki mmoja wa washindi wa kampeni ya Shika Ndinga kwa upande wa wanaume, Silvan Gabriel iliyofanyika katika  Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Mtwara jana. Katikati ni Meneja wa NBC Tawi la Mtwara, Job Nshatsi. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao
3
 Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Biashara cha Benki ya NBC, Japhet Fungo (kushoto) akiwaeleza  waendesha bodaboda kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zinzowafaa zitolewazo na NBC wakati wa kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Mkoani Mtwara jana. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.

4
 Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC , Dunstan Lipawaga (kushoto) akizungumza na washiriki wa Shindano la Shika Ndinga Mkoani Mtwara kuhusu huduma za Kibenki zitolewazo na benki katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Mkoani Mtwara jana. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.

5
 Mkazi wa Mtwara, Ismail Sama (kulia), akiweka alama ya gumba ili kufungua akaunti ya Fasta ya Benki ya NBC, katika kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo, mkoani Mtwara juzi. Kushoto ni Ofisa Mauzo wa NBC, Dunstan Lipawaga. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.6
 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Ashura Mchopa (kushoto) akiangalia wakati mmoja wa wakazi wa Mtwara akiweka alama ya dole gumba ili kufungua akaunti ya Fasta ya benki ya NBC katika kampeni ya Shika Ndinga mkoani humo jana.  NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.

7
 Mkazi wa Mtwara, Yakini Suwedi (kushoto), akiweka alama ya gumba ili kufungua akaunti ya Fasta ya Benki ya NBC, katika kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo, mkoani Mtwara jana. Kushoto ni Ofisa wa Benki ya NBC,  Baraka Mponda.  NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.8
 Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Pwani, Daudi Mfalla (kulia), akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliojitokeza katika kampeni ya Shika Ndinga kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi       Majengo, mkoani humo jana. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo na pia kupata huduma nyingine za kibenki zitolewazo na NBC.

9
 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Ashura Mchopa (kulia) akimkabidhi  kadi ya ATM aina ya Visa kwa mkazi wa Mtwara Abduli Ally,  baada ya kufungua akaunti ya Fasta wakati wa kampeni ya Shika Ndinga katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mkoani humo jana.  NBC inadhamini kampeni iliyoandaliwa na Kituo cha Redio cha EFM kwa malengo ya kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.

10
 Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Dunstan Lipawaga (kushoto) akimkabidhi kadi ya  ATM aina ya  Visa  mkazi wa Mtwara, Ismail Sama   baada ya kufungua akaunti ya Fasta  wakati wa kampeni ya Shika Ndinga katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mkoani humo juzi.  NBC inadhamini kampeni hiyo kwa malengo ya kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.
11
 Baadhi ya washiriki wa kampeni ya Shika Ndinga wakichuana ili kumpata mshindi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mkoani Mtwara jana. Kampeni ya Shika Ndinga inayoendeshwa na Kituo cha Redio cha EFM na kufanyika mikoa mbalimbali nchini inadhaminiwa na Benki ya NBC.
12
 Washindi wa Shika Ndinga wa Mkoani Mtwara waliojishindia pikipiki wakipozi kwa picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wa NBC mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Kampeni ya Shika Ndinga inayoendeshwa na Kituo cha Redio cha EFM na kufanyika mikoa mbalimbali nchini imedhaminiwa na Benki ya NBC.
13
Washiriki wakichuana katika mbio za magunia katika kampeni hiyo mkoani Mtwara jana.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive