Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya SCI AMEAA Ltd, Bw. Gilad Kaham, akifafanua jambo
wakati wa uzinduzi rasmi wa Mfumo wa Kidigital (FMAS), unaolenga
kukomesha wizi, upotevu na uchakachuaji wa mafuta na bidhaa za petrol
nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Net-Soft Consult, Bw.
Richard Shirima,
akiongea na wadau kuhusu faida zinazotokana na Mfumo mpya wa Kidigital
(FMAS) wa kudhibiti wizi na uchakachuaji wa mafuta na bidhaa zingine za
petrol katika sekta za Umma na binafsi nchini Tanzania.
Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Net-Soft Consult, Bw.
Richard Shirima (kushoto), akimsikiliza Moja ya Mteja aliehudhulia hafla hiyo (Picha na Brian Peter).
Na Mwandishi Wetu
Kampuni
ya Kimataifa SCI EMAA LTD (SCI) kwa kushirikiana na Kampuni ya Net Soft
Consult-Tanzania jana wamezindua mfumo maalum wa kigitali unaolenga
kukomesha wizi, upotevu na uchakachuaji wa mafuta na bidhaa zingine za
petroli na gesi katika sekta binafsi na umma inchini Tanzania.
Wataalamu
wa teknologia ya habari na mawasiliano wanautaja mfumo huo “Fuel
Management Automation System (FMAS)” kama mwarobaini wa tatizo sugu la
wizi na upotevu wa mafuta katika taasisi, mashirika na makapuni ya sekta
binafsi na ile ya umma, unaosababisha hasara ya mabilioni ya shilingi.
Akiongeza
katika uzinduzi wa mfumo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Net Soft Consult, Richard Shirima, amesema matumizi ya mfumo
huo yapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uendashaji katika makampuni
binafsi na taasisi za serikali, hivyo kuongeza kasa ya ukuaji wa uchumi
wa Taifa.
“Mfumo
huu unakwenda sambamba na sera ya Serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais John Magufuli, inayolenga kupunguza gharama za uendeshaji na
kuongeza tija katika sekta binafsi na ile ya umma--hatimae kuifanya
Tanzania kutimiza ndoto zake za uchumi wa viwanda,” amesema Bw. Shirima.
“Badala
ya kuajiri watu wengi kusimamia matumizi ya mafuta katika shiriki,
kampuni binafsi au ya umma, kazi hii inaweza kufanywa kirahisi sana kwa
kutumia mfumo huu maalum (FMAS),” ameongeza Bw. Shirima.o
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Net-Soft Consult, mfumo huu uwezesha mashirika,
makampuni na taasisi binafsi na za umma, kufahamu kiwango cha mafuta
yanayotumika au yanapaswa kutumika (katika shughuli zao) kwa siku, kwa
wiki, mwezi na mwaka, hali itakayosaidia mashirika na makampuni husika
kuweka mipanga sahihi inayohusu matumizi ya mafuta.
Bw.
Shirima amesema mfumo huu unawezesha wamiliki wa makampuni ya mafuta
kufahamu kiwango cha mafuta yaliogizwa, yaliyouzwa na yaliyobaki katika
vituo vyake vilivyoko nchi nzima, kiwango kinachopaswa kuongezwa katika
vituo husika na wakati gani.
“Kwa
kutumia teknologia hii, makampuni ya kusafirisha mafuta ndani au nje ya
nchi, yanaweza kufatilia magari yaliobeba mafuta na kuhakikisha
yanafika mahali husika, bila kupakuliwa kinyemela njiani, hivyo
kuthibiti wizi na upotevu wa mafuta,” ameongeza.
Katika
sekta ya umma, Shirima amesema teknologia ya FMAS inawezesha taasisi,
mashirika na kampuni ya serikali, kufatilia mafuta yanayoagizwa,
kutumika katika magari na shughuli mbalimbali, kiwango kilichobaki, bila
kupoteza hata “tone” moja la mafuta.
Msululu
wa wafanyakazi wanaosimamia matumizi ya mafuta katika sekta mbalimbali
ya umma, utapungua sana, kwa sababu kazi yote ya usimamizi na ufatiliaji
itafanywa na mfumo maalamu, amesema Andrew Charles, mmoja wa watumishi
wa umma uliohojiwa wakati wa uzinduzi wa mfumo huu.
“Hii
itaiwezesha serikali kusevu fedha nyingi (zilizokuwa zinatumika katika
kudhibiti matumizi ya mafuta) na kuzielekeza fedha hizi katika miradi
mingine ya maendeleo,” ameongeza.
Mmoja
wa wadau wa sekta binafsi, Salehe Mwango, amesema “Kwa kutumia mfumo
huu, mashirika ya umma na binafsi yanaweza kufuatilia kwa karibu kiwango
cha mafuta kinachotumika katika magari yake, kilichobaki na
kinachopaswa kuongezwa, hivyo kukomesha kabisa wizi wa mafuta na bidhaa
zingine za petrol.”
Mbali
na kudhibiti wizi na upotevu wa mafuta, mfumo huu pia unaweza
kuangalia/kufuatilia ubora wa mafuta yanayotumika katika sekta binafsi
na umma, jambo litakalosaidia kuondoa tatizo sugu la uchakachuaji wa
mafuta.
0 comments:
Post a Comment