A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, March 28, 2019

Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC

Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa (kulia), akipeana mikono na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alipomtembelea ofisini kwake akiwa pamoja na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe (kushoto), Dar es Salaam jana.

Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa (kulia), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi pamoja na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe walipomtembelea ofisini kwake, Dar es Salaam jana. 
Share:

Wednesday, March 27, 2019

KAMPUNI YA USAFIRISHAJI MTANDAONI YA LITTLE SASA KUMENOGA

k1
Meneja Mkuu wa Huduma wa kampuni ya usafiri ya Little akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana.
k2
Kutoka kulia ni Jefferson Aluda Meneja Huduma, Meneja Mkuu wa Huduma wa kampuni ya usafiri ya Little na Abbas Mfundo Mkurugenzi Mtendaji wakipiga makofi mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri jijini Dar es salaam jana.
k4
Jefferson Aluda Meneja Huduma Kampuni ya Little akizungumz katika uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
k5
Baadhi ya wadau walioalikwa kwenye uzinduzi huo wakiwa katika picha ya pamoja.k6
Meneja Masoko wa kampuni hiyo Bw. Katimpu Kisessa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo.
k7
Wadau kutoka DSTV kushoto ni Grace Mgaya na Katibu Muhtasi Levina Bandiai wakiwa katika uzinduzi huo.
k8
Hussein Machozi  na bendi yake akitumbuiza katika hafla ya uzinduzi huo
k9
Picha mbalimbali zikionyesha wadau waliohudhuria katika hafla hiyo katika uzinduzi huo.
k10k11
KAMPUNI ya usafirishaji abiria mtandaoni ya Little imezindua huduma ya usafiri kwa Jiji la Dar es Salaam huku ikisema wao wamekuja tofauti na kampuni nyingine zinazoto huduma hiyo na hivyo watakaotumia usafiri wa Little watafurahia huduma bora na nzuri.
Katika kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kila mahali tayari Kampuni ya Little imeshasajili zaidi ya madereva 500 ambapo pamoja na mambo mengine wamehakikishiwa usalama wao ikiwemo kuwa na bima ya afya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana usiku wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo ,mmoja wa Wkurugenzi wa Little nchini Tanzania Abbass Mfundo amesema kabla ya kuanzisha huduma hiyo wameangalia changamoto zilizoko kwenye kampuni nyingi zinazotoa huduma ya kusafirisha abiri na kisha wao kuja tofauti kabisa jambo ambalo linawapa matumaini huduma zao zitakuwa bora.
Amesema kwa watakaotumia usafiri wa Little kuna huduma nne muhimu ambazo watazipata wakiwa safarini.Ametaja huduma hizo ni mteja kuona gharama ya safari yake kila baada ya dakika mbili na hivyo itamuwezesha kujua gharama kadri safiri inavyoendelea.
Amesema kumuwepo na kawaida ya baadhi ya abiria wasiokuwa waamini kuwaonesha abiria wao bei ambayo ni tofauti.”Kuna baadhi ya madereva wana Screen Short bei na kisha anamuonesha mteja huku akijua sio ya wakati huo.Hivyo kwetu dereva hawezi kuonesha bei tofauti na ile halisi kulingana na safari husika,”amesema Mfundo.
Pia amesema kutakuwa na huduma ya kumuwesesha abiria akiwa safarini mwingine anayetaka kujua atafahamu alipo kupitia ‘Safari share’ ambapo ametoa mfano ukiwa safarini mhusika atamuunganisha mtu wake na kisha atakuwa anajua mahali alipo.
Ameongeza huduma nyingine ambayo ni muhimu sana abiria au dereva wanapokuwa na mashaka kila mmoja kwa wakati wake ataweza kutoa taarifa kwa kubonyeza kitufe cha ‘Panic’ ambacho kitatoa taarifa katika kampuni ya ulinzi ambayo Little imeingia nayo mkataba.
Amesema wamefanya hivyo ili kuhakikisha wanaotumia usafiro huo iwe kwa dereva au abiria wote wanakuwa salama na kwamba kupitia huduma hiyo ni rahisi kupata msaada na kama kulikuwa na tatizo la tishio la usalama basi litakuwa limepata ufumbuzi wake.
Wakati huduma nyingine ambayo inapatikana Little na kwingine hakuna ni abiria(mteja) kuwa na uwezo wa kuchagua dereva anayemuhitija kwani kupitia App yao kuna sehemu ambayo utaona picha ya dereva na namba yake ya simu,hivyo kama alikupakia kwa mara ya kwanza na huduma yake ukaifurahia unaweza kumuita tena na kama hukuridhika naye unamkataa.
Pia amesema kwa kampuni ya Little wamekuwa wakisikia malalamiko ya madereva na hasa kuchelewa kulipwa fedha zao kwa wateja wanaotumia kadi,hivyo kwao hata kama dereva atampakia mteja anayelipa kwa kadi hata ikiwa kwa wiki,dereva atalipwa fedha yake siku hiyo hiyo.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Little Katimpu Kisessa amesema katika kuhakikisha pande zote zinanuifa,kampuni yao imeamua kuweka mifumo itakayomuwezesha dereva aliyekuwa kwao kunufaika na kazi anayoifanya.
Amesema mbali ya Little kutoa ajira kwa watanzania wengi kutokana na kuanzishwa kwa huduma hiyo ya usafirishaji,pia wamezingatia usalama wa afya zao na ndio maana mbali ya kupata fedha kutokana na kazi hiyo wamezingatia umuhimu wa madereva kuwa na bima ya afya.
Kuhusu huduma ya Little amesema kwa sasa wameanza na Dar es Salaam na baadae itafuata Dodoma,Mwanza,Mbeya na Arusha huku akisisitiza kuwa Little imekuja kivingine na kwamba huduma ambazo wao wanazo haziko kwenye kampuni nyingine.
“Little hatutaki ujanja ujanja kama ambao unafanywa na wengine.Ndio maana baada ya kupakua App yetu mteja kwa maana ya abiria kila kitu ataona kwenye simu yake ya mkononi.Kuna ile tabia inayoitwa kuchezesha dishi kwa kuonesha nauli ambayo sio ya kweli,huku kwetu hakuna.Ukitaka ku-screen short nauli itakukatalia,” amesema Kisessa.
Share:

Sunday, March 24, 2019

WAKAZI WA MTWARA WAFURIKA TAMASHA LA SHIKA NDINGA

1
 Meneja wa Benki ya NBC,  Kanda ya Pwani, Daudi Mfalla (kushoto) akimkabidhi pikipiki mmoja wa washindi wa kampeni ya Shika Ndinga kwa upande wa wanawake, Mariamu Hamisi wakati wa kampeni hiyo  katika  Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mkoani Mtwara jana. Kulia ni Meneja wa Tawi la NBC Mtwara, Job Nshatsi. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo pamoja na kufahamishwa huduma nyingine za kibeni za benki hiyo.
2
 Meneja wa Benki ya NBC, Kanda ya Pwani, Daudi Mfalla (kulia) akimkabidhi pikipiki mmoja wa washindi wa kampeni ya Shika Ndinga kwa upande wa wanaume, Silvan Gabriel iliyofanyika katika  Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Mtwara jana. Katikati ni Meneja wa NBC Tawi la Mtwara, Job Nshatsi. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao
3
 Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Biashara cha Benki ya NBC, Japhet Fungo (kushoto) akiwaeleza  waendesha bodaboda kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zinzowafaa zitolewazo na NBC wakati wa kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Mkoani Mtwara jana. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.

4
 Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC , Dunstan Lipawaga (kushoto) akizungumza na washiriki wa Shindano la Shika Ndinga Mkoani Mtwara kuhusu huduma za Kibenki zitolewazo na benki katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Mkoani Mtwara jana. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.

5
 Mkazi wa Mtwara, Ismail Sama (kulia), akiweka alama ya gumba ili kufungua akaunti ya Fasta ya Benki ya NBC, katika kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo, mkoani Mtwara juzi. Kushoto ni Ofisa Mauzo wa NBC, Dunstan Lipawaga. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.



6
 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Ashura Mchopa (kushoto) akiangalia wakati mmoja wa wakazi wa Mtwara akiweka alama ya dole gumba ili kufungua akaunti ya Fasta ya benki ya NBC katika kampeni ya Shika Ndinga mkoani humo jana.  NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.

7
 Mkazi wa Mtwara, Yakini Suwedi (kushoto), akiweka alama ya gumba ili kufungua akaunti ya Fasta ya Benki ya NBC, katika kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo, mkoani Mtwara jana. Kushoto ni Ofisa wa Benki ya NBC,  Baraka Mponda.  NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.



8
 Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Pwani, Daudi Mfalla (kulia), akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliojitokeza katika kampeni ya Shika Ndinga kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi       Majengo, mkoani humo jana. NBC inadhamini kampeni hiyo ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo na pia kupata huduma nyingine za kibenki zitolewazo na NBC.

9
 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Ashura Mchopa (kulia) akimkabidhi  kadi ya ATM aina ya Visa kwa mkazi wa Mtwara Abduli Ally,  baada ya kufungua akaunti ya Fasta wakati wa kampeni ya Shika Ndinga katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mkoani humo jana.  NBC inadhamini kampeni iliyoandaliwa na Kituo cha Redio cha EFM kwa malengo ya kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.

10
 Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Dunstan Lipawaga (kushoto) akimkabidhi kadi ya  ATM aina ya  Visa  mkazi wa Mtwara, Ismail Sama   baada ya kufungua akaunti ya Fasta  wakati wa kampeni ya Shika Ndinga katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mkoani humo juzi.  NBC inadhamini kampeni hiyo kwa malengo ya kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wao ambapo wateja wanafungua akaunti ya Fasta na kupata kadi ya ATM ya Visa hapo hapo.
11
 Baadhi ya washiriki wa kampeni ya Shika Ndinga wakichuana ili kumpata mshindi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mkoani Mtwara jana. Kampeni ya Shika Ndinga inayoendeshwa na Kituo cha Redio cha EFM na kufanyika mikoa mbalimbali nchini inadhaminiwa na Benki ya NBC.
12
 Washindi wa Shika Ndinga wa Mkoani Mtwara waliojishindia pikipiki wakipozi kwa picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wa NBC mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Kampeni ya Shika Ndinga inayoendeshwa na Kituo cha Redio cha EFM na kufanyika mikoa mbalimbali nchini imedhaminiwa na Benki ya NBC.
13
Washiriki wakichuana katika mbio za magunia katika kampeni hiyo mkoani Mtwara jana.
Share:

Friday, March 22, 2019

NEW GSMA STUDY: MOBILE SIGNIFICANTLY ADVANCING ECONOMIC AND DEVELOPMENT GOALS IN TANZANIA

Mobile Adding $2.5 Billion in Economic Value to Tanzania Economy
Tanzania’s mobile industry is contributing significantly to the realisation of the country’s economic and development goals, according to a new GSMA report. The new report – Digital Transformation in Tanzania – is launched today at a meeting organised by the GSMA that brings together representatives from Tanzania’s three main mobile operators, Airtel, Tigo and Vodacom.
g02
“Mobile technology is at the centre of Tanzania’s digital transformation, providing access to essential services, increasing productivity, and driving economic growth,” said Akinwale Goodluck Head of Sub-Saharan Africa, GSMA. “Leveraging mobile technology to further advance economic and development goals in Tanzania requires collaboration by all stakeholders, including operators, government and development organisations.
g3
We also require a supportive regulatory environment that encourages investment and innovation, and ensures operators have access to sufficient spectrum in a timely and affordable manner.”

The report highlights four key areas where Tanzania’s mobile industry is making a significant contribution to the country’s transformation into a digital economy and realisation of its development goals:
g04
Access to key services – Mobile operators provide affordable access to life-enhancing services for people in underserved communities. Inclusive and innovative business models have emerged from the convergence of various mobile services, particularly connectivity, mobile financial services, digital identity, and M2M and IoT;
Driving productivity and efficiency – Mobile is driving productivity and efficiency gains in Tanzania’s businesses and public institutions, especially in the agricultural sector;
Contribution to economic growth and social development – In 2016 the total value added generated by the mobile operators alone was around $2.5 billion, equivalent to 5.2 per cent of Tanzania’s GDP. The country’s mobile industry also employs more than 1.5 million people directly and indirectly, equivalent to 2.6 per cent of the population;

Encouraging good governance – Mobile is a key channel for Tanzania’s e-government strategy, with public institutions now using mobile money, SMS and USSD platforms to deliver services, collect payments and engage with the general public.
The new report ‘Digital Transformation in Tanzania’ is authored by GSMA Intelligence, the research arm of the GSMA. To access the full report please visit: ADD LINK
Share:

Barclays Bank Tanzania under Absa Group Limited announces English Premier League #superfansunited campaign winne

Barclays Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (left), makes a phone call to the bank's English Premier League 'superfansunited' campaign grand winner in Dar es Salaam yesterday. The bank's Mikocheni Branch customer, Catherine Arsen, won a fully paid trip to United Kingdom, to spend time with an English Premier League legend and watch a live match on the English Premier League. Other seven winners won a range token prizes.  To his left are BBT Head of Retail Banking, Oscar Mwamfwagasi and Gaming Board of Tanzania Inspector, Bakari Maggid. 




Barclays announces grand winner of superfansunited campaign

By Our Reporter

Barclays Bank Tanzania under Absa Group Limited, one of Africa’s largest financial services providers,
yesterday announced the grand winner   their English Premier League #superfansunited promotional campaign which ended on March 10.

The lucky winner, Catherine Arcene from the bank’s Mikocheni branch in Dar es Salaam, will enjoy a full paid trip to the UK to enjoy a true Clubhouse experience. She is expected to fly to the UK in the first week of May and is scheduled to spend a week there.

Other seven joint runners-up were also announced, who will have token package featuring being put up in one of the classic  hotels in Dar es Salaam, watch  live English Premier League in a superfans clubhouse replica in the city,  cash prize of 300,000 each, a cap and a t-shirt of an  EPL team of their like.

The seven winners, who will convene in Dar es Salaam on April 20 this year,  are Mwanahamisi  Salum, Majid Omary, , Sharifu Bashiru, Yuda Thadey, Frederick Edward  all from Dar es Salaam, Suleiman Nassor from Zanzibar and Godfrey Mollel from Arusha.

The campaign was launched in November 2018 and has run for three months.

Addressing the press yesterday, the Head of Marketing and Corporate Relations, Mr Aron Luhanga, commented, “our lucky winner will travel to United Kingdom, spend time with an English Premier League legend, watch a live match on the English Premier League and have a total new experience for being part of a great #superfansunited campaign”.

He added: “We appeal to all other customers to join Barclays Bank and be part of a great bank. Our focus is to help customers achieve their ambitions in the right way’.

Head of Retail banking, Mr Oscar Mwamfwagasi, “This campaign was opened to all our customers who Bank with Barclays. A customer needed to make five transactions or more using their Barclays card, and get into the draw to stand a chance to win a fully paid trip to United Kingdom to experience the superfansunited  live’,

He added that customers who switch to Barclays have multiple reasons to do so including but not
limited to their being attracted by the bank’s wide range of exciting products and exceptional services from friendly staff.

Share:

Wednesday, March 20, 2019

MultiChoice yatangaza fursa kabambe kwa wadau wa filamu Afrika!

CAPTION 1 Mshana

 Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya MultiChoice Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun mapema leo asubuhi.

CAPTION 2 Mama Fisoo

 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Mama Joyce Fisoo  akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya MultiChoice Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun mapema leo asubuhi.


H01

Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana akizungumza na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Mama Joyce Fisoo  akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya MultiChoice Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun mapema leo asubuhi.

 H02

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Mama Joyce Fisoo  akiwa na Afisa Uhusiano MultiChoice Tanzania, Grace Mgaya wakati wa uzinduzi wa programu ya MultiChoice Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun mapema leo asubuhi.

H3


Baadhi ya picha zikionyesha baadhi ya wadau na waigizaji wa filamu walioalikwa kwenye uzinduzi wa programu ya MultiChoice Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun mapema leo asubuhi.
Jumanne Machi 19, 2019:MultiChoice Tanzania imetangaza  fursa ya kipekee kwa wadau wa tasnia ya filamu Tanzania na barani Afrika kwa ujumla ijulikanayo kama MultiChoice Talent Factory Portaliliyodhamiria kuleta mapiduzi ya hali ya juu katika uaandaaji wa filamu zenye viwango vya kimataifa kutoka barani Afrika.



Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano kutoka MultiChoice Tanzania Johnson Mshana alieleza kuwa programu hiyo ni muendelezo wa program maalum ya iliyodhamiria kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu barani Afrika. MultiChoice Talent Factory ambayo ni progamu mama  ilizinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka jana naimedhamiria kuleta mabadiliko chanya kwenye tasnia ya filamu hapa nyumbani Tanzania na Afrika kwa ujumla. Tulianza kwa kupeleka vijana wanne katika kambi maalum ya mafunzo ya uandaaji filamu katika akademia maalum kule Nairobi nchini Kenya, kisha mafunzo maalum kwa magwiji wa sauti yaliyofanyika mnamo mwezi Januari mwaka huu na hatimaye leo hii tumekuja tena na platform maalum yenye dhamira ile ile ya kuleta mapinduzi katika tasnia ya filamu barani Afrika”, alisema Mshana.



Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fisoo alisema kuwa, anaishukuru sana kampuni ya MultiChoice kwani imekuwa mstari wa mbele katika kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu hapa nyumbani Tanzania. “Binafsi nilishuhudia uzinduzi wa programu ya MultiChoice Talent Factory mapema mwaka jana kule mjini Dodoma na leo hii tunazindua tena sehemu nyingine ya programu hiyo hiyo. Hakika ni fursa ya kipekee na ninapenda kuchukua nafasi hii kuwahamasisha wadau wote waliopo katika Tasnia yetu kuitumia nafasi hii ipasavyo ili kuweza kujifunza, kubadilishana ujuzi na hatimaye kupata kazi zenye maudhui ya hali ya juu kutoka hapa hapa Afrika”, alisema Mama Fisoo.
 

Naye Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Grace Mgaya alimalizia kwa kueleza kuwa ukurasa huu wa ni wa wazi kwa watu wote hususani wadau wa filamu waliopo hapa nyumbani na Afrika kwa ujumla. “Tunaamini kwa kupitia program hii tutaweza kuwafikia wadau wengi zaidi na tunatarajia kazi zenye ubora wa hali ya juu kutoka barani Afrika kwa siku zijazo kutokana na matokeo chanya yatakyoletwa na program hii ya MultiChoice Talent Factory”, alisema Grace.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive