A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, November 10, 2017

Airtel yaja na programu mpya ya U900 kuboresha huduma za Intaneti

Meneja Uhusiano wa AIRTEL Tanzania Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari leo katika uzinduzi wa programu mpya ya  Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Mradi Tayari ushazinduliwa na kuwasha mitambo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha. Kulia ni Meneja Ubora wa huduma za Mtandao Emmanuel Luanda
uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Meneja Ubora wa huduma za Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda (kulia) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja na kuongeza ubora wa upatikaniji wa intaneti bila kujali maeneo mteja alipo uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa na Masoko Airtel Tanzania Anorld Mandale (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua programu mpya ya  Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Kampuni hiyo pia huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambapo wateja wataweza kufaidi huduma hii kwa kupiga *150*60#  na kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa siku saba uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa na Masoko Airtel Tanzania Anorld Mandale (katikati) akishika bango pamoja na maofisa wenzake wa kampuni hiyo baada ya kuzindua huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambapo wateja wataweza kufaidi huduma hii kwa kupiga *150*60#  na kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa siku saba. Kushoto ni Meneja Ubora wa huduma za Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando
 Teknolojia ya U900 kuwapatia watumiaji wa Airtel Intaneti yenye kasi  popote
•Airtel yawekeza kwenye teknolojia mpya ya intaneti kutoa mtandao bora hata ukiwa ndani ya jengo.

Airtel Tanzania Plc kampuni ya  mawasiliano iliyojikita katika huduma zenye ubunifu wa teknolojia zaidi nchini, leo katika muendelezo wake wa kutimiza dhamira yake ya kuwa mtandao bora zaidi imetangaza na kuzindua rasmi programu yake ya maboresho ya huduma za mtandao wake kupitia teknolojia ya iliyopewa jina la ‘Mradi wa U900’  ukiwa na lengo la kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini.

Mradi wa U900 ni uwekezaji mkubwa unaolenga kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa huduma ya 3G, ujazo wa data kamili pamoja na kuongeza kasi ya intaneti kwa kutumia teknolojia hii ya mawimbi ya mawasiliano ya masafa ya  900 Mhz. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja kuongeza ubora wa upatikani wa intaneti bila kujali maeneo mteja alipo, Popote utapata Intaneti bora.

Akiongea leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza huduma hiyo, Meneja huduma wa mtandao Airtel Bw, Emanuel Luanda alisema kuwa Airtel imewekeza kwenye kuimarisha huduma ya mtandao kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za smartphone na pia kutokana na uhitaji wa huduma mpya za ziada. Kutokana na uboreshaji wa mtandao wetu, wateja wote nchini watakuwa wakitapa huduma yenye kasi na hivyo kuwa na uhakika na huduma bora kutoka Airtel wakiwa popote.

Bw, Luanda alidokeza “ripoti ya hivi karibuni ya TCRA inayotoa mchanganuo wa matumizi ya huduma za Intaneti (Data)  inaweka wazi kuweko kwa ongezeko la watumiaji wa huduma za intaneti kutokea 34% kwa mwaka 2015 na kupaa hadi 40% kwa mwaka 2016.  Hali hiyo ndio inatoa msukumo hata kwetu Airtel kuendelea kuwekeza zaidi katika teknolojia mpya  ili kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi”.

“Tayari tushafanya maboresho kwenye miji ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza huku maboresho mengine yakiendelea kufanyika Dodoma, Morogoro na miji mingene yenye uhataji mkubwa wa huduma zetu hapa Tanzania.” Alieleza Luanda

Kwa upande wake, Meneja wa Masoko Airtel Tanzania Arnold Madale alisema, “kwa kuwa Airtel tunatambua mahitaji ya wateja wetu, hali ya soko tumekuwa tukifanikiwa kuleta bidhaa zenye ubunifu  na mpangilio wa huduma zinazozingatia mahitaji ya mteja, hii ni hatua kubwa sana hasa kwenye ushindani wa biashara. Tunao  wateja ambao wanatumia mtandao wetu kwa ajili ya intaneti tu, lakini pia kuna wale wanaotumia kwa kupiga na kupokea simu, tunazo bidhaa na huduma ambazo zinakidhi matakwa ya wateja hao kwa muda wote wakiwa mahali popote. Kwa sasa hivi tunaendelea pia kuboresha huduma yetu ya 2G ili kutoa huduma yenye uhakika wa hali ya juu ikiwemo huduma ya Airtel Money ili kuendelea kuwafikia Watanzania wengi waishio pembezoni  huduma za kibenki na huku tukitimiza sera ya serikali ya kushiriki katika uboreshaji wa huduma bora za kifedha vijijini.”

“Tunapotangaza huduma hii muhimu ya kuboresha mtandao wetu, tunayo furaha kutangazia huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambayo inapatika kwa urahisi na kumfanya mteja kuwa na Uhuru zaidi wa kutumia Intaneti  yenye kasi kwa muda mrefu zaidi kwa kuwasiliana na ndugu, marafiki  au wadau katika biashara mahali popote. Wateja wetu wataweza kufaidi huduma hii ya bando kwa kupiga *150*60#  na kujipatia 1GB, dakika150 kupiga mitandao yote na kudumu nazo kwa muda wa siku saba, aliongeza Madale.

‘Nia yetu ni kuendelea kukua kupita Maelezo huku tukitengeneza ujuzi wa kuaminiwa na wateja wetu kwa kuwa na gharama nafuu. Mradi wa U900 unadhihirisha kuwa Airtel imeamua kuinua taifa letu kufikia lengo la kuishi kidigitali kwa kuwepo na huduma za kidigitali, aliongeza Madale.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive