A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, November 9, 2017

NBC YASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI YA SARATANI YA MATITI

01
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kibenki cha Taasisi za Sekta ya Umma, Noelina Kivaria (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk. Julius Mwaiselage wakati wa matembezi ya hisani kuchangia juhudi za kupambana na saratani ya matiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo.
02
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakiwa na nyuso za furaha wakishiriki matembezi ya hisani  kuchangia juhudi za kupambana na taztizo la ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo.

03
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya (kushoto), Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage (wa pili kulia), wakishiriki matembezi ya hisani  kuchangia juhudi za kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa saratani ya matiti. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo.
04
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza kwa matembezi hayo. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo.
05
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakilisikiliza kwa makini hotuba na shuhuda mbalimbali zilizokuwa zikitolewa muda mfupi baada ya kumalizika kwa matembezi hayo ya hisani kuchangia juhudi mbalimbali zinazoendelea za kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa sarani ya matiti. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo.

06
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha ya kumbukumbu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kabla ya kuanza kwa matembezi hayo ya hisani kuchangia harakati za kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa saratani. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo.
07
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipiga picha pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu baada ya kumalizika  kwa matembezi hayo. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo.
08
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kibenki cha Taasisi za Sekta ya Umma, Noelina Kivaria (kushoto), akimsikiliza  Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati),  wakati wa matembezi ya hisani kuchangia juhudi za kupambana na saratani ya matiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road(ORCI), Dk. Julus Mwaiselage.
09
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kibenki cha Taasisi za Umma, Noelina Kivaria (kushoto) akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa kutambua mchango wa NBC katika kufanikisha matembezi ya hisani ya kuchangia juhudi za kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa saratani ya matiti. NBC ilikuwa moja kati ya wachangiaji wakubwa waliofanikisha matembezi hayo.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive