Maendeleo Benki imeongeza muda wa
mwezi mmoja wa kufanya manunuzi ya hisa kwenye Benki hiyo ili kuwafikia
watanzania wengi zaidi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Ibrahim Mwangalaba ambapo
amesema zoezi la uuzaji wa hisa litakamilika tar 4 Desemba 2017.
Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa
watanzania kuchangamkia fursa ya ununuzi wa hisa ambapo hisa Moja inauzwa
shilingi 600 na kiwango cha chini cha kununua hisa ni hisa 100 thamani yake ni
shilingi 60000 na zinapatikana kwenye Matawi yote ya Benki ya Maendeleo. Crdb
bank, Uchumi Commercial Bank Moshi na mawakala wa hisa waliohidhinishwa na
mamlaka wa mitaji na viwango Tanzania
0 comments:
Post a Comment