
Balozi wa Airtel Money, Lukas Mhavile, akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Airtel Money Ni Buree na Ni Nafuu, kulia ni Mkuruenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, na kussoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Airtel, Jackson Mmbando. “Kampeni Airtel Money ni Bure na Ni Nafuu inaleta unafuu zaidi na kuwapa uhuru wa kufanya mambo mengi zaidi. Airtel Money Ni Bure, mteja ataweza kufanya miamala yake ya kutuma pesa Airtel Kwenda Airtel BURE kupitia my Airtel APP kiwango cha hadi milioni 5, Airtel Money Ni Nafuuu, mteja ataweza kutoa pesa chini ya kiwango cha shilingi 10,000 BURE Bila TOZO ya serikali. Hii inamaana ya kwamba Airtel tutalipa TOZO hiyo ili mteja wetu aweze kufanya muamala wake BURE kabisa.
Airtel Money Tanzania leo imetangaza uzinduzi wa kampeni mbili kabambe maalum kwa wateja wake wa Airtel Money itakayojulikana kama Airtel Money Ni Buree na Ni Nafuu, ikiwa na lengo la kuendelea kutoa uhuru zaidi kwa wateja wote wanaotumia Airtel Money.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Makao Makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, alisisitiza manufaa ya kampeni ya Airtel Money ni Bure na Ni Nafuu:
“Kampeni Airtel Money ni Bure na Ni Nafuu inaleta unafuu zaidi katika kutuma na kutoa pesa, ikiwasaidia wateja wetu kuokoa zaidi na kuwapa uhuru wa kufanya mambo mengi zaidi kwa fedha zao."
Airtel Money Ni Bure, mteja ataweza kufanya miamala yake ya kutuma pesa Airtel Kwenda Airtel BURE kupitia my Airtel APP kiwango cha hadi milioni 5,
Airtel Money Ni Nafuuu, mteja wetu ataweza kutoa pesa chini ya kiwango cha shilingi 10,000 BURE Bila TOZO ya serikali. Hii inamaana ya kwamba Airtel tutalipa TOZO hiyo ili mteja wetu aweze kufanya muamala wake BURE kabisa.
Uzinduzi huu unathibitisha dhamira ya Airtel kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza ujumuishi wa kifedha kupitia mifumo ya kidijitali na kuharakisha safari ya kuelekea kwenye uchumi usiotegemea pesa taslimu.
Airtel Money tunaamini huduma za kifedha zinapaswa kuwa nafuu, jumuishi na kupatikana kwa kila mmoja. Airtel Money kwa kuamua kubeba gharama za huduma za kutoa pesa chini ya shilingi elfu kumi, au kuwezesha Wateja wetu kutuma pesa Kiwango chochote BURE kupitia App yetu, tunajibu moja kwa moja mahitaji ya huduma bora na nafuu ambapo-hii itasaidia wateja wetu kuokoa pesa na kuzitumia kufanya mambo mengine iwe ni kununua umeme, muda wa maongezi au huduma nyingine. Hivi ndivyo tunavyosukuma mbele ujumuishi wa kifedha na kufanya miamala ya kidijitali kuwa nafuu kwa kila Mtanzania.”
Rugamba aliongeza kuwa kampeni za Airtel Money Ni Buree na Ni Nafuu zimetengenezwa ili kuimarisha mfumo wa kifedha wa kidijitali nchini na kuongeza manufaa kwa wateja katika kila muamala wanaofanya.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Airtel jackson Mmbando alisema: “Wateja wetu wametuambia wanataka huduma nafuu zaidi na rahisi zaidi. Airtel Money Ni Nafuu inaleta yote mawili. Airtel Money Ni Bureee na Nafuuu inathibitisha dhamira ya Airtel katika kutoa huduma za kifedha zilizo nafuu, bunifu na jumuishi ambazo zinaendana na dira ya kitaifa ya Tanzania ya kuwa na uchumi imara wa kidijitali.”

Mkuruenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, katikati akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Ni Buree na ni Nafuu wakati wa kutoa pesa kutoka Airtel kwenda airtel kulia ni Balozi wa Airtel Maoney, Lukas Mhavile, na kusoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Airtel, Jackson M,bando. “Kampeni Airtel Money ni Bure na Ni Nafuu inaleta unafuu zaidi na kuwapa uhuru wa kufanya mambo mengi zaidi. Airtel Money Ni Bure, mteja ataweza kufanya miamala yake ya kutuma pesa Airtel Kwenda Airtel BURE kupitia my Airtel APP kiwango chochote yaani hadi milioni 5, Airtel Money Ni Nafuuu, mteja ataweza kutoa pesa chini ya kiwango cha shilingi 10,000 BURE Bila TOZO ya serikali. Hii inamaana ya kwamba Airtel tutalipa TOZO hiyo ili mteja wetu aweze kufanya muamala wake BURE kabisa.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Airtel, Jackson Mmbando, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Ni Buree na ni Nafuu ambapo sasa wateja wa Airtel Money wataweza kutoa pesa chini ya kiasi cha 10000 bila makato ya TOZO na pia Airtel Ni BURE wataweza kutuma pesa kiwango chohote BURE kupitia Airtel App (wakwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, katikati Balozi wa Airtel Money, Lukas Mhavile.
0 comments:
Post a Comment