A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, August 28, 2025

Absa Bank Tanzania yasisitiza dhamira yake kuendeleza ukuaji wa uchumi halisi nchini Tanzania

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Suleiman Hassan Serera (kushoto), akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, kwa kutambua mchango wa benki hiyo kama mdhamini mkuu wa Kongamano la Biashara la tatu la Maofisa Watendaji Wakuu (200 CEO Business Forum), lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Benki ya Absa Tanzania imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuendeleza ukuaji wa uchumi halisi wa nchini Tanzania, ikidhamini jukwaa mahsusi linalowakutanisha watendaji wakuu wa makampuni nchini, likijulikana kwa jina la ‘The 200 CEOs Business Forum’.

Jukwaa hilo la ngazi ya juu lilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt Suleiman Hassan Serera, sambamba na viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na wengineo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mgeni rasmi Dkt. Serera alisitiza umuhimu wa hatua za pamoja ili kupanua ajira na mauzo ya nje huku Benki Kuu ya Tanzania ikitoa mrejesho wa mwelekeo wa uchumi unaosaidia kupanga maamuzi ya bodi, na uwasilisho wa udhamini wa Absa ukugusia suluhisho za kifedha ambazo benki ya Absa inatoa kuwawezesha kampuni kuendesha na kusimamia biashara kwa urahisi ambapo katika mijadala mitatu iliyofanyika ikijikita katika uongozi na utawala bora, afya na uimara wa rasilimali watu, pamoja na njia za ufadhili zinazofungua ukuaji na kuhitimishwa na dira ya PPP.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania alisema Jukwaa hili si mkutano wa mawazo pekee bali ni chombo cha maamuzi yanayosukuma mitaji, kuunda ajira, kurasimisha minyororo ya thamani na kufungua fursa za mauzo ya nje akisema kama Absa, wanajivunia kusimama pamoja na viongozi wa biashara wa Tanzania katika wakati huu nyeti hususani kupitia dhamira yao ya “Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja… hatua moja baada ya nyingine”.

Stori yako ina thamani” si ahadi tu, ndivyo tunavyojitokeza, tumesikiliza kwa makini vipaumbele na mahitaji ya wakurugenzi wakuu, na kwa kujibu tunawasilisha suluhisho zinazochochea kasi ya biashara, zikiwemo Absa Infinite Card, Absa Business Credit Card, Vehicle Asset Finance (VAF), uwezo mpana wa Cash Management & Payments, Trade & Working Capital, Treasury & Risk Management, pamoja na majukwaa yetu ya kidijitali ya benki kwa makampuni yanayosaidia idara za fedha kufanya kazi kwa kasi na udhibiti.

Tunawezesha malengo ya Watendaji wakuu (CEOs) na wajasiriamali kupitia suluhisho bora za kifedha, zenye bei shindani na zinazotolewa kwa wakati na umahiri.” Bw. Laiser aliongeza.

Udhamini huu mkubwa wa Absa unaonesha ushirikiano wa muda mrefu wa benki na Serikali na sekta binafsi wa kuharakisha ukuaji jumuishi. Kuwakutanisha watunga sera na viongozi wa viwanda katika ukumbi mmoja kunawawezesha kuoanisha kanuni, kuandaa miradi inayoweza kufadhiliwa na kuweka mifumo inayochochea uwekezaji kwa kiwango kikubwa - kigeuza dhamira kuwa utekelezaji.

Aidha watendaji hao walipata nafasi za kuzungumza na wafanyakazi wa Absa wakioneshwa suluhisho mbalimbali za kifedha zinazorahisisha maisha yao. Miongono mwa hizo ni huduma ya kifahari inayorahisisha safari za kimataifa kupitia Absa Infinite Card, udhibiti wa matumizi ya kampuni kwa Absa Business Credit Card, udhamini wa manunuzi ya magari binafsi na ya kibiashara kupitia Vehicle & Commercial Asset Finance. Ulinzi wa hatari na mipango ya ukwasi kupitia Bancassurance na Flexi Fixed Deposit, huduma za Prestige na Premier kwa wateja wa hadhi ya juu, Diaspora Banking ikirahisisha miamala ya kuvuka mipaka, na kwa upande wa sekta ya umma, e-Loans, yote yakithibitisha ahadi ya Absa kwamba Stori yako ina thamani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akichangia mada isemayo “Fedha kama chachu ya ukuaji wa biashara Tanzania; Mikakati na Fursa”, wakati wa Kongamano la Biashara la tatu la Maofisa Watendaji Wakuu (200 CEO Business Forum), lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive