A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, March 11, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAMFURAHISHA RC MONGELLA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati), akikata utepe  kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha kushoto ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, pamoja na  Meneja wa Tawi la Tanzania Commercial Bank  Usa river, Speratus Kamala.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la benki hiyo jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi,wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha kulia ni Meneja wa Tawi hilo Speratus Kamala. 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi,wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha

 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi wakifungua pazia kwenye jiwe la msingi  kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha.

 
 
 
Tanzania Commercial Bank (TCB) yazidi kuchanja mbuga kutanua huduma zake imeendelea kuongeza jitihada kuwafikia Watanzania nchi nzima
Tanzania Commercial Bank imeendelea na juhudi zake za kuendelea kutanua huduma zake kwa kufungua matawi katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha kila mtanzania anaitumia Tanzania Commercial Bank.


Benki hiyo imetimiza haja yake hiyo kupitia huduma zake mbalimbali katika kuigusa jamii kwa kufungua tawi jipya katika mkoa wa Arusha wilaya ya Arumeru USA river katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali.


Tawi la USA River lilianzishwa mwaka 2007 kwenye ofisi za posta, Usariver ikiwa ni benki ya kwanza kufika na kutoa huduma za kifedha katika wilaya ya Arumeru Katika mkoa wa Arusha, Benki ya Biashara Tanzania ina matawi sita (6) Arusha Meru,Usariver, Rombo, Mto mbu,Sokoine na Tanzanite.
 

Tawi la Usariver lina jumla ya mawakala 60 ambao wamesambaa katika wilaya ya Arumeru pamoja na kusogeza huduma za kibenki kwa wananchi, Tanzania Commercial Bank pia inategemewa kufungua na kuendeleza fursa mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kuinua uchumi katika mkoa huo


Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, alisema wateja wa benki hiyo wapo katika mikono salama na kuwaomba wananchi waitumie benki hiyo kwani imekuwa ikifanya mambo mengi yanayolenga jamii.


“Benki imepata mafanikio makubwa, kwa sasa Tawi la Usariver lina jumla ya wateja 5,916 wanaofurahia huduma mbalimbali za kibenki hususani mikopo yenye riba nafuu kama ya kilimo, biashara, watumishi na wastaafu pamoja na kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ndani na nje ya nchi.

Lakini vilevile, Tanzania Commercial Bank ni wabunifu kwenye upande wa kidigitali tumeanzisha huduma ya kuweka akiba kwenye vikundi ambayo tumeshirikiana naVodacom na tumeshakusanya zaidi ya Tshs bilioni 27 lakini pia sisi ni wamiliki wa huduma ya Songesha ni huduma inayomuwezesha mteja kukamilisha miamala pale anapokua hanasalio. 


Lakini kikubwa zaidi, Benki yetu imefanikiwa kutoa kadi za Visa, hivyo basi wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla karibuni sana mjipatie Visa ATM card kwa kufanikisha miamala yeyote popote mlipo Kwa kipindi cha mwaka 2020 mpaka February 2021 tawi limeweza kutoa mikopo ya kiasi cha Tshs 5.78 Billioni  kwa wadau mbalimbali.


 Kuna jumla ya mawakala 60 wanaotoa huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha. Kukua kwa biashara kumefanikisha benki kuhama kutoka katika ofisi ndogo za TPC na kuhamia katika jengo Jipya tunalolizinduliwa leo lenye nafasi kubwa na kuwezesha kutoa huduma kwa ubora na umahiri zaidi.


 Kwa sasa tawi lina wafanyakazi 12 waliobobea katika mambo ya fedha na benki wakitoa huduma bora na kwa weledi wa hali juu.


“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo ya huduma za jamii; Tumefanikiwa kutoa misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa bweni la Shule ya sekondari ya wasichana Nduruma.”
Ni matarajio yetu kuwa biashara itaendelea kukua na kutuwezesha kufungua matawi katika kila wilaya ili kuwezesha bidhaa na huduma zetu kuwafikia watanzania wote kwa ukaribu zaidi .”


Benki imechangamkia fursa ya kukua katika wilaya ya USA river, huku pia ikipanua uwepo wetu nchini.
Tawi linapatikana kwa urahisi, huduma zote za kibenki zipo, pamoja na timu ya wataalam wenye ujuzi. Tunatazamia kukutana na wakazi wa USA river, wafanya biashara na fursa zinazoifanya Benki ya Biashara ya Tanzania kuwa mahali pazuri pa kufanya kazi.


Tanzania Commercial Bank pia inatoa huduma za Kibenki Mtandaoni kama vile Internet Banking, Mobile App & Mobile Banking. Lakini Benki pia iko karibu na wateja wake kupitia vituo vyetu vya Huduma kwa Wateja.


Mkuu wa Mkoa Arusha, alitoa shukrani kwa Benki kuweza kuwafikia wananchi wa Usariver na alitoa wito kwa wananchi ili kuweza kuchangamkia fursa hususani makundi ya kina mama kwasababu Tanzania Commercial Bank, ina akaunti maalum kwa ajili ya wanawake.


Aliongeza kwa kuishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kuendelea kuwekeza katika mkoa huo na kuwataka waendelee kuwekeza katika wilaya zote za mkoa huo.


Mongella amewasisitiza wananchi wa Arusha wajitokezea kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Tanzania Commercial Bank kwani imekuwa benki ya kwanza kuwajali na kuwasogezea huduma wananchi wa mkoa huo.


Kuhusu Tanzania Commercial Bank

Tanzania Commercial Bank Plc ni taasisi ya fedha iliyoundwa kisheria kutoka iliyokuwa
Benki ya Posta Tanzania (Tanzania Post Bank). Mtandao wa Tawi la Tanzania Commercial
Bank una jumla ya matawi 82 Tanzania nzima ikijumuisha bara na visiwani yenye makao
yake makuu jijini Dar es Salaam. TCB inatoa bidhaa na huduma ili kukidhi mahitaji ya
benki ya kibinafsi na ya biashara ya wateja. Tembelea tovuti yetu kujifunza zaidi
www.tcbbank.co.tz
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive