A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Tuesday, March 8, 2022

TUME YA PAMOJA YA FEDHA (JFC) YASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA MWANAMKE DUNIANI.

 

 

.com/img/a/
 Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika maandamano walipoungana na wanawake wengine  duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake duniani katika viwanja vya Uhuru jiji Dar es Salaam ambapo maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Visiwani Zanzibar ikiwa mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani

 
.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/
Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika picha za matukio mbalimbali

 

 Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  ambayo hufanyika kila Machi 8 ambapo wanawake hao wameonyesha kujiamini katika kutenda kazi kwa maendeleo ya Taifa kama kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani Kizazi cha Haki na Usawa katika Maendeleo Endelevu,wafanyakazi hao walikuwa na shamlashala za za namna yake katika katika viwanja vya uhuru jijini Dar es Salaam.


KATIKA Maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani  Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) imetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu hassan kwa jitihada za kuwawezesha Wanawake katika sekta mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo na mwakilishi wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC)   alieleza kuwa katika  Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) imezingatia  kuwapa kipaumbele wanawake  na kutoa majukumu sawa na wanaume ili kutekeleza kauli mbiu ya Siku ya wanawake duniani.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive