A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, March 16, 2022

KONNECT TANZANIA YAFANYA UZINDUZI RASMI WA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI NCHINI

 Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi rasmi wa mtandao wenye kasi zaidi nchini Konnect utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.Meneja Mkuu wa Konnect Tanzania Bw. Philippe Baudrier akizungumza na wadau mbalimbali pamoja na maofisa kutoka Konnect wakati wa ghafla maalumu ya uzinduzi rasmi wa mtandao mpya wa satelaiti nchini utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.


Mshereheshaji wa shughuli ya uzinduzi rasmi wa mtandao wa Konnect Bernice Fernandez akizungumza na wadau mbalkimbali pamoja na maofisa wa Mtandao wenye kasi zaidi Konnect wakati wa shughuli ya uzinduzi wa Mtandao huo utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.


Baadhi ya wageni waalikwa na wana habari wakiwa katika majukumu yao kusikiliza na kufatilia uzinduzi rasmi wa mtandao wenye kasi zaidi konnect utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.





Konnect Tanzania yajenga daraja la usawa wa kidigitali Tanzania

Dar Es Salaam, Tanzania, Machi 16, 2022 – Konnect Tanzania, iliyosajiliwa kama: “Konnect
Broadband Tanzania Limited” ni kampuni tanzu ya Eutelsat iliyojitolea kutoa huduma za kasi
zaidi za satelaiti. Kampuni imetangaza kuzindua ofa mpya ya mtandao wa satelaiti nchini
Tanzania yenye kasi ya hadi 100Mbps. Pamoja na leseni zote na kibali cha kiserikali, Konnect
Tanzania ina vibali vyote vinavyohitajika ili kuweza kutoa huduma za kimtandao wa bei nafuu
nchini.


Kulingana na Utafiti wa Uchumi wa Simu wa GSMA wa 2021, chini ya 28% ya watu katika Afrika
Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaweza kupata mtandao wa simu. Hii inashiria kuwa kuna
sehemu nyingine ulimwenguni ufikiaji wake ni wachini kama vile Europe na zaidi ya 80% ya
watu wameunganishwa. Uchumi wa intaneti barani Afrika una uwezo wa kufikia dola bilioni 180
ifikapo 2025, ambayo ingewakilisha 5.2% ya Pato la Taifa la bara kupitia kupanua matumizi ya
kidijitali, ukuaji wa miji na kupenya kwa simu mahiri.


Utoaji wa huduma za uhakika na haraka kote Tanzania ni muhimu kwa kuzingatia upenyezaji
mdogo wa intaneti nchini, iliyo chini ya 20%. Huku muunganisho ukiwa juu zaidi, huduma za
mtandao wa Konnect Tanzania, zilizoundwa na kupangwa kwa mahitaji ya ndani, sasa
zinapatikana kwa watumiaji wa aina zote nchini kote, kuanzia majumbani na biashara hadi
mamlaka za umma.


Meneja Mkuu wa Konnect Bw. Philippe Baudrier alieleza kuwa: “Huduma za mtandao wa
Konnect zimeundwa kukidhi mahitaji ya makazi na SMBs (wafanyabiashara wadogo na wa kati)
lakini pia zinaweza kusaidia katika maendeleo ya sekta mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo,
utalii, madini, elimu na afya.

Mtandao wa satelaiti ya kasi ya juu na uboreshaji wa sekta ya kilimo Tanzania
Mtandao wa kasi wa juu ni ufunguo wa kuboresha shughuli za kilimo ambazo zinawakilisha
26,74% ya pato la taifa la Tanzania. Kuongeza tija katika sekta ya kilimo sio tu kukuza Pato la
Taifa,bali kutaongeza maendeleo ya taifa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kitaifa wa Kikundi cha Wakulima nchini Tanzania Bw
Stephen A. Ruvuga alisema kuwa: “Mashamba mengi ya kilimo nchini Tanzania yapo katika
maeneo yaliyotengwa na hakuna mtandao wa intaneti. Kuunganisha mashamba haya kwa
mtandao wa satelaiti kutawawezesha wakulima kukusanya data muhimu kama vile unyevu wa
udongo na viwango vya mabwawa, pamoja na ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuboresha ufanisi
kwa kasi.


Kusaidia Sekta ya Utalii ya Tanzania katika ufufuaji wake baada ya Janga
Uwepo wa mtandao wa Kasi katika nyumba za kulala wageni utaongeza usalama na mvuto
katika sehemu za kitalii Tanzania, ambao umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na janga la
kimataifa na mchango katika Pato la Taifa kushuka kutoka 10.7% mwaka 2019 hadi 5.3% mwaka
2020. .


Bw. Kennedy Edward, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Hoteli za HAT Tanzania aliangazia:
“Wajasiriamali wa utalii wa Tanzania wanahitaji mtandao wa uhakika ili kutoa huduma bora,
kukuza ujuzi, na kufungua masoko mapya. Kwa vile tovuti nyingi nzuri zaidi za Tanzania ziko
katika maeneo ya mbali, Broadband ya satelaiti ya Konnect inaweza kusaidia sekta ya utalii kwa
kutoa muunganisho wa intaneti kwa wageni na wafanyakazi katika nyumba za kulala wageni,
zisizoweza kufikiwa na mitandao ya kitamaduni.”


Kuongeza usalama na tija katika sekta nzima ya madini
Janga la Covid-19 limeharakisha kwa kiasi kikubwa sekta ya madini kufahamu faida za mtandao
wa kasi wa juu. Idadi kubwa ya tovuti za uchimbaji madini za Tanzania ziko katika maeneo
yaliyotengwa bila muunganisho wa Wi-Fi au 4G.


Bw. Peter Kabepela, Naibu Mkurugenzi wa chama ya wachimbaji madini Tanzania: “Kuunganisha
migodi ya mbali ya Tanzania kwenye mtandao wa satelaiti kutaongeza tija na kuchangia katika
kulinda eneo lao. Pia itaboresha hali ya maisha ya mafundi wanaofanya kazi kwenye maeneo ya
uchimbaji madini yaliyo mbali na makazi yao.” Shukrani kwa muunganisho wake wa kasi wa
satelaiti, mtandao wa satelaiti wa Konnect ni nyenzo dhabiti katika kusaidia ukuaji wa mchango
wa Pato la Taifa wa sekta ya madini kutoka 3,5% hadi 10% ifikapo 2025.


Kujibu hitaji muhimu la mtandao wa bei nafuu wa kutegemewa wa kasi ya juu kote Tanzania
kutatoa manufaa mengi ya kijamii na kiuchumi. Kuongeza usawa wa kidijitali nchini Tanzania
kwa hakika kutakuwa na manufaa kwa maendeleo ya kiuchumi na kibinadamu na riziki; kusaidia
kuifanya nchi kuvutia na kustahimili.

Hatua rahisi za kusakinisha mtandao mpana wa satelaiti wa kasi zaidi wa Konnect
Kufikia mtandao mpana wa satilaiti ya kasi ya juu sana wa Konnect kunahitaji hatua kadhaa
rahisi. Wateja wanaweza kutembelea tovuti ya Konnect (www.konnect.com), kuzungumza moja
kwa moja na huduma kwa wateja kwa kupiga nambari +255 768 132 829 kuanzia saa 3.00
asubuhi mpaka saa 12.00 jioni au kwenda kwenye duka la washirika lenye leseni ili kukutana
moja kwa moja na mshiriki wa timu ya Konnect. Wafanyakazi waliojitolea watasaidia wateja
kuchagua kifurushi sahihi na kupanga usakinishaji wa haraka. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya
kujisajili kama mshirika tafadhali tembelea Konnect.com

About Konnect
Konnect is the Eutelsat Group entity in charge of retail marketing for a new generation of superfast
satellite broadband services. As its implementation accelerates, Konnect is redefining the connectivity
expectations of people who live and/or work outside the geographical boundaries of fibre, enabling
them to access an immediately available service with ultra-fast, unlimited and competitive offers of up
to 100Mbps. To find out more about Konnect's offers, visit www.konnect.com.

Contact

Name: Obafemi AGBANRIN
Tel: +255 767 256 405
Email: oagbanrin@eutelsat.com

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive