Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa tayari kwa ajili ya kujibu maswali ya mashabiki katika tukio la kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Taifa Stars’ lililofanyika jijini Mbeya ambapo mashabiki walikutana uso kwa uso na baadhi ya nyota wa timu ya taifa.
Mchezaji wa Taifa Stars Kibwana Shomari, akijibu moja ya swali kutoka kwa mashabiki wa soka wakati wa tukio lililowakutanisha wacheza wa timu hiyo ya taifa na washabiki wao lililofanyika jijini Mbeya chini ya kampeni ya Nje ya Dimba na Stars inayoendeshwa na bia ya Serengeti Lager.
Baadhi ya mashabiki wa Taifa Stars mkoani Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo ya taifa, muda mfupi baada ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na bia ya Serengeti Lager ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Taifa Stars’.
Bia ya Serengeti Lager leo imewakutanisha uso kwa uso baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars na mashabiki katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Mbeya ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’
Kampeni ya 'Nje ya Dimba na Stars' inalenga kuwapa nafasi mashabiki wa Taifa Stars kukutana na nyota wanaowapenda katika baa zao na pia watapata fursa ya kuwauliza maswali kuhusu maisha yao nje ya soka pamoja kupiga nao picha za ukumbusho. Kampeni hiyo ya nchi nzima itadumu kwa miezi mitatu.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, meneja masoko wa kanda za juu kusinini wa SBL Denis Tairo alisema bai ya Serengeti lager ikiwa kama shabiki mkuu wa Taifa Stars inajivunia kuwaletea mashabiki wa Taifa Stars mkoani Mbeya nyota inaowapenda na kuwapa nafasi kuzungumza nao na hivyo kuwafahamu kwa undani zaidi.
“Shabiki mkuu na mdhamini wa timu yetu ya taifa, Taifa Stars Bia ya Serengeti Lager leo amewakutanisha mashabiki wa hapa Mbeya uso-kwa-uso na nyota ambao mara nyingi wamekuwa wakiwaona uwanjani. Hii ni fursa pekee ya mashabiki kujua maisha ya nota wao nje ya uwanjani,” alisema
Denis alisema kampeni hiyo ya nchi nzima itahusisha wachezaji wa Taifa Stars ambapo watatembelea mikoa ya Mbeya, Mwanza na Arusha na kukutana na mashabiki wao kupitia matukio kama pati za mwisho wa mwezi ‘Nje ya Dimba na Stars’. Kwenye matukio kama hayo mashabiki wataweza pia kujishindia zawadi mbali mbali na ofa za bei yao pendwa ya Serengeti lager.
"Wachezaji watakuwa kwenye baa mbali mbali na wakati wateja wetu wa bia ya Serengeti Lager wakiendelea kuburudika na bia yao pendwa iliyotengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 na isyoongezwa sukari, watapata nafasi ya kuwauliza maswali, kupiga picha na kupata sahihi zao,” alisema
Aliwataka mashabiki wa Stars kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya bia ya Serengeti Lager Pamoja na kusikiliza redio kwa ajili ya kujua linin a wapi nyota wa taifa Stars watakuwa.
0 comments:
Post a Comment