Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya Biashara ya Tanzania Commercial Bank TCB Sosthenes Nyenyembe akizungumza wakati wa hafla yakukabidhi madawati 50 yaliyozolewa na Benki hiyo katika Shule ya Msingi Komboa iliyopo wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Vijijini Samwel Komba (wannekushoto), akipokea msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya Biashara ya Tanzania TCB kwa Shule ya Msingi Komboa iliyopo wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma kutoka kwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Tanzania Commercial Bank Sosthenes Nyenyembe hafla ya makabidhiano hayo imefanyika hivi karibuni shuleni hapo.
Kama ilivyo kawaida ya Benki ya Tanzania Commecial Bank kusaidia jamii, leo Tanzania Commercial Bank imepata fursa ya kukabidhi Madawati 50 Katika Shule ya Msingi Komboa Iliyopo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, hii yote nikutambua mchango wa Serikali hasa sekta ya Elimu.
Tumeamua Kama Benki ya Biashara ya Tanzania kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuinua na kukuza kiwango cha elimu nchini.
Msaada huo wa Madawati yamekabidhiwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani waTanzaniaCommercial Bank
akiambatana na Afisa Elimu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbinga, Uongozi wa Kijiji, Uongozi wa shule pamoja na Diwani wa kata hiyo
Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani wa Benki hiyo Sosthenes Nyenyembe alisema msaada huo wa madawati 50 uliotolewa na TCB unathsamani zaidi ya milioni nne na laki tano
0 comments:
Post a Comment