A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, October 20, 2017

NBC yapongezwa kwa kusapoti VICOBA

01
Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Philip Mpango akifurahi pamoja na baadhi ya washiriki zaidi ya 1000 wakati maadhimisho ya Siku ya VICOBA jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Benki ya NBC ilikuwa mmoja ya wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo.
02.
Katibu Mtendaji  wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akizungumza katika maadhimisho hayo.
03
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Fibert Mponzi kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya VICOBA nchini. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga.
04
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi akishikana mikono na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), John Jingu (kushoto) mara baada ya kupokea cheti kutoka kwa mheshimiwa waziri wa fedha.
05
Mkururugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (wa pili kulia), akishikana mikono mmoja wa washiriki wa maadhimisho ya Siku ya VICOBA. Wanaongalia wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Meneja Masoko, Alina Maria Kimaryo. NBC ilikuwa mmoja ya wadhamini wakuu wa maadihimisho hayo.
06
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea bango lililoandikwa ujumbe wa kuishukuru serikali kwa kuiunga mkono VICOBA kutoka kwa mmoja wa wanachama wa VICOBA, Devota Likolola (wa pili kulia). Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa.
07
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi akishikana mikono na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa (kushoto), wakati wa maadhimisho hayo. Maadhimisho ya Siku ya VICOBA yalihudhuriwa na washiriki zaidi ya 1000 na Benki ya NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini wakuu.
08
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi  huku Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa (katikati), akifurahia wakati wa maadhimisho hayo. Benki ya NBC ilikuwa ni mmoja ya wadhamini wakuu wa maadhimisho ya Siku ya VICOBA.
09
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe (kulia), huku Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi (katikati) akisikiliza wakati wa maadhimisho hayo.
10
Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru (katikati), akitoa maelezo kuhusu mchango wa benki hiyo katika katika kuwainua na kuwajengea uwezo wajasiriamali wakati wa maadhimisho hayo. Hafla hiyo ilihudhuriwa na washiriki zaidi ya 1000 na kudhaminiwa na NBC.
11
Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo, akishikana mikono na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa (kulia), wakati wa maadhimisho hayo. Wengine kutoka kushoto waliosimama  ni, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.  
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive