A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Sunday, October 15, 2017

DANUBE YAZINDUA DUKA LAO JIPYA MLIMANI CITY

https://4.bp.blogspot.com/-R8op0z0n3y0/WeMl4Wto7bI/AAAAAAAJ3Ps/ATAMUPjc9nsonk5RQS2b3GJ62awnNZyZwCLcBGAs/s1600/WhatsApp%2BImage%2B2017-10-15%2Bat%2B10.16.04%2BAM.jpeg

Waziri wa viwanda na uwekezaji Charles Mwijage akiwa pamoja na Viongozi kutoka Danube pamoja na Balozi wa Duka hilo la Danube Zarina Hassan kwa pamoja wakikagua baadhi ya bidhaa ambazo hupatkana kwa wingi katika Duka hilo baada ya kuzindua duka hilo jipya lililopo mliman city.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya GSM na washirika wake Danube kwa kutoa fursa za ajira kwa watanzania zaidi ya watu 50.
Waziri Mwijage amesema hayo  katika uzinduzi wa  duka hilo jipya la samani, Danube Mlimani City na kusema kuwa ni fursa nyingine pia kwa watanzania kwani samani ambazo zitatumika kutengenezea samani hizo zitakuwa zikitoka hapahapa nchini pia kuongeza soko la ajira kwa vijana wakitanzania.
 
Naye Balozi wa Danube  Zarina  Hassan amesema kuwa anafuraha kubwa sana kuchaguliwa na kuaminiwa kuwa balozi wa duka hilo pia anawasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kujipatia huduma katika duka hilo kwani hata gharama zake ni za kawaida ambazo hata mwenyekipato cha kawaida anaweza kumudu.
Image result for uzinduzi wa danube
Purukushani zilitawala nje ya duka hilo wakati kila mmoja akijaribu kumsukuma mwenzake ili aweze kumuona Zari ambae pia ni balozo wa duka hilo aliyekuwa amekaa katika makochi  baada ya uzinduzi wa duka hilo.
 
Watu walivutiwa kumuona mwanamke huyo kutokana na hivi karibuni kupamba vichwa vya habari baada ya mpenzi wake kukiri kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Ujio wa Zari nchini amekuwa na mvuto kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakilinganisha matukio katika maisha ya Zari na Hamisa.
 
 baadhi ya samani zinazopatikana katika duka hil
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive