Barcelona wamepoteza mchezo wa kwanza wa fainali
ya Super Cup baada ya kuruhusu magoli matatu dhidi ya mahasimu wao wakubwa Real
Madrid katika uwanja wa Camp Nou.
Real walianza kupata bao la kwanza ambalo beki
Gerard Pique wa Barcelona alijifunga baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na
mlizni Mbrazili, Marcelo na kumhadaa golikipa wake.
Real walipata goli la pili kupitia Cristiano
Ronaldo aliyeingia kuchukua nafasi ya Karim Benzema baada ya kupiga shuti kali
nje kidogo ya eneo la hatari la Barca.
Ronaldo alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati wakati
akishangilia mbele ya washabiki wa Barcelona, na dakika tatu baadae alitolewa
kwa kadi nyekundu baada ya kujiangusha baada ya kushindana na Umtiti katika
kuwania mpira.
Real walifunga goli la tatu kupitia kwa Marco
Asencio aliemalizia vizuri kazi ya Lucas Vazquez nje ya box la hatari umbali wa
mita 25.
Ushindi huu unawapa Real nafasi kubwa ya kunyakua
kombe hili wakirudi Bernabeu na akiba ya magoli mawili waliyopata leo ugenini
Camp Nou.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za mtanange huo.
0 comments:
Post a Comment