A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, March 8, 2021

AKIBA COMMERCIAL BANK YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUCHAGUA CHANGAMOTO KULETA FIKRA MPYA KWA MAENDELEO

 
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (kulia), akikata keki pamoja na wateja wake kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya kuwashukuru wateja wake.
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (kulia), akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya futa vicoba endelevu ambae pia ni mteja wa Benki hiyo Hanipha Tarimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya kuwashukuru wateja wake hafla hiyo imefanyika katika ofisi za benki ya ACB Tawi la Kijitonyama leo Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Dora Siria.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Dora Siria akimlisha keki Afisa wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Amani Mwakitalima wakati wa maadhimisho wa siku ya wanawake duniani ambapo Benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya wateja wake.
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (katikati), akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani taasisi mbalimbali zimetakiwa kuhakikisha wanatoa huduma katika hali ya usawa bila kubagua jinsia.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Akiba commercial (ACB), Dora Siria Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Hayo yamesemwa wakati wa Benki ya ACB kuwashukuru wateja wao waliokuwa nao kwa kipindi cha muda kirefu.

Amesema, kauli mbiu ya mwaka huu ni “Choose to Challenge" yaani Chagua Changamoto zaidi kwa maana kuwa changamoto maranyingi zinaleta fikrampya, mitazamomipya na mabadiliko.

Siria amesema, wanatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii bora ndio maana zaidi ya asilimia 50 ya wateja wanaopata huduma kwenye benki yao ni wanawake.

"Asilimia 50 ya wateja wetu ni wanawake ambao wamewezeshwa kwa kupewa huduma mbalimbali ambazo zimewasaidia kubadilisha hali zao za maisha kwa kuwa na maisha bora," amesema Dora.

Akiba Commercial Bank kama sehemu ya jamii pia inalichukulia swala hili kwa umakini na uzito wake tunaelewa na tunatambua na kuheshimu nafasi ya Mwanamke katika jamii.

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Fata Vicoba Endelevu ambae pia ni mteja wa benki hiyo Hanipha Tarimo amesema amekuwa mteja wa ACB kwa kipindi cha muda wa miaka mitano na ameweza kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya biashara yake ya kuuza nywele origino za kike, maduka ya Nguo yaliyopo karioo mtaa wa msimbazi, na ameendesha maisha yake vizuri tokea aanze kutumia Benki hiyo.

Amesema, anawasihi wanawake wengine wasisite kuchukua kuitumia Benki ya Akiba Commercial bank kwani inasaidia kuinua wanawake kiuchumi na pia ACB wamekuwa ni moja ya taasisi wasikivu hususani pale mteja anapokua amekwama.
Share:

Benki ya NBC Yawafunda Wanawake Kuhusu Ubora wa Bidhaa na Mikopo

 PIC%2B1.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TABWA) Bi Noreen Mawala (kushoto), akikabidhi zawadi kwa niamba ya wanawake wajasiliamali nchini kwenda kwa Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo (Kulia) na Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya hiyo Bw Jonathan Bitababaje (katikati) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kuwasaidia na kuwawezesha wanawake wajasiliamali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika jana wakati wa kufunga Maonesho ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.PIC%2B2.Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo akizungumza WANAWAKE WAFANYA BIASHARA  na washiriki wa maonesho hayo waliohudhulia mafunzo ya ujasiliamali yaliyodhaminiwa na benki ya NBC kwa kushirikiana na TABWA pamoja na wadau wengine ili kuwatia shime wanawake katika ujasiliamaliPIC%2B9.

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo (kushoto), akikabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo kwa mmoja kati ya washiriki  waliohudhuria semina hiyo.


Dar es Salaam: Machi 8, 2021: Wanawake wajasiliamali na wafanyabiashara nchini wameshauriwa kuongeza jitiahada zao zaidi katika kuboresha zaidi mawazo ya biashara sambamba na kuongeza ubora za wa bidhaa zao ili kuongeza ushawishi kwa taasisi za kifedha nchini ziweze kuwakopesha kwa urahisi.


Akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku nne, Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo alisema taasisi za kifedha zinashawishika zaidi kutoa mikopo kwa kuzingatia ubora wa wazo la biashara na sio jina au jinsia ya mkopaji.


Alisema hiyo ndio sababu benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaendelea kuwaongezea ujuzi wajasiliamali hao ili kuboresha mawazo na bidhaa zao ili kuwajengea uwezo utakaowezesha kufanya biashara zao kwa weledi na kutengeneza faida itayowawezesha kurejesha mikopo yao.


“Ndio maana kupitia wataalamu ambao tunawatumia kutoa elimu kwa wajasiliamali kupitia maonesho kama haya, tumekuwa tukifundisha na kusisitiza sana juu ya umuhimu wa kujenga zaidi majina ya bidhaa zao kuliko majina yao binafsi kwa kuwa taasisi za kifedha zinatazama zaidi biashara zao na sio jinsia wala majina yao binafsi,’’ alisema  Consolatha.


Pamoja na kudhamini maonesho hayo, benki hiyo pia iliandaa programu kadhaa za mafunzo kwa wajasiliamali ikiwemo kliniki ya biashara kwa kushirikisha taasisi na mamlaka mbalimbali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).


Zaidi benki hiyo ilitumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mahususi kwa ajili ya wanawake na wajasiliamali zikiwemo akaunti za NBC kua Nasi na akaunti mpya ya Johari.


“NBC Kua nasi ni akaunti maalum kabisa kwa wote wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kama vile mama na baba lishe, wenye maduka ya reja reja, wasindikaji wa vyakula na mazao, bodaboda, wazabuni wa taasisi mbalimbali wakati akaunti ya Johari ni mahususi kwa ajili ya wanawake na inawezesha kuweka akiba kidogo kidogo kwa kianzio cha shilingi 10,000 tu. Akaunti zote hizi hazina makato ya mwezi,’’ alisema.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TABWA) Bi Noreen Mawala ambae taasisi yake ndio iliratibu maonesho hayo pamoja na kuipongeza benki ya NBC pamoja na wadau wengine kwa kufanikisha maonesho hayo, alisema taasisi hiyo kwasasa inaandaa safari ya mafunzo na maonesho ya biashara katika nchi za Oman na Comoro ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao kutangaza biashara zao katika mataifa hayo.


“Baada ya mafanikio kupitia maonesho haya yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani  tunatarajia kuwa na safari za maonesho ya biashara zetu katika nchi za Oman na Comoro ili kufungua milango zaidi ya kutangaza biashara zetu nje nchi,’’ alisema.

Share:

Saturday, March 6, 2021

BENKI YA NBC YADHAMINI MAONESHO YA WAFANYA BIASHARA WANAWAKE TANZANIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wafanya biashara wanawake yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC yenye kauli mbiu MWANAMKE MILIKI KIWANDA KWA UCHUMI ENDELEVU, maonesho yaliyozinduliwa na waziri huyo katika viwanja vya mlimani city jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wafanya biashara wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki hiyo ambapo katika uzinguzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo halfla ya uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya mlimani city jijini Dar es Saalam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo (katikati) akipokea zawadi ya kifungashio kilichotengenezwa na wajasiliamali wakitanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wafanya bishara wanawakeTanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC kutoka kwa Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (Tabwa), Noreen Mawalla (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho
Baadhi ya wanawake waliohudhulia hafla ya uzinduzi huo wakifurahia jambo kutoka kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja waziri pamoja na wadhamini wa maonesho hayo.

Serikali imewataka wanawake kuchangamkia fursa zinazotolewa katika mikoa wanayoishi ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa kwenye swala zima la mitaji.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubumgo wakati alipoalikwa kuwa Mgeni rasmi na kuzindua maonyesho ya biashara za wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya Taifa ya bishara NBC,kwa lengo mahususi la kuwainua wanawake kiuchumi yanayofanyika Mlimani City kwa siku tatu mfurulizo.

Waziri Mkumbo amesema Serikali kwa kutambua umuhimu na mchango wa maendeleo kwa wanawake kwa Taifa, letu na Serikali inayoongozwa na jemedali wetu Rais John Pombe Magufuli wameanzisha dirisha maalumu la mikopo kwa halmashauri zote nchini kwa ajili ya kuwainua wanawake na vijana.

"Tunatambua jitihada zenu na malengo yenu lakini Serikali tunatoa wito kwa wanawake wote nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa kupitia mikoa yao ziweze kuwasaidia kwenye changamoto zinazowakabili,” amesema Waziri Mkumbo.

Waziri huyo pia ameishukuru Benki ya Taifa ya Biashara NBC ambayo ndio mdhamini mkuu wa maonesho hayo kwa uzalendo walioufanya kutambua kuwa hakuna maendeleo bila wanawake na kulibeba hili ili wanawake waweze na vijana waweze kwenda sawa na spidi ya uchumi wa kati na kuzitaka Taasisi nyengine kuiga mfano huo kwani utaleta matokeo nyanya katika sekta ya uwekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (Tabwa), Noreen Mawalla aliiomba Serikali kuwasaidia majengo ya wazi ili wanawake wafanyie biashara zao katika mazingira mazuri na salama yatakayowawezesha kulipa kodi kwa wakati.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho katika uzinduzi huo leo, amemwambia Waziri kuwa lengo kuu la udha mini wa benki hiyo kwa maoneso ya wanawake wafanya biashara tanzania ni kuwawezesha wajasiliamari wadogo na wa kati ambao ndiyo walengwa wakuu wa maonesho haya.

NBC ni Benki inayo wajali wateja wake na watanzania wote kwa ujumla hivyo ili waweze kuwa wafanyabiashara bora nilazima wapate elimu ya kifedha hivyo tunawakaribisha NBC waje wapate elimu pia kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo alisema mwinyidaho.
Share:

AKIBA COMMERCIAL BANK RECEIVES TSHS 17 BILLION IN STRATEGIC INVESTMENTS FROM THE NATIONAL BANK OF MALAWI

01
Akiba Comercial Bank's Acting Managing Director, Juliana Swai (right) speaks to reporters at a press conference in Dar es Salaam yesterday. She is flanked by the Bank's Head of Marketing & Communications, Dora Saria.

Dar es Salaam - Akiba Commercial Bank (ACB) has received Sh17 billion in strategic investments from the National Bank of Malawi (NBM) in a merger that was concluded February 2021.

Through the investment, Akiba Commercial Bank has strengthened its capital base to meet requirements of the Bank of Tanzania required for operations of commercial banks in the country.

Addressing reporters at a press conference yesterday, Akiba Comercial Bank's Acting Managing Director, Juliana Swai said the merger aimed at strengthening the bank’s capital as required by the Bank of Tanzania.

“Akiba Commercial Bank has been looking at the market demands as well as a strategic investor or shareholder in order to strengthen the bank and improve its services as well as starting more other services required in the country’s market,” she said.

She pledged major and positive changes in services delivery as well as systems of services delivery, saying customers will be serviced with the highest integrity and professionalism based on the experience from both institutions.

“We also understand the bilateral relations between the two countries in various areas including trade and creating an enabling environment for trade prosperity through easy access of financial services.

Share:

Thursday, February 4, 2021

MAENDELEO BENKI YAZINDUA KAMPENI YA UPENDO WOTE KWAKO

  
Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Benki hiyo George Wandwalo.
Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula (katikati), akionesha maandishi kuashiria uzinduzi rasmi i wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Benki hiyo George Wandwalo.
Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Maendeleo Benki George Wandwalo (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula.

Na Mwandishi Wetu | Dar es Salaam | Leo tarehe 04/02/2021 katika ukumbi wa Mikutano wa Maendeleo Bank iliyopo Posta jijini Dar es Salaam, Meneja wa huduma kwa Wateja wa Maendeleo Bank Sylvia Chaula, amezindua rasmi kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank.

Sylvia Chaula ameeleza kuwa kilele cha kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO kitakuwa ni siku ya wapendanao (Valentine’s day) yaani tarehe 14/02/2021 ambapo washindi watatu watakaoshinda watapata zawadi mbalimbali kama vile Laptop, Simu Janja, Saa pamoja na kupata chakula cha usiku na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr Ibrahim Mwangalaba pamoja na jopo la wafanyakazi wa Maendeleo Bank katika Hotel ya Holiday Inn iliyopo Posta.

Washindi wote watatu wapata nafasi adhimu ya kuwaalika wapendwa wao katika chakula cha usiku, yaani kila mshindi atakuja na +plus one wake katika siku hiyo ambapo pamoja na chakula cha usiku pia kutakuwa na tukio la washindi kupokea zawadi zao kutoka Maendeleo Bank.” Aliongeza Sylvia Chaula.

Unajua maneno matupu hayanogeshi shughuli, siku hiyo ya wapendanao sisi kama Maendeleo Bank tunapenda kutumia muda wetu kuwaonyesha wateja wetu kuwa tunawapenda, tunawajali na kuwathamii ndio mana tumechagua siku hiyo kuwaonyesha wateja wetu upendo tulio nao kwao kwa vitendo na sio maneno.” Aliongeza Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Bank na Tehama Ndg. George Wandwalo.

Maendeleo Bank imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma na kuja na majawabu mbalimbali yanayoweza kuwakwamua watu kiuchumi na hivyo kutoka kwenye hali moja ya maisha na kwenda kwenye hatua nyingine.

Maendeleo Bank imekuwa ikifanya hivi kwa kuja na huduma mbalimbali kama vile Huduma za Mikopo kwa Wajasiriamali wadogo wadogo, Wafanyakazi, Taasisi, Vikundi, na huduma nyingine nyingi za kibenki.

Kwa mawasiliano zaidi;
Eliupendo Mziray,
Mratibu wa Kampeni ya Upendo Wote Kwako
Maendeleo Bank
0758698022
Share:

Sunday, January 24, 2021

KILA JAMBO JIPYA MAISHANI LINA VITA VIPYA

       
Na Mwandishi Wetu | Arusha | Wakristo kote ulimwenguni wametakiwa kujiandaa na kutambua kuwa kila jambo jipya linalotokea katika maisha ya Mtu linakuwa na vita vipya.

Wito huo umetolewa na Askofu Joseph Lai Laizer wakati akihubiri neno la Mungu lililokuwa na kichwa cha somo kisemacho “Jambo Jipya na Vita vipya” katika Kanisa la Christian Life Church Sinai Mlima wa Washindi lililopo Kiranyi Mkoani Arusha.

Askofu Laizer amesema kuwa kila jambo jipya linalotokea katika maisha ya Wakristo lazima yawe na vita vipya hivyo Wakristo wanapaswa kujiandaa kupambana na vita hivyo kwa silaha ya maombi pamoja na kumtolea Mungu sadaka.

Lazima uombe maombi ya vita huku ukiambatanisha na sadaka, sadaka ni kitu cha muhimu sana

Jambo jengine katika kuvishinda vita hivi, yakupasa kumpata Kuhani atakayesema na kutoa matamshi juu ya hivyo vita vyako

"Wakati Mfalme wa Israel alipoingia vitani na vita kuwa vikali alilikumbuka hili umuhimu wa kuwa na Kuhani katika vita vyako vipya ......Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hapana hapa nabii wa Bwana, ili tumwulize Bwana kwa yeye? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake Eliya..... 2Wafalme 3:11"

Napenda kuwaasa watu wa Mungu, kuwa usifurahi sana kuwa kuna jambo jipya linakwenda kutokea kwasababu Unabii umetoka, au kwasababu Mungu amesema kupitia watumishi wake yakupasa kujiandaa na vita vipya

Hata mwaka kuna mambo Mungu anakwenda kufanya kwako lakini lazima ujiandae kwasababu kila jambo jipya lina vita yake” alisema Askofu.

Laiton Deo Shinze mmoja wa Waumini wa Kanisa hilo waliohudhuria Ibada hiyo alitoa maoni yake kuhusu somo hili na kusema “Kwa kweli neno la Mungu alilotufundisha leo Askofu Lai, limetufundisha kwakila jambo yatupasa tumtegemee Mungu

Nae Bi Flomena Fredrick aliongeza kuhusu neno alilofundisha Askofu Lai “Neno la leo limenibariki sana. Mtumishi wa Mungu alikuwa anatufundisha jinsi ya kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, yakwamba kila unapotoka hatua moja kwenda nyingine unajenga kitu kipya na kila kitu kipya huja na changamoto mpya, hivyo kuelekea hatua nyingine hupaswi kulegea, unahitajika kupambana ili kuyafikia yale mafanikio yaliyokusudiwa

Ibada hiyo iliitimishwa kwa maombi maalumu kwaajili ya Wakristo wote Ulimwenguni. Kanisa la ‘Christian Life Church’ Sinai Mlima wa Washindi ni huduma inayopatikana katika jiji la vArusha maeneo ya Kiranyi, Sakina. Engi wanapokea na kushuhudia ukuu wa Mungu kupitia Mtumishi wake Askofu Joseph Lai Laizer.
Share:

Sunday, January 17, 2021

MWANADAMU UMEUMBWA KUSHINDA

Na Mwandishi Wetu | Arusha | Askofu wa Kanisa la ‘Christian Life Church’ Sinai Mlima wa Washindi lililopo Sakina jijini Arusha, Joseph Laizer amewaasa vijana waliohitimu katika vyuo mbalimbali nchini kuwa mwanadamu ameumbwa kushinda.
Askofu Laizer, Baba wa Washindi ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum aliyoyafanya na mwandishi wetu jijini humo.

Vijana wengi huishia kulalama na kuiona serikali kama sio msaada kwao kisa kukosa namna ya kupata ajira mara tu ya wao kuhitimu elimu yao, huku wakisahau ile nafasi ya kupata elimu bure na ya mkopo vyuoni ni njia tosha ya kuwapelekea kwenye mafanikio wayatakayo

Wanadamu tumeumbwa washindi, sasa ili kufikia lengo la ushindi kuna vitu vya kufanya na sio kulalamika, na kubweteka, unahitajika kufanya mambo kwa zaidi ya vile ilivyozoeleka

Mchezaji bora kwenye mashindano ni Yule anayejituma na kufanya jambo la ziada ambalo litapelekea timu yake kushinda, na sio kulalama kutegemea huruma za mwamuzi wa mchezo” alisema Askofu Laizer.

Vijana wanasahau kuwa thamani ya maisha yao yapo ndani yao wenyewe, hakuna atakayekuthamini usipojithamini wewe mwenyewe

Wewe ni msomi leo, hakikisha hautembei jinsi ile wengine walitembea, maana unachokifanya leo ndio matokeo ya kesho yako, ukipanda malalamiko utavuna hay ohayo malalamiko, hakikisha unafanya kile wengine hawafanyi

Unataka kufanya biashara sawa, hakikisha unafanya zaidi na vile wengine wanafanya hapo ndipo utakapoona ushindi, siku zote tumeumbwa kushinda, hatukuumbwa kushindwa

Biblia mara kadhaa inatufundisha kuwa Mkono wa mwenye bidii Utatawala, ni waase vijana na watanzania kwa ujumla, serikali imetutengenezea jukwaa tayari la mafanikio, ni sisi ndio tunatakiwa kujipanga vizuri ni namba gani tunaiweza kuicheza kiufasaha na kwa ubora huku tukiongeza bidii na ubora kwenye kile tunachokitakakukifanya” aliongeza Askofu Laizer.

Kanisa la ‘Christian Life Church’ Sinai Mlima wa Washindi ni huduma inayopatikana katika jiji la Arusha maeneo ya Sakina, wengi wanapokea na kushuhudia ukuu wa kiungu kupitia Roho wake Mtakatifu.
Share:

Sunday, December 20, 2020

Tanga Cement yashinda ushindi wa jumla tuzo za NBAA kwa Mwaka 2019

 03

Kamishna wa Fedha anaesimamia sekta za maendeleo kutoka Wizara ya Fedha Dk. Charles Mwamaja (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji Bora katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2019 kwa Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mthibiti Fedha wa kampuni ya Tanga Cement Emmanuel Nkonyoka.
02%2B%25282%2529
Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela (kulia) pamoja na timy ya wahasibu kutoka kampuni ya Tanga Cement PLC wakifurahia tuzo ya ushindi wa Jumla ya uwasilishaji Bora wa Taarifa ya Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika tuzo hizo.
01
Kamishna wa Fedha anaesimamia sekta za maendeleo katoka Wizara ya Fedha Dk. Charles Mwamaja (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji Bora katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2019 kwa Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Wahasibu kutoka kampuni ya Tanga Cement.

KAMPUNI ya saruji, Tanga Cement Plc, imeibuka kidedea katika tuzo za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) yam waka 2019/2020 kwa mara ya tano mfululizo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mhasibu Mkuu wa Tanga Cement Plc, Issaac Lupokela, alisema kuwa kampuni hiyo imeibuka na ushindi wa Jumla katika tuzo hizo kwenye kipengele cha watumiaji wa mahesabu kwa kutumia viwango vya kimataifa (IFRS) kwa miaka mitano mfululizo. Mshindi mwingine katika kipengele cha viwango vya kimataifa vya utunzaji fedha katika Sekta ya Umma ni TRA

Aidha, Tanga Cement waliibuka kidedea tena kwa kutangazwa kuwa washindi wa kwanza katika wazalishaji viwandani katika uwasilishaji bora wa taarifa za mahesabu za Boodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Washindi wengine ni kampuni ya bia, TBL PLC na Kiwanda cha Sigara, TCC.

“Huu ushindi nimejisikia furaha sana na kama vile waswahili tunavyosema ngoja ngoja huumiza tumbo ilikuwa kila saa niangalie vitabu vyangu kama mahesabu yamekaa vizuri kwa sababu nilikuwa nina wasiwasi. Ushindi nimeupokea kwa furaha sana kubwa huu ushindi ni wa mara ya tano mfululizokwenye Idara ya Uzalishaji na Ushindi wa Jumla kwa Kampuni zinazotumia Kanuni za Kimataifa za Uaandaaji Mahesabu “International Financial Report Standards (IFRS) imedhihirisha vitu tunavyofanya kwa ubora wa hali ya juu Tanga Cement Plc,” alisema Lupokela.

Akizungumzia siri ya kuibuka na ushindi kwa miaka mitano mfululizo, Lupokela alisema kuwa “Kila siku Tanga Cement Plc inataka iwe bora zaidi ya jana ambapo wameweka viwango vya juu sana. Kampuni yetu inaangalia mbali katika uendeshaji wake.”

Lupokela anasema kila mara huwa anasoma sana kuhakikisha kila mifumo ya uhasibu inapobadilika na kuja mipya hujaribu kuendana nayo kwa mujibu wa kanuni za kimataifa kitu kinachosaidiankatika maboresho.

Mhasibu huyo wa Tanga Cement Plc ameipongeza Bodi ya NBAA kwa kubuni tuzo hizo zinazosaidia kuongeza ubora katika utunzaji wa hesabu kwenye taasisi za Umma na Binafsi.

“Kila mtu anapoandaa mahesabu anajua kwamba kuna shindano liko nyuma kwa hiyo mashindano haya yanatupa motisha sana wa kuyafanya kwa ubora Zaidi. Lakini kitaaluma kubwa wahasibu ndio wanahakikisha coporate zinafanya kazi. Mahesabu yakiandaliwa vizuri yanasaidia hao wanayoyatumia kutumia kwa kufanya maamuzi yaliyo mazuri sana,” alisema.

Kwenye kipengele cha Benki Bora; Benki ya CRDB PLC ilkiibuka kidedea huku ikifuatiwa na NMB PLC na ABSA. Pia kwenye kipengele cha Benki Ndogo; DCB iliibuka mshindi huku ikifuatiwa na KCB Bank Tanzania, na City Bank Tanzania.

Katika kipengele cha Biashara na Usamabazaji; Vodacom Tanzania iliibuka mshindi huku ikifiuatiwa ba Swissport Tanzania na CMC Automobile. Mbali na hilo lakini pia TRA, iliibuka mshindi kwenye kipengele cha Taasisi za Umma na kufuatiwa na TASAC pamoja na TBC. Aidha, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Taasisi nyingine zilizoibuka washindi ni TAAWASA, DAWASA, IRUWASA, EWURA, TCAA, KYERWA District Council, Msksmbsko Town Council, Ilsls Municipsl, Mzumbe University, Sokoine University, Institute of Social Work, Catholic University of Health Science Life, Ministry of Finance & Planing, Account General Deptment, Drug Control & Enforcement Authority.

Taasisi nyingine za umma zilizoibuka kidedea katika kipengele cha watumiaji wa utunzaji fedha kwa viwango vya kimataifa (IFRS) kwa sekta ya Umma ni TANESCO na AICC. Kwenye kipengele cha Sekta ya Bima; mshindi ni Tanzania Re-insurance Compny Limited na kufuatiwa na Sanlam Life Insurance. Kwenye kipengele cha Mamlaka zinazohudumia Maji (Regulatory Authorizes) nalo liliibuka mshindi Ufanyaji

Bw. Maneno: “NBAA ilibuni shindano kuhakikisha watumiaji wanatumia viwango hivyo. Imekuwa kawaida kwa mashirika ya Umma na Taasisi binafsi kuleta mahesabu yao NBAA ambapo tumeweka viwango tunavyotumia katika mtandao. Viwango vina vinavyozingatiwa ni pamoja na lazima mshindi afikie pointi 75. ”

Mwaka huu washiriki walifikia 61 ambapo waligawanywa katika makundi 13; Benki Kubwa, Benki Ndogo, Mashirika ya Uzalishaji (Manufacturers), Mashirika yanayofanya biashara ya Usambazaji (Trading & Distribution), Wakala wa Serikali (Government Agencies), Wanaotumia Hesabu za Umma, Wanaotumia Mahesabu kwa kutumia viwango vya Kimataifa (IFRS), Makampuni ya Bima, Makampuni Usambazaji Maji, Serikali za Mitaa, Vyuo, Tawala za Mikoa (Local Government), Wizara na Idara za Serikali, Taasisi zisizotengeneza faida (NGOs), Makampuni madogo ya Ukaguzi.

“Hesabu lazima ziwe za mwaka 2019 (Januari -Desemba 2019), Taarifa za hesabu lazima ziwe zimefuata katika viwango vya kimataifa, Kampuni lazi iwe imesajiliwa Tanzania, Lazima kampuni ama Taasisi ya Serikali iwe imefuata viwango vya kimataifa vya utayarishaji na ukaguzi iwe imetumian mkaguzi aliyesajiliwa na NBAA, Iwe imepata hati safi ya ukaguzi,” alisema.

Awamu nyingine; Kampuni/Taasisi ya Umma imetimiza sharia za kuundwa kwake kwa kuangalia sharia zilizoundwa na Bunge ama sharia za makampuni (Company’s Act), Wakurugenzi wake wameonesha taarifa za hesabu vizuri, Wamefwata kanuni kwa walioorodheshwa kwenye soko la hisa, Zimefwata kanuni bora kwa mujibu wa kanuni za Soko la Mitaji (CMSA), Namna gani wameonesha viwango vya mahesabu.

Bw, Maneno, ametoa rai kwa kampuni na taasisi za umma ambazo hazikushiriki kushiriki kwani ukishiriki wa mashindano haya ya tuzo hakuna adhabu lakini iwapo utatoa taarifa ambazo hazikufuata viwango tunakuadhibu.
Share:

Saturday, December 19, 2020

AKIBA COMMERCIAL BENKI YAIPIGA JEKI TAASISIS YA FATA VICOBA ENDELEVU YADHAMINI MKUTANO WA MWAKA

 
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (kushoto) akizungumza na wanachama wa Taasisi ya fata vicoba endelevu wakati wa halfa ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi hiyo ambapo mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza nakunufaisha wajasiliamali wadogo na wakubwa. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa 361 uliyopo mwenge jijini Dar es Salaam (wapili lishoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi futa vicoba endelevu Hanipha Tarimo, katibu wa Taasisi hiyo Rehema Sombi pamoja na Mtunza fedha Jefferson Makubo. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Songolo
Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC (ACB), Innocent Ishengoma akizungumza na wanachama wa Taasisi ya fata vicoba endelevu wakati wa halfa ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi hiyo ambapo mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza nakunufaisha wajasiliamali wadogo na wakubwa ili watimize ndotozao kupitia benki ya ACB. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa 361 uliyopo mwenge jijini Dar es Salaam. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Songolo
Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Songolo ambae pia alikuwa Mgeni rasmi katika hafla ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi ya fata vicoba endelevu mkutano uliodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza nakunufaisha wajasiliamali wadogo na wakubwa ili waweze kutimiza ndotozao kupitia Benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa 361 uliyopo mwenge jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Taasisi futa vicoba endelevu Hanipha Tarimo akitoa ufafanuzi kuhusu Taasisi hiyo wakati wa halfa ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi hiyo ambapo mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza nakunufaisha wajasiliamali wadogo na wakubwa ili watimize ndotozao kupitia benki ya ACB. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa 361 uliyopo mwenge jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kinondoni kaya ya Mwananyamala Mulinga Samangwa, Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB),Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo, katibu wa Taasisi ya fata vicoba endelevu Rehema Sombi, pamoja na Mtunza fedha wa Taasisi hiyo Jefferson Makubo. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Songolo
Baadhi ya wanachama wa Taasisi ya fata vicoba endelevu na wateja wa Benki ya ACB wakiwa katika hafla ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka Uliodhaminiwa na Benki hiyo.
Picha ya Pamoja
Share:

KITILA MKUMBO AANZA KAZI ZAKUSAKA WA WEKEZAJI KWA SPEED YA 4G


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo (wa kwanza kutoka kushoto) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha KNAUF Gypsum Tanzania Ltd kilichopo mkoani Pwani, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ilse Boshoff (Aliyevaa nguo za Kitenge.)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo akisalimiwa na baadhi ya Maafisa wa Halmashauri ya Ubungo alipofika kuangalia fursa za Uwekezaji katika Kituo kipya cha Mabasi Mbezi Luis.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akipata maelekezo ya Uzalishaji wa Unga katika Kiwanda cha Bakheresa Group kilichop Buguruni jijini Dar es Salaam.

KATIKA kuhakikisha Sekta ya Uwekezaji nchini inaendelea kukua kwa kasi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo ameendelea na uhamasishaji katika kutangaza vivutio vya Uwekezaji kwa kutembelea Miradi mbalimbali Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Prof. Kitila ametembea Kiwanda cha KNAUF Gypsum Tanzania Limited cha uzalishaji ‘Gypsum’ kilichopo mkoani Pwani ambacho kinazalisha bidhaa mbalimbali za ‘Gypsum Boards’, ‘Metal Profile’ na ‘Plaster Powder’ mahususi kwa ujenzi.

Akizungumza wakati wa ziara yake Kiwandani hapo, Prof. Kitila amepongeza uwekezaji huo kwa Uwekezaji hilo bora katika eneo hilo la mkoa wa Pwani, amesema Serikali inahitaji uwekezaji ambao unazalisha Ajira kwa Vijana na kuheshimu utu wa Watanzania. 

Prof. Kitila amepongeza Kiwanda hicho kukosa changamoto nyingi, pia ameeleza Serikali inahitaji kuwa na Uwekezaji ambao utaleta faida.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ilse Boshoff amesema wamevutiwa kuwekeza Tanzania kutokana na jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda, hivyo wao kuona fursa ya Uwekezaji.

Pia ametembelea Kiwanda cha Bakheresa Group ambacho kinazalisha Unga kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam, Prof. Kitila amesema Serikali ina maono ya kuvutia, kuchochea Uwekezaji ili kusukuma Uchumi. 

“Bakheresa ni Mwekezaji mkubwa hapa nchini, sisi tumekubali kwa hilo tunaona ametoa ajira kwa Watu wapatao 4500 ambao ni wengi. Pia ni Mwekezaji anayetumia Malighafi za hapa ndani Kwa hiyo ni Mwekezaji muhimu kwa Wakulima”, amesema Prof. Kitila.

Amesema kuna uhitaji mkubwa wa mazoa ya Kilimo hivyo ni budi kwa Wakulima wa ndani kuhakikisha wanakuzi Kilomo cha ndani ili kuwa na Malighafi za kutosha kwa Wawekezaji, pia amesisitiza kuwa na ushirika kwa Wakulima hao ili kufikia lengo la uzalishaji wa Malighafi hizo.

Katika Kituo cha Kipya cha Mabasi kilichopo Mbezi Luis, Prof Kitila amefika kuangalia fursa za Uwekezaji kwa Wawekezaji wa ndani na wa nje, ameagiza Kituo cha Uwekezaji TIC kufanya uchambuzi wa kutosha kuhusu fursa zinazopatikana.
Share:

ZANTEL YAWAWEZESHA WATEJA KUMILIKI SIMU ZA SMARTA KWA URAHISI KUPITIA MALIPO KIDOGO KIDOGO

 

Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Haba na Haba Hununua Smarta’ iliyofanyika jana. Kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kununua simu aina ya Smarta kwa kulipa kidogo kidogo kuanzia Shilingi elfu moja kupitia akaunti ya Ezypesa. Kushoto kwake ni Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga.
Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga akionesha namna ya kufanya malipo kidogo kidogo kupitia akaunti ya Ezypesa ili kununua simu aina ya Smarta wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ijulikanayo kama ‘Haba na Haba Hununua Smarta’. Kushoto ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa.

Na Mwandishi Wetu | Zanzibar | Kwa kulipa kidogo kidogo kuanzia Shiling elfu moja, wateja wa Zantel wanaweza kununua simu aina ya Smarta ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni kuwawezesha watu wengi zaidi kunufaika na huduma za kidigitali.

Huduma hiyo imezinduliwa chini ya kampeni ijulikanayo kama ‘Haba na Haba Hununua Smarta’ itawawezesha wateja wa Zantel kutunza fedha kidogo kidogo kuanzia shilingi elfu moja (1,000/-) kwenye akaunti za Ezypesa na pale mteja anapofikisha kiwango cha 39,999/- ataweza kukitumia kununua simu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa alisema kama kampuni ya kidigitali imeona kuna haja ya kuja na suluhisho litakalowawezesha wateja kumiliki simu janja bila kuathiri bajeti au matumizi muhimu kwa kulipa kidogo kidogo.

Tunatambua kwamba siyo watu wote wana uwezo wa kununua simu kwa kulipa pesa taslimu (Cash) na ndiyo maana tumekuja na huduma hii ili kuwawezesha wateja kulipa kidogo kidogo na kuwapunguzia mzigo wa kulipa kwa mara moja,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga alisema mbali na kutunza pesa kwa njia ya Ezypesa, kupitia huduma hii wateja wanaweza kuchangiana kwa kumuingizia kiasi cha fedha kwenye akaunti yake ya Ezypesa ili kumuwezesha mmoja wao kumiliki simu janja aina ya Smarta.

Azma yetu ni kuhakikisha kila mtu anafikiwa na huduma za kidigitali na anufaike na fursa zake ikiwamo kujumuika na ndugu jamaa na marafiki lakini pia kufanya shughuli za uchumi.Kupitia huduma hii tumerahisisha zaidi upatikanaji wa simu janja bila kujali kipato cha mteja wetu,” alisema Muga.

Ili kupata huduma hii mteja wa Zantek atatakiwa kupiga *149*15# kisha 0 na kufuata maelekezo.Wateja watakaofanikiwa kufikisha kiwango wataweza kununua simu za Smarta kupitia maduka ya Zantel yaliyopo nchi nzima.

Simu za Smarta ni simu za bei nafuu zaidi sokoni hivi sasa zenye uwezo wa 4G na zinakuja na application mbalimbali ikiwamo YouTube, Google, Facebook na WhatsApp zinazomuwezesha mtumiaji kufurahia huduma mbalimbali za kidigitali.

Kuhusu Zantel:

Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.
Share:

Friday, December 18, 2020

BENKI YA CRDB YAWAPA ZAWADI ZA KUFUNGA MWAKA WANAFUNZI WA VYUONI

  
Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Abel Lasway (katikati) akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa kampeni ya JIPE 5 na Scholar ambayo inaendeshwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo hapa nchini. Kulia ni Meneja wa Udhamini na Matukio wa Benki ya CRDB, Lilian Kanora na kushoto ni Evance Mkao ambae ni Meneja Uhusiano Upande wa Mauzo katika benki hiyo.
Sehemu ya laptop (kompyuta pakato) na smart phone (simu janja) ambazo zitatolewa kwa washindi wa kampeni ya JIPE 5 na Scholar ambayo inaendeshwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo hapa nchini.

Benki ya CRDB imetoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya kampeni ya JIPE 5 ambayo ilizinduliwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa na malengo ya kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba kuelekea mwisho wa mwaka. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Abel Lasway amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 mwezi huu, benki tayari imeshatoa jumla ya zawadi zinazofikia Shilingi Milioni 20. Zawadi hizo zimetolewa kwa wateja zaidi ya 4,000 huku akaunti zaidi ya 74,000 zikiwa zimekwisha funguliwa.

Tunawashukuru sana Watanzania kwa kuipokea vyema kampeni ya Jipe Tano ambapo mafanikio yaliyopatikana sio tu ni kwa faida ya Benki ya CRDB bali yanaonyesha ni kwa jinsi gani Benki ya CRDB imeweza kuwajumuisha Watanzania wengi katika mfumo rasmi wa huduma za fedha,” alisema Lasway.

Meneja huyo mwandamizi alisema katika kampeni hiyo ya Jipe Tano makundi mbalimbali ya wateja yameweza kuzawadiwa ambapo kwa mwezi huu wa Disemba Benki inawazawadia ada za shule wazazi wanaofungua akaunti ya watoto za Junior Jumbo. Jumla ya Shilingi Milioni 30 zimeandaliwa kwa ajili ya kutolewa kama zawadi ya ada kwa akaunti za watoto za Junior Jumbo zitakazofunguliwa mwezi Disemba.

“Benki ya CRDB tunajinasibu kwa kauli mbiu yetu ya “Ulipo Tupo” ambayo haiishii tu kufikisha huduma mahali ambapo wateja wetu wapo bali inalenga kuhakikisha Benki inakua pamoja na mteja katika hatua zote za maisha yake,” aliongezea Lasway.

Sambamba na zawadi hizo kwa akaunti za akiba na watoto, alisema Benki ya CRDB pia ililenga kundi la wanafunzi wa vyuo ambavyo vimefunguliwa hivi karibuni ambapo timu ya mauzo ya Benki iliweka kambi katika vyuo mbalimbali nchini ili kutoa elimu ya masuala ya fedha pamoja na kutoa huduma za kufungua akaunti kwa wanafunzi.

Nimefurahi kuona tumeweza kufanikiwa kuwaingiza katika mfumo rasmi wa fedha wanafunzi wengi na tukaona pamoja na kuwapa huduma hizi tuweze kuwazawadia vitu ambavyo vitarahisha maisha yao wawapo chuoni,” alisema Lasway huku akiongeza kuwa kupitia kampeni hiyo ya wanafunzi ya JIPE 5 na Scholar, jumla ya wanafunzi 100 kutoka vyuo mbalimbali nchini watazawadiwa laptop (kompyuta pakato) na smart phone (simu janja).

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa laptop (kompyuta pakato), Jackline Masayanyika mwanafunzi kutoka chuo cha Mtakatifu Agustino kilichopo jijini Mwanza, amesema kuwa zawadi hiyo itakua msaada mkubwa katika masomo yake ukizingatia uwepo wa fursa nyingi za masomo zinazopatikana mtandaoni.
Share:

TIC YAPOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI UTURUKI

 

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea Ugeni wa wafanyabiashra/wawekezaji kutoka Nchini Uturuki na umejumuisha Makampuni matano. Ugeni huo ukiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof. Elizabeth Kiondo ugeni huo umefika chini ili kukutana na wadau mbalimbali wanaohusika na kuwezesha uwekezaji nchini. 

Vilevile imebainika kwamba ugeni huo umefika nchini kutokana na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji yanayosimamiwa na Kituo cha Uwekezaji kwa wawekezaji Tanzania TIC ambapo muwekezaji anaweza kupatiwa ardhi, usajili wa kampuni, vibali na ushauri wa kimazingira. 

Akizungumza na vyombo vya habari, Mhe.Prof. Kiondo ameeleza kwamba ujgeni huo unawakilisha sekta za kilimo na zana za kilimo, viwanda vya nguo, viwanda vya kutengeneza pampas za watoto na watu wazima, vifaa tiba na dawa na viwanda vya kuunganisha vifaa vya kilimo. 

Pamoja na mambo mengine, ugeni huo umefika ili kueleza nia yao ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. Wawakilishi wa Taasisi zenye jukumu la kusaidia wawekezaji, wameeleza kwamba maeneo wanayokusudia kuwekeza ni miongoni mwa kipaumbele cha Serikali. 

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Taasisi ambayo inahamasisha na kuvutia uwekezaji nchini, imetumia fursa hiyo kuelezea maeneo ambayo nchi inakaribisha wawekezaji hususan eneo la kuongeza thamani bidhaa za kilimo, uvuvi, madini, ufugaji, vifaa tiba, na katika eneo la utalii. 

Naye mmoja ya wageni hao akizungumza na waandiahi wa habari ameeleza kwamba wamekuja Tanzania kwa kuwa wameshafanya uchunguzi na kubaini kuwa Tanzania inakwenda na kasi ya Uchumi wa viwanda hivyo wamefanya maamuzi ya kuweka kiwanda cha kutengeneza pampas na vifaa tiba ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, katika sekta ya uchumi wa Viwanda. . 

Tayari tuna wawekezaji nchini kutoka Uturuki ambao wamewekeza kwenye sekta ya viwanda, elimu, ujenzi, kilimo na madini. 

Mkutano huo pia umehudhuriwa na wawakilishi kutoka TPSF, EPZA, SIDO, TCCIA na TNBC ambapo taasisi zote zimeonesha utayari wa kushirikiana na kampuni hizo katika kufanilisha uwekezaji wao hapa nchini.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive