A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, December 19, 2017

AIRTEL YARAHISISHA MAWASILIANO KWA KILA MTANZANIA

Meneja Masoko Airtel Tanzania Aneth Muga akitoa Maelezo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa blog mbalimbali kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ 

Airtel yafanyia kazi changamoto za watanzania.
Ikiwa na lengo lakurahisisha mawasiliano kwa  watanzania kote nchini.

Moja ya makampuni ya mawasiliano yanayokuwa kwa kasi zaidi nchini, Airtel imesema kwamba itaendelea  kutoa huduma zake  kwa wateja wake kwa ubora zaidi na kwa bei nafuu 
Akiongea na waandishi  wa habari za mitandaoni (Blogers) Meneja  Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando  alisema kwamba maboresho ya vifurushi vya intaneti vimefanywa ili kukidhi hali ya kiuchumi na mahitaji ya  watanzania.

Tumeamua kuongeza kiwango cha Baadhi ya GB  mara mbili ya kile tulichokuwa tukitoa mwanzo kwa bei  ile ile ili kumuwezesha  mtanzania kufurahia thamani ya pesa yake alisema Mmbando.

aliongeza kwakusema kwamba kwa mara ya kwanza  kampuni hiyo imekuja na  kifurushi cha shilingi mia mbili (200)Kifurushi  hiki kinamwezesha mteja wetu kupata  MB 40.

kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Anethy Muga, alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote, na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa kujipatia bando za gharama nafuu na kabambe za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ itamuwezesha mteja wa AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu”
Share:

Monday, December 18, 2017

BENKI YA DTB YAIBUKA KIDEDEA LIGI YA BRAZUKAKIBENKI

Waziri wa Habari sanaa utamaduni na michezo  Dk   Harrison Mwakyembe (kushoto),Akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya soka ya Diamond Trust Benki (DTB), David Kikambako  baada ya timu hiyo kuibuka kidedea kwakuichakaza  timu ya benki ya Exim kwa mikwaju ya penati  katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabenki iliyopewa jina la brazuka kibenki, wa katikati ni Mratibu na Muanzilishi wa ligi hiyo Nasikiwa Berya.
Waziri wa Habari sanaa utamaduni na michezo  Dk   Harrison Mwakyembe  akishangilia pamoja na wachezaji wa benki hiyo kushoto kwa Waziri ni Mratibu na Muanzilishi wa ligi hiyo Nasikiwa Berya.


Wachezaji wa DTB wakifurahia ushindi huku wamembeba kocha wao Michael Lugalela
 Timu ya Exim ambayo imeshika nafasi ya pili katika michuano hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakionesha zawadi zao

Share:

AIRTEL YAZIDI KUWANUFAISHA WATEJA WAKE

 Meneja Masoko Airtel Tanzania Aneth Muga, akitoa Maelezo wakati wa mkutano na watangazi wa radio mbalimbali  nchini  kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ .
 Baadhi ya watangazaji wa radio mbalimbali nchini wakifuatilia mada kwa umakini wakati wa mkutano na watangazi wa radio mbalimbali  nchini  na Airtel kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekutana na watangazi wa radio mbalimbali  nchini  na kuongelea ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia kuzinduliwa kwa  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zilizozinduliwa  mwanzoni mwa wiki hii kwa lengo lengo la kuwapatia wateja na watumiaji wote wa intaneti bando nafuu zaidi.
Meneja Masoko Airtel Tanzania Anethy Muga alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote, na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa kujipatia bado za gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kupata MB 40. Vilevile ofa kabambe ya ‘SMATIKA Yatosha bando’ itamuwezesha mteja wa AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu”
kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Yatosha mpya inakupa bado za siku, wik, mwezi gharama nafuu kuliko zote nchini, kwa mfano bado ya 5,000 zamani ilikuwa na GB 1,  kwa sasa Yatosha Intaneti Mpya unapata  GB 2 kwa siku 7, vile vile kwa shilingi 10,000 zamani ulikuwa unapata bando la GB 2.5 kwa siku 7 lakini sasa tumeliongeza zaidi unapata GB 6 zakutumia wiki nzima. Alieleza Muga
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni ishara ya Airtel kuanza vyema shamrashamra kusherehekea  sikukuu kwa kuwapatia uhakika wateja na watumiaji wa huduma ya intaneti wa kutoishiwa bando kwa muda mfupi,

Ukiwa na Airtel Yatosha Intaneti hainaga kuzima data tena!” Alisisitiza Mmbando.
Share:

Sunday, December 17, 2017

Washindi 12 droo ya pili Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC wapatikana

Maofisa wa NBC wakiendesha droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Humudi Semvua kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Meneja Masoko wa NBC, Alina  Kimaryo, Meneja Amana za Wateja, Dorothea Mabonye na Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos lyimo. Jumla ya washindi 12 wakijishindiaa kila mmoja shs milioni 1.
Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchezeshaji wa droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana ambapo washindi 12 walijishindia kila mmoja shs milioni 1. Katikati ni Meneja Amana za Wateja wa NBC, Dorothea Mabonye na Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos Lyimo.

Meneja Maendeleo ya Biashara wa NBC, Amos Lyimo (kulia) akipiga simu kwa mmoja wa washindi  wakati wa droo ya pili ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humudi Semvua, Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo na Meneja wa Amana za Wateja, Dorothea Mabonye. Washindi 12 walijishindia shs milioni 1 kila mmoja. 


Share:

Friday, December 15, 2017

TMRC YAWATIA MOYO WAGONJWA WA MOYO WALIOKATA TAMAA JKCI

Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa mikopo kwa mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya  akikabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya shilingi milioni nane kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (JKCI), Profesa Mohamed Janabi,   kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto wane (4) ambao wamekosa pesa kwaajili ya matibabu hayo kushoto ni Mkurugenza wa Fedha wa TMRC, Oswald Urassa. Na wengine ni maofisa wa hospitali hiyo makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa Mikopo kwa Mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya wapili ( kushoto) akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni nane kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto wanne (4) ambao hawana uwezo wakupata pesa kwaajili ya matibabu hayo


                                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TMRC YAWEZESHA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO WANNE  

14, DESEMBA 2017 - (DAR ES SALAAM), Kampuni ya Tanzania Mortgage Refinance Limited (TMRC), imetoa msaada wa kiasi cha Shilingi milioni Nane (Shilingi 8,000,000) kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanne jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi mfano wa hundi hiyo ya Shilingi milioni Nane kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (JKCI), Profesa Mohamed Janabi, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa TMRC, Oscar Mgaya, alisema kuwa wameamua Kuitikia wito huu wa kuwasaidia watoto hao ambao hawana uwezo na bila msaada huo pengine wasingeweza kupata huduma hiyo na maisha yao yangekua hatarini.

"Tumeamua kusaidia tiba kwa hawa watoto baada ya kuona tangazo kwenye kituo cha televisheni cha Clouds. Hivyo basi, tukaona umuhimu wa kufanikisha malipo kwa ajili ya upasuaji wa watoto hawa wanne," Bw. Mgaya alisema.

Aidha, Mtendaji Mkuu huyo, alisema taasisi yake hiyo ambayo inatoa mikopo ya ujenzi au ununuzi wa nyumba kupitia mabenki na taasisi nyingine za fedha kuwa, waliamua kutoa kiasi cha Shilingi milioni mbili (Shilingi 2,000,000) kwa upasuaji wa kila mtoto kwa kuwa ni taifa la kesho.  Hii ni sehemu ya kutekeleza wajibu wetu katika jamii (corporate social responsibility).   
"Tumeamua kutoa kiasi kidogo  kwa watoto hawa wadogo ambao miongoni mwao wana ndoto za kuwa wataalamu wa benki, madaktari, marubani n.k. Hivyo, taasisi yetu imeona umuhimu wa kufanya ndoto za hawa watoto kutimia kwa kuwawezesha kupata tiba," alisema.
Bw. Mgaya ametoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia wenye uhitaji wa tiba hii ya moyo hasa kwa wale wenye maisha duni ambapo uhitaji unaelezewa kuwa ni mkubwa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (JKCI), Profesa Mohamed Janabi, alisema kwamba taasis yake imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kupunguza idadi ya wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje ya nchi, kutokana na magonjwa ya moyo na badala yake kutibiwa nchini kwa gharama nafuu.

"Licha ya kuwasaidia watanzania kupunguza gharama kwa matibabu ya moyo hapa nchini badala ya nje ya nchi, pia hii imepunguza sana gharama ambazo serikali imekuwa ikizitumia kila mwaka kutibu maradhi kama hayo nje ya nchi," Prof Janabi alisema.

Tangu taasisi yetu ianze kutoa tiba hii mwaka 2008, tumeweza kupunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya watanzania wanaotibiwa nje ya nchi. Hata hivyo, ameishukuru TMRC, kwa msaada wa fedha kwa ajili ya tiba kwa watoto hao wanne na kuziomba taasisi nyingine kuiga mfano.

“Taasisi yetu inahamasisha watu kuchangia milioni 2 kwa ajili ya watoto walio katika hali ngumu na kiasi kingine kinachangiwa na serikali. Kwa wiki hii tumejipanga kufanya upasuaji kwa watoto 60  na hii ndiyo zawadi ya Sikukuu ya Krismas toka kwetu,” alisema Prof. Janabi.

Hadi sasa, Prof. Janabi alisema kuwa watoto 300 wameshafanyiwa upasuaji wa moyo toka Januari hadi sasa ingawa lengo ilikuwa ni kufikia watototo 400.

Akizungumzia kuhusu uhitaji wa huduma hii ya upasuaji wa moyo, Prof. Janabi alisema kuwa ni mkubwa sana ambapo kati ya watoto miloini 2 wanaozaliwa, asilimia 1 wanatatizo la moyo.

“Miongoni mwa mambo yanayosababisha tatizo la moyo kwa watoto linatokana na wazazi kutozingatia chanjo, lishe nakadhalika,” alisema
Share:

Wednesday, December 13, 2017

TMRC YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI MBILI KITUO CHA KULELEA YATIMA KIWALANI

Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa mikopo kwa mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akikabidhi msaada wa vyakula pamoja na mahitaji muhimu ya kibinadamu kwa Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias Mwakalukwa, kushoto ni Mkurugenza wa Fedha wa Taasisi hiyo, Oswald Urassa.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa Mikopo kwa Mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula pamoja na mahitaji muhimu ya kibinadamu yenye thamani ya shilingi Milion 2  kwa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,kushoto ni Mlezi Mkuu wa Kituo hicho Elias Mwakalukwa wengine ni maofisa wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa mikopo kwa mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas kwa mwakilishi wa Wanafunzi wa Kituo hicho.
                              
                              



                                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TMRC YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KIWALANI  

13, DESEMBA 2017 - (DAR ES SALAAM), Kampuni ya Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC), imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili (Shilingi 2,000,000) kwa Kituo cha Watoto yatima cha Kiwalani (Kiwalani Orphanage Centre) kilichopo jijini Dar es Salaam.

Zawadi hizo zimekabidhiwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bw. Oscar P. Mgaya kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mchungaji   Elias Mwakalukwa -, katika ghafla iliyofanyika kwenye Kituo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa kituo hicho cha watoto yatima ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, unga wa sembe, maharage sabuni za kufulia na kuogea, sukari ,  chumvi,  dawa za meno, majani, kalamu na madaftari

“Kwa upendo wetu wa dhati kabisa tumeona umuhimu wa kushiriki pamoja na watoto yatima, ambao wapo katika mazingira magumu, katika kusherehekea Sikukuu ya Krimas mwaka 2017,” alisema Bw. Mgaya.

Bw. Mgaya, alisema kuwa taasisi yake imeamua kujumuika na watoto hawa yatima katika kuelekea kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa kutoa zawadi mbalimbali za vyakula kama njia ya kuwafanya wajisikie furaha.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu huyo, amezitaka taasisi nyingine na watu binafsi kujitoa kwa dhati kuwasaidia watoto  walioko maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mchungaji   Elias Mwakalukwa, ameishukuru TMRC, kwa msaada huo na ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano wao.
“Tunaishukuru sana TMRC, ninyi mmeonyesha mfano na hakika mmeonyesha upendo wa dhati kwa watoto hawa. Niziombe taasisi nyingine kuchukua mfano huu uliofanywa na taasisi yenu,” Mchungaji   Elias Mwakalukwa alisema.

Aliongeza kuwa uhitaji wa misaada kwa kituo chake ni mkubwa, lakini taasisi yao inapata faraja kupata wadau wanao ona umuhimu wa kusaidia watoto hao yatima.
Share:

Tuesday, December 12, 2017

Airtel yaja na bando mpya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano (kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo  itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA GB 1  ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda Hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Isack Nchunda  (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo  itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA GB 1  ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu (kulia), ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano, Hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano, wakionyesha bango lemye aina mbalimbali za bando za huduma hiyo baada ya uzinduzi huo. Picha na Brian Peter

Airtel yaleta ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ SMATIKA NA 1GB  siku tatu kwa 2000 tu f
  • ‘SMATIKA NA 1GB Yatosha Intaneti inayokupa muda mrefu kwa gharama nafuu zaidi.
Airtel Tananzania Mtandao bora kwa Smartphone yako imewapatia wateja wake uhuru zaidi kwa kuwaletea  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ maalum kwa watumiaji wa huduma za intaneti.   

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Isack Nchuna wakati wa hafla ya kuzindua ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti, alisema “Airtel itaendelea kuleta huduma zenye ubora na ubunifu wa hali ya juu ili kuendelea kuwa  sambamba na mahitaji ya wateja katika huduma za intaneti ambapo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa Airtel imejiwekea mikakati endelevu mingi ili kukidhi uhitajika na wateja wote”

“Tuaendelea kudhihirisha dhamira yetu ya kutoa suluhisho la mawasiliano kupitia uzinduzi wa ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ kwa kutoa huduma nafuu ya Intaneti kwa watumiaji wote nchini  huku tukiweka kipaumbele zaidi katika ubora wa mtandao pamoja na kuwapatia  wateja uhuru zaidi” aliongeza Nchunda.
 
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni zawadi ya awali kabisa tunayowapatia watumiaji wa Airtel katika msimu huu wa sikukuu, tunaamini kuwa ndani ya msimu huu wa sikukuu wateja wanauhitaji mkubwa sana wa intaneti katika kukamilisha 

shamrasharna wakiwa wanawasiliana na ndugu, jamaa na marafiki  wakati wote!”
Akifafanua  zaidi Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano alisema Bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote wa airtel kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote.

“Mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kujipatia MB 40, vilevlie mteja ataweza KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu” alieleza Bi Singano.

“kujiunga na ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ unatakiwa kupiga *149*99# kisha chagua 5 Yatosha Intanet vilevile  unaweza kujiunga kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kisha chagua  Yatosha Intanet”.

Airtel Tanzania imekuwa katika programu ya uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano yake ili kukamilisha lengo lake la kutoa mawasiliano bora  na yenye uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya U900. Tayari Airtel imezindua maboresho ya mtandao wake kwa kutumia teknolojia hiyo ya U-900 kwenye mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Mwanza huku ikiendelea kuwahakikishia wateja wake mawasiliano bora hasa katika maeneo ya nje na ndani ya majengo marefu au yenye uhitaji zaidi.

Share:

Tuesday, December 5, 2017

Vijana wahitimu wa vyuo kunufaika na programu ya Wajibika ya Benki ya NBC

Mmoja wa waratibu wa programu ya  Wajibika wa Benki ya NBC, Imani Sinkonde (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu  Programu ya Wajibika yenye lengo la kuwaandaa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi.
Mmoja wa waratibu wa programu ya  Wajibika wa Benki ya NBC, Loveness Mseke (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu  Programu ya Wajibika yenye lengo la kuwaandaa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi.

Mmoja wa waratibu wa programu ya  Wajibika wa Benki ya NBC,Rahma Suleiman (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), jijini Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu  Programu ya Wajibika yenye lengo la kuwaandaa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi.

Mmoja wa waratibu wa programu ya  Wajibika wa Benki ya NBC, Emanuel Agostino (kulia), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia na Uongozi Kilimanjaro jijini Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu  Programu ya Wajibika yenye lengo la kuwaandaa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi.

Mmoja wa waratibu wa programu ya  Wajibika wa Benki ya NBC, Michael Mwangoka (kulia), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia na Uongozi Kilimanjaro jijini Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu  Programu ya Wajibika yenye lengo la kuwaandaa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi.


Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive