A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Sunday, March 20, 2022

JUKWAA LA "Getpaid" KUTOA FURSA KWA VIJANA WA KITANZANIA

 

Mkuu wa Kitengo cha Biashara-GetPaid, Bw. Justine Mahinyila, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa la GetPaid, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Mpiga Picha Wetu

Washiriki wakifuatia  mijadala jinsi ya kutumia la Jukwaa la GetPaid, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa hili jijini Dar es Salaam jana. (Mpiga Picha Wetu)


Jukwaa la “GeitPaid” kutoa fursa kwa watanzania

 

Na Mwandishi Wetu

 
Jukwaa la Kijidital, “GetPaid” lenye lengo la kutoa fursa za Ajira na nyinginezo limezinduliwa jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mchango wa sekta binafsi kusaidia mikakati ya serikali inayolenga kupanua wigo wa fursa kwa vijana na watanzania kwa ujumla.

 
Mbali na mambo megine Jukwaa la GetPaid,  litasaidia Tanzania kupunguza wimbi kubwa la ukosefu wa ajira—kwa vijana na watanzania wote (wasomi na wasio soma,  amesema Bw. Richard Lema, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania DLT CP iliyobuni  na kutengeneza Mtandao wa GetPaid—wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa hilo jijini Dar es Salaam jana.

 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Lema, GetPaid ni jukwaa la kimkakati la kidijitali ambalo lengo lake kuu ni kuwaunganisha watanzania, ikiwa nia pamoja na vijana,  wafanyabiashara, wasomi, wasio soma, wajasiriamali, wanaofanyakazi binafsi na fursa mbalimbali duniani.

 
"Kwa kweli, hili ni jukwaa la kidijitali la pekee, ambalo linawaunganisha watu—wasaka fursa na watoa fursa, " ameongeza Bw. Lema

 
Alielezea GetPaid kama ni teknolojia ya kisasa, ambayo itawaunganisha watu na fursa mbalimbali kitaifa, kikanda na kidunia.   

 
Kwa njia ya jukwaa la GetPaid, watu wa aina mbalimbali – wazalishaji,  wafanyabiashara, wanaofanya kazi binafsi, watu wazima, vijana, wenye weledi na wasio na weledi - watawezeshwa kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo Afrika na nje ya Afrika.

 
"Jukwaa la GetPaid linawafanya waweze kunufaika na fursa mbalimbali duniani, elimu ya kidijitali na uvumbuzi. Hili linafanyika kupitia kikundi cha jumuiya, utumiaji rahisi na elimu," alisema Bw. Lema na kuongeza kwamba "bidhaa ya GetPaid ina vitu vitatu na inawapa watumiaji (waanzilishi, wafanyabiashara na wafanyakazi binafsi vifaa na elimu wanayohitaji kuishi, kufanyakazi na kupata ujira."

 
Akizungumza wakati wa uzinduzi, mtaalamu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari (ICT) Baraka Mafore alisema ingawa kuna ukuaji wa kasi wa uchumi wa kidijitali, bado kuna pengo kubwa linalotakiwa lijazwe, kwa vile mamilioni ya vijana katika nchi nyingi za Afrika hawana ajira.

 
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba pamoja na kwamba vijana wanaomaliza chuo na kuingia kwenye soko la kazi Tanzania wanaanzia 800,000 hadi 1,000,000 kila mwaka (NBS-2015), kwa wastani uchumi unatengeneza ajira zipatazo 250,000 tu kwa mwaka na asilimia 75 ya hawa vijana wanabaki bila ajira.

 
"Hata hivyo, kutumia njia na vifaa sahihi, kama jukwaa la GetPid, nchi za Afrika zinaweza kushuhudia idadi kubwa ya vijana wakijiunga na kuingia kwenye uchumi wa kidijitali," alisema mhitimu mmoja kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Asha Mkwezu wakati wa uzinduzi wa GetPaid APP.

 
DLT CP-Tanzania ni kampuni iliyosajiliwa na inamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania wenye vipaji ambao wameingia kwenye "huu uchumi wa kidijitali."
Share:

Wednesday, March 16, 2022

KONNECT TANZANIA YAFANYA UZINDUZI RASMI WA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI NCHINI

 Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi rasmi wa mtandao wenye kasi zaidi nchini Konnect utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.Meneja Mkuu wa Konnect Tanzania Bw. Philippe Baudrier akizungumza na wadau mbalimbali pamoja na maofisa kutoka Konnect wakati wa ghafla maalumu ya uzinduzi rasmi wa mtandao mpya wa satelaiti nchini utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.


Mshereheshaji wa shughuli ya uzinduzi rasmi wa mtandao wa Konnect Bernice Fernandez akizungumza na wadau mbalkimbali pamoja na maofisa wa Mtandao wenye kasi zaidi Konnect wakati wa shughuli ya uzinduzi wa Mtandao huo utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.


Baadhi ya wageni waalikwa na wana habari wakiwa katika majukumu yao kusikiliza na kufatilia uzinduzi rasmi wa mtandao wenye kasi zaidi konnect utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.





Konnect Tanzania yajenga daraja la usawa wa kidigitali Tanzania

Dar Es Salaam, Tanzania, Machi 16, 2022 – Konnect Tanzania, iliyosajiliwa kama: “Konnect
Broadband Tanzania Limited” ni kampuni tanzu ya Eutelsat iliyojitolea kutoa huduma za kasi
zaidi za satelaiti. Kampuni imetangaza kuzindua ofa mpya ya mtandao wa satelaiti nchini
Tanzania yenye kasi ya hadi 100Mbps. Pamoja na leseni zote na kibali cha kiserikali, Konnect
Tanzania ina vibali vyote vinavyohitajika ili kuweza kutoa huduma za kimtandao wa bei nafuu
nchini.


Kulingana na Utafiti wa Uchumi wa Simu wa GSMA wa 2021, chini ya 28% ya watu katika Afrika
Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaweza kupata mtandao wa simu. Hii inashiria kuwa kuna
sehemu nyingine ulimwenguni ufikiaji wake ni wachini kama vile Europe na zaidi ya 80% ya
watu wameunganishwa. Uchumi wa intaneti barani Afrika una uwezo wa kufikia dola bilioni 180
ifikapo 2025, ambayo ingewakilisha 5.2% ya Pato la Taifa la bara kupitia kupanua matumizi ya
kidijitali, ukuaji wa miji na kupenya kwa simu mahiri.


Utoaji wa huduma za uhakika na haraka kote Tanzania ni muhimu kwa kuzingatia upenyezaji
mdogo wa intaneti nchini, iliyo chini ya 20%. Huku muunganisho ukiwa juu zaidi, huduma za
mtandao wa Konnect Tanzania, zilizoundwa na kupangwa kwa mahitaji ya ndani, sasa
zinapatikana kwa watumiaji wa aina zote nchini kote, kuanzia majumbani na biashara hadi
mamlaka za umma.


Meneja Mkuu wa Konnect Bw. Philippe Baudrier alieleza kuwa: “Huduma za mtandao wa
Konnect zimeundwa kukidhi mahitaji ya makazi na SMBs (wafanyabiashara wadogo na wa kati)
lakini pia zinaweza kusaidia katika maendeleo ya sekta mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo,
utalii, madini, elimu na afya.

Mtandao wa satelaiti ya kasi ya juu na uboreshaji wa sekta ya kilimo Tanzania
Mtandao wa kasi wa juu ni ufunguo wa kuboresha shughuli za kilimo ambazo zinawakilisha
26,74% ya pato la taifa la Tanzania. Kuongeza tija katika sekta ya kilimo sio tu kukuza Pato la
Taifa,bali kutaongeza maendeleo ya taifa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kitaifa wa Kikundi cha Wakulima nchini Tanzania Bw
Stephen A. Ruvuga alisema kuwa: “Mashamba mengi ya kilimo nchini Tanzania yapo katika
maeneo yaliyotengwa na hakuna mtandao wa intaneti. Kuunganisha mashamba haya kwa
mtandao wa satelaiti kutawawezesha wakulima kukusanya data muhimu kama vile unyevu wa
udongo na viwango vya mabwawa, pamoja na ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuboresha ufanisi
kwa kasi.


Kusaidia Sekta ya Utalii ya Tanzania katika ufufuaji wake baada ya Janga
Uwepo wa mtandao wa Kasi katika nyumba za kulala wageni utaongeza usalama na mvuto
katika sehemu za kitalii Tanzania, ambao umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na janga la
kimataifa na mchango katika Pato la Taifa kushuka kutoka 10.7% mwaka 2019 hadi 5.3% mwaka
2020. .


Bw. Kennedy Edward, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Hoteli za HAT Tanzania aliangazia:
“Wajasiriamali wa utalii wa Tanzania wanahitaji mtandao wa uhakika ili kutoa huduma bora,
kukuza ujuzi, na kufungua masoko mapya. Kwa vile tovuti nyingi nzuri zaidi za Tanzania ziko
katika maeneo ya mbali, Broadband ya satelaiti ya Konnect inaweza kusaidia sekta ya utalii kwa
kutoa muunganisho wa intaneti kwa wageni na wafanyakazi katika nyumba za kulala wageni,
zisizoweza kufikiwa na mitandao ya kitamaduni.”


Kuongeza usalama na tija katika sekta nzima ya madini
Janga la Covid-19 limeharakisha kwa kiasi kikubwa sekta ya madini kufahamu faida za mtandao
wa kasi wa juu. Idadi kubwa ya tovuti za uchimbaji madini za Tanzania ziko katika maeneo
yaliyotengwa bila muunganisho wa Wi-Fi au 4G.


Bw. Peter Kabepela, Naibu Mkurugenzi wa chama ya wachimbaji madini Tanzania: “Kuunganisha
migodi ya mbali ya Tanzania kwenye mtandao wa satelaiti kutaongeza tija na kuchangia katika
kulinda eneo lao. Pia itaboresha hali ya maisha ya mafundi wanaofanya kazi kwenye maeneo ya
uchimbaji madini yaliyo mbali na makazi yao.” Shukrani kwa muunganisho wake wa kasi wa
satelaiti, mtandao wa satelaiti wa Konnect ni nyenzo dhabiti katika kusaidia ukuaji wa mchango
wa Pato la Taifa wa sekta ya madini kutoka 3,5% hadi 10% ifikapo 2025.


Kujibu hitaji muhimu la mtandao wa bei nafuu wa kutegemewa wa kasi ya juu kote Tanzania
kutatoa manufaa mengi ya kijamii na kiuchumi. Kuongeza usawa wa kidijitali nchini Tanzania
kwa hakika kutakuwa na manufaa kwa maendeleo ya kiuchumi na kibinadamu na riziki; kusaidia
kuifanya nchi kuvutia na kustahimili.

Hatua rahisi za kusakinisha mtandao mpana wa satelaiti wa kasi zaidi wa Konnect
Kufikia mtandao mpana wa satilaiti ya kasi ya juu sana wa Konnect kunahitaji hatua kadhaa
rahisi. Wateja wanaweza kutembelea tovuti ya Konnect (www.konnect.com), kuzungumza moja
kwa moja na huduma kwa wateja kwa kupiga nambari +255 768 132 829 kuanzia saa 3.00
asubuhi mpaka saa 12.00 jioni au kwenda kwenye duka la washirika lenye leseni ili kukutana
moja kwa moja na mshiriki wa timu ya Konnect. Wafanyakazi waliojitolea watasaidia wateja
kuchagua kifurushi sahihi na kupanga usakinishaji wa haraka. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya
kujisajili kama mshirika tafadhali tembelea Konnect.com

About Konnect
Konnect is the Eutelsat Group entity in charge of retail marketing for a new generation of superfast
satellite broadband services. As its implementation accelerates, Konnect is redefining the connectivity
expectations of people who live and/or work outside the geographical boundaries of fibre, enabling
them to access an immediately available service with ultra-fast, unlimited and competitive offers of up
to 100Mbps. To find out more about Konnect's offers, visit www.konnect.com.

Contact

Name: Obafemi AGBANRIN
Tel: +255 767 256 405
Email: oagbanrin@eutelsat.com

Share:

Sunday, March 13, 2022

WANAWAKE KKKT BOKO WAFANYA MATEMBEZI YA SHUKURANI

 

.com/img/a/
Mwenyekiti wa Wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Sylvia Lupembe, akizungumza wakati wa matembezi ya shukrani 2022 yaliyowashirikisha wanawaka wa kanisa hilo..com/img/a/

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boko, Ambakisye Lusekelo (wa pili kulia) akiongoza matembezi ya Shukrani ya kilometa 5 yaliyoanzia Kanisa la KKKT - Boko na kuishia katika ufukwe wa Ndege Beach Mbweni jijini Dar es Salaam leo Machi 12, 2022. Matembezi hayo yakiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia ambapo Umoja wa Wanawake wa Usharika huo wametumia fursa hiyo kuhamasishana katika kuwachangia watoto waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambao wakisumbuliwa na ugonjwa wa saratani.

.com/img/a/
.com/img/a/
.com/img/a/
.com/img/a/
.com/img/a/
.com/img/a/
Share:

Friday, March 11, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAMFURAHISHA RC MONGELLA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati), akikata utepe  kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha kushoto ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, pamoja na  Meneja wa Tawi la Tanzania Commercial Bank  Usa river, Speratus Kamala.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la benki hiyo jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi,wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha kulia ni Meneja wa Tawi hilo Speratus Kamala. 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi,wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha

 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi wakifungua pazia kwenye jiwe la msingi  kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha.

 
 
 
Tanzania Commercial Bank (TCB) yazidi kuchanja mbuga kutanua huduma zake imeendelea kuongeza jitihada kuwafikia Watanzania nchi nzima
Tanzania Commercial Bank imeendelea na juhudi zake za kuendelea kutanua huduma zake kwa kufungua matawi katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha kila mtanzania anaitumia Tanzania Commercial Bank.


Benki hiyo imetimiza haja yake hiyo kupitia huduma zake mbalimbali katika kuigusa jamii kwa kufungua tawi jipya katika mkoa wa Arusha wilaya ya Arumeru USA river katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali.


Tawi la USA River lilianzishwa mwaka 2007 kwenye ofisi za posta, Usariver ikiwa ni benki ya kwanza kufika na kutoa huduma za kifedha katika wilaya ya Arumeru Katika mkoa wa Arusha, Benki ya Biashara Tanzania ina matawi sita (6) Arusha Meru,Usariver, Rombo, Mto mbu,Sokoine na Tanzanite.
 

Tawi la Usariver lina jumla ya mawakala 60 ambao wamesambaa katika wilaya ya Arumeru pamoja na kusogeza huduma za kibenki kwa wananchi, Tanzania Commercial Bank pia inategemewa kufungua na kuendeleza fursa mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kuinua uchumi katika mkoa huo


Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, alisema wateja wa benki hiyo wapo katika mikono salama na kuwaomba wananchi waitumie benki hiyo kwani imekuwa ikifanya mambo mengi yanayolenga jamii.


“Benki imepata mafanikio makubwa, kwa sasa Tawi la Usariver lina jumla ya wateja 5,916 wanaofurahia huduma mbalimbali za kibenki hususani mikopo yenye riba nafuu kama ya kilimo, biashara, watumishi na wastaafu pamoja na kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ndani na nje ya nchi.

Lakini vilevile, Tanzania Commercial Bank ni wabunifu kwenye upande wa kidigitali tumeanzisha huduma ya kuweka akiba kwenye vikundi ambayo tumeshirikiana naVodacom na tumeshakusanya zaidi ya Tshs bilioni 27 lakini pia sisi ni wamiliki wa huduma ya Songesha ni huduma inayomuwezesha mteja kukamilisha miamala pale anapokua hanasalio. 


Lakini kikubwa zaidi, Benki yetu imefanikiwa kutoa kadi za Visa, hivyo basi wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla karibuni sana mjipatie Visa ATM card kwa kufanikisha miamala yeyote popote mlipo Kwa kipindi cha mwaka 2020 mpaka February 2021 tawi limeweza kutoa mikopo ya kiasi cha Tshs 5.78 Billioni  kwa wadau mbalimbali.


 Kuna jumla ya mawakala 60 wanaotoa huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha. Kukua kwa biashara kumefanikisha benki kuhama kutoka katika ofisi ndogo za TPC na kuhamia katika jengo Jipya tunalolizinduliwa leo lenye nafasi kubwa na kuwezesha kutoa huduma kwa ubora na umahiri zaidi.


 Kwa sasa tawi lina wafanyakazi 12 waliobobea katika mambo ya fedha na benki wakitoa huduma bora na kwa weledi wa hali juu.


“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo ya huduma za jamii; Tumefanikiwa kutoa misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa bweni la Shule ya sekondari ya wasichana Nduruma.”
Ni matarajio yetu kuwa biashara itaendelea kukua na kutuwezesha kufungua matawi katika kila wilaya ili kuwezesha bidhaa na huduma zetu kuwafikia watanzania wote kwa ukaribu zaidi .”


Benki imechangamkia fursa ya kukua katika wilaya ya USA river, huku pia ikipanua uwepo wetu nchini.
Tawi linapatikana kwa urahisi, huduma zote za kibenki zipo, pamoja na timu ya wataalam wenye ujuzi. Tunatazamia kukutana na wakazi wa USA river, wafanya biashara na fursa zinazoifanya Benki ya Biashara ya Tanzania kuwa mahali pazuri pa kufanya kazi.


Tanzania Commercial Bank pia inatoa huduma za Kibenki Mtandaoni kama vile Internet Banking, Mobile App & Mobile Banking. Lakini Benki pia iko karibu na wateja wake kupitia vituo vyetu vya Huduma kwa Wateja.


Mkuu wa Mkoa Arusha, alitoa shukrani kwa Benki kuweza kuwafikia wananchi wa Usariver na alitoa wito kwa wananchi ili kuweza kuchangamkia fursa hususani makundi ya kina mama kwasababu Tanzania Commercial Bank, ina akaunti maalum kwa ajili ya wanawake.


Aliongeza kwa kuishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kuendelea kuwekeza katika mkoa huo na kuwataka waendelee kuwekeza katika wilaya zote za mkoa huo.


Mongella amewasisitiza wananchi wa Arusha wajitokezea kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Tanzania Commercial Bank kwani imekuwa benki ya kwanza kuwajali na kuwasogezea huduma wananchi wa mkoa huo.


Kuhusu Tanzania Commercial Bank

Tanzania Commercial Bank Plc ni taasisi ya fedha iliyoundwa kisheria kutoka iliyokuwa
Benki ya Posta Tanzania (Tanzania Post Bank). Mtandao wa Tawi la Tanzania Commercial
Bank una jumla ya matawi 82 Tanzania nzima ikijumuisha bara na visiwani yenye makao
yake makuu jijini Dar es Salaam. TCB inatoa bidhaa na huduma ili kukidhi mahitaji ya
benki ya kibinafsi na ya biashara ya wateja. Tembelea tovuti yetu kujifunza zaidi
www.tcbbank.co.tz
Share:

Wednesday, March 9, 2022

ABSA TANZANIA KUDUMISHA HAKI NA USAWA WA MAENDELEO KWA WAFANYAKAZI WAKE

 
Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick Foya (wa sita kushoto), akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake jijini Dar es Salaam Jana. Absa iliandaa hafla hiyo kwa ajili ya Wanawake wateja wao, watoa Huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Pamoja naye ni baadhi ya viongozi wa Absa wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed (wa nane kushoto).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro (wa pili kulia) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume (kushoto) huku Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdi Mohamed akiangalia katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa kwa ajili ya baadhi ya wateja wake wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (kulia) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya baadhi ya wateja wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (katikati) akipokea tuzo ya shukrani kuwa mgeni rasmi kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya baadhi ya wateja wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- (Redskirts), Irene Sengati- Giattas.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro (wa pili kulia) akipokea tuzo ya shukrani kuwa mtoa mada kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Benki ya Absa Africa, Elizabeth Willilo katika hafla ya Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas na Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa benki hiyo, Esther Maruma.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume (wa pili kulia) akipokea tuzo ya shukrani kuwa mtoa mada kutoka kwa Mkuu wa wateja Wadogo wa benki hiyo, Ndabu Swere wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na benki ya Absa jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas na Mkuu wa Vipaji, Mafunzo na Uongozi wa Absa, Veronica Muumba.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa pili kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Ndabu Swere katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa baadhi ya wateja wake wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wa Absa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Benki ya Absa Tanzania, Eveline Kamara wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa Absa. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (katikati) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji uliotukuka Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Mauzo ya Masoko ya Nje, Irene Rwegalulira wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wanawake watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa Absa. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Ofisa katika kitengo cha wateja binafsi, Irene Msungu wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake benki hiyo. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Vipaji, Mafunzo na Uongozi wa Absa, Veronica Muumba, katika wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dkt. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Kitengo cha Malipo wa Benki ya Absa Tanzania, Jane Mbwilo katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa Absa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (wa tatu kushoto) akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo huku wakionyesha alama ya usawa wa kijinsia ambayo ni kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam Jana.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Red Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa pili kulia) na Mjumbe wa Bodi ya Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume, wakikata keki katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na benki Absa kwa ajili ya baadhi ya wateja wake wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Share:

Tuesday, March 8, 2022

TUME YA PAMOJA YA FEDHA (JFC) YASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA MWANAMKE DUNIANI.

 

 

.com/img/a/
 Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika maandamano walipoungana na wanawake wengine  duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake duniani katika viwanja vya Uhuru jiji Dar es Salaam ambapo maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Visiwani Zanzibar ikiwa mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani

 
.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/
Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika picha za matukio mbalimbali

 

 Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  ambayo hufanyika kila Machi 8 ambapo wanawake hao wameonyesha kujiamini katika kutenda kazi kwa maendeleo ya Taifa kama kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani Kizazi cha Haki na Usawa katika Maendeleo Endelevu,wafanyakazi hao walikuwa na shamlashala za za namna yake katika katika viwanja vya uhuru jijini Dar es Salaam.


KATIKA Maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani  Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) imetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu hassan kwa jitihada za kuwawezesha Wanawake katika sekta mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo na mwakilishi wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC)   alieleza kuwa katika  Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) imezingatia  kuwapa kipaumbele wanawake  na kutoa majukumu sawa na wanaume ili kutekeleza kauli mbiu ya Siku ya wanawake duniani.
Share:

Sunday, March 6, 2022

Tanzania Commercial Bank blue economy commitment excites Mwinyi

The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Hon. Dr. Hussein Ali Mwinyi, speaking during the opening of the Zanzibar Women Entrepreneurs Conference organized by Tanzania Commercial Bank at the Golden Tulip Kiembesamaki Hotel in Zanzibar City.

The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Hon. Dr. Hussein Ali Mwinyi and Chairman of the Board of Directors of Tanzania Commercial Bank (TCB), Edmund Mndolwa opening the door to mark the official launch of the Zanzibar Women's Forum organized by Tanzania Commercial Bank (TCB) The witnesses are the First Lady of Zanzibar who is also the Chairperson of the Zanzibar Better Life Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, Chief Executive Officer of Tanzania Commercial Bank, (TCB), Sabasaba Moshingi and leadership from the Government of Zanzibar and Officials from Tanzania Commercial Bank

 The First Lady of Zanzibar Mama Mariam Mwinyi who is also the Chairperson of the Zanzibar Life Better Foundation (ZMBF) and (second left), receiving a check for ten million shillings from the Chief Executive Officer of Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi, to fund the Zanzibar Foundation for Better Life Foundation (ZMBF), during the opening ceremony of the Zanzibar Women's Conference organized by Tanzania Commercial Bank and officially opened by the President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Hon. Dr. Hussein Ali Mwinyi (right to Mother) and (left to Mother) is the Chairman of the TCB Board of Directors Mr. Edmund Mndolwa.


Tanzania Commercial Bank (TCB) commitment and readiness to support prosperity of the blue economy in Zanzibar has impressed President Hussein Mwinyi who yesterday said the lender was doing a commendable job in advancing national development causes.
 
Dr Mwinyi showered TCB with the compliments in his speech to grace the opening of Zanzibar’s Business Forum for Women noting that the networking platform to make finance work for women was a good example of the good work it is doing.
 
According to him, the women empowerment forums are a noble TCB idea that accords women a rare opportunity to deliberate pertinent issues affecting their welfare and learn how they can meaningfully contribute to national development efforts.
 
He said the initiative was worth the investment since it promotes and shows the pivotal role of women in national growth and development endeavours such as the blue economy, which his administration has embraced for spearheading inclusive prosperity and sustainable development in the Spice Islands.
 
“TCB decision and engagement to organize and run these special enlightening forums to deliberate issues affecting women’s personal and national development issues whose ultimate goal is to better their welfare has impressed me a lot,” Dr Mwinyi told the roundtable’s participants.
 
Themed, The Role of Women in Blue Economy Growth for Sustainable Development, the one-day forum was also attended by senior officials in the Revolutionary Government of Zanzibar and TCB senior leaders led by Board Chairman Dr Edmund Mndolwa and CEO Sabasaba Moshingi.
 
Yesterday’s gathering, which attracted more than 300 empowerment eager women, was the fourth to be held since the launch of the initiative last October in Dodoma that was followed by the roundtables in Mbeya and Mwanza.
 
TCB plans to organise similar conferences in other parts of the country, including Dar es Salaam, Tanga and Arusha, as it seeks to showcase commercial and entrepreneurship opportunities in its innovative financial solutions in a bid to empower women economically and contribute to their financial independence.
 
“In that regard, I am overwhelmed to see this bank coming with the forums’ idea for educating and mobilising women in Zanzibar and the whole of Tanzania to seize the opportunities emanating from our plans and strategies to promote the blue economy,” Dr Mwinyi noted.
 
He said TCB commitment to support women participation in the key sectors of the blue economy such as fisheries, marine transport and ocean tourism was strategically vital that should be emulated by other stakeholders. He said the government was aware of women’s contribution in seaweed farming therefore the forum should be used to show ways to modernise it.
He said the authorities will continue supporting women seaweed farmers with capital, working tools and markets for selling their produce as well as support other women groups in their productive activities.
 
“The response and involvement of financial institutions in the development of the blue economy gives us hope to succeed in our efforts to sustainably harness ocean and coastal resources to spur economic growth, improve livelihoods and create jobs in the cpountry,” Dr Mwinyi pointed out.
 
“I call upon wananchi to cooperate with these institutions as well as both local and foreign investors in the endeavour to develop the blue economy. Let us fully utilise the opportunities our banks are providing in that regard,” he added.
 
Speaking early, CEO Moshingi said the blue economy initiative has the potential to make Zanzibar the Singapore and Mauritius of East Africa. He said TCB fully supports the isle’s ambitious blue economy agenda and is ready to work closely with the Revolutionary Government of Zanzibar to realise the noble mission.
 
According to him, the oldest bank in the country in which Zanzibar has a three per cent stake in its shareholding has the financial muscle, innovation prowess and unrivalled market reach to support the blue economy venture.
 
Mr Moshingi showed and proved that in a presentation on the bank’s strong financials and history. He said TCB’s recent successful transformation journey has made it among the most profitable banks in the country that boasts of a health and growing balance sheet.
    
    
   

Share:

Saturday, March 5, 2022

NGAIZA FOUNDATION KUSHIRIKIANA NA DC ALBERT MSANDO KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI WILAYA YA MOROGORO

 .com/img/a/

Wasema lengo ni kuhakikisha ifikapo 2025 suala la Migogoro Wilaya ya Morogoro linabaki historia. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. ALBERT MSANDO kwa kushirikiana na Taasisi ya NGAIZA FOUNDATION wanataraji kuendesha zoezi la utatuzi na usuluhishi wa Migogoro mbalimbali Wilayani humo ili kuiwezesha Serikali kupunguza changamoto hiyo.

 

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bi. ELIZABETH NGAIZA amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na miongoni mwa Mambo yatakayoshughulikiwa ni pamoja na Migogoro ya Ardhi, Mirathi, usuluhishi wa Migogoro ya ndoa pamoja na suala la matunzo ya mtoto. Aidha NGAIZA amesema Taasisi hiyo itatoa huduma hiyo bila malipo Chini ya Wataalamu wa masuala ya kisheria na utatuzi waliojitoa kuhakikisha kila Mwananchi atakaewasilisha kero na changamoto yake anasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi Jambo lake.

 

 Hata hivyo Bi. NGAIZA amesema tayari Taasisi yake imefanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. ALBERT MSANDO ambae amepokea kwa mikono miwili Jambo hilo na ameahidi kushirikiana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa. Pamoja na hayo amesema anaamini kupitia Usuluhishi itasaidia kupunguza mlundikano wa kesi zisizo na ulazima Mahakamani kwakuwa kipaombele Cha Taasisi hiyo ni upatanishi na pale inaposhindikana ndipo kesi zifikishwe ngazi ya Mahakama. Sanjari na hayo ametoa wito kwa Wananchi Wenye Migogoro kujitokeza kwa wingi kuwasilisha mashauri yao.

Share:

Thursday, March 3, 2022

KAMPUNI YA TANGA CEMENT YAWATAKA WADAU KUSHIRIKI MBIO ZA KILI MARATHON

Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya saruji Tanga Cement (TCPLC), Peet Brits, akigawa maji kwa mmoja wa washiriki wa mbio za Kilimanjaro Marathon ambapo kampuni hiyo imetumia zaidi ya shilingi milioni 36 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Mhazini wa Kampuni ya saruji Tanga Cement (TCPLC), Frederick Emmanuel akigawa maji kwa mmoja wa washiriki wa mbio za Kilimanjaro Marathon ambapo kampuni hiyo imetumia zaidi ya shilingi milioni 36 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya saruji Tanga Cement (TCPLC), wakishiriki mbio za KM 21 wakati wa mbio za killimarathon ambapo Kampuni Hiyo imetumia zaidi ya shilingi milioni 36 kudhamini vituo vya maji na kupoozea wakimbiaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Bi. Mtanga Noor (kulia), akigawa maji kwa mmoja wa washiriki wa mbio za Kilimanjaro Marathon.
Mkuu wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi (katikati), akigawa maji kwa mmoja wa washiriki wa mbio za Kilimanjaro Marathon.

Wadau mbalimbali wa michezo nchini kutoka katika sekta binafsi na ya umma wameshauriwa kuendelea kujiunga na mbio za nyika za Kilimarathon kila mwaka – Ambazo kwa sasa ni mbio maarufu kupita zote nchini, kwa kutoa udhamini na vilevile kwa kupeleka washiriki.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Tanga Cement, Bw Peet Brits, wakati wa mahojiano maalum kuhusu Kilimarathon mbio ambayo imekuwa ikivutia washiriki kutoka ndani ya nchi na ng’ambo, ambapo alijadili mbio hizo na manufaa yake kwa mapana.

“Ningependa kushauri mashirika na makampuni mengine, ya Serikali na yasiyo ya kiserikali, kujiunga na mbio hizi. Ninaposema kujiunga nina maana ya kushiriki katika mbio hizo, kudhamini na vilevile kwa kuleta washiriki kwa manufaa ya kiafya na vilevile kwa ajili ya kukuza bishara zao,” Alisema Brits.

Akiongelea mvuto wa mandhari ya Moshi ambako mbio hizo hufanyika mara moja kila mwaka kuwa ni rafiki na yanashamirisha mbio hizo. Meneja huyo wa biashara wa Tanga cement alisema kuwa wale ambao hawajajiunga na mbio hizo, 'wanakosa mazuri mengi’ na kuwa ‘ wanajikosesha muda mzuri wa burudani tosha’

Brits aliongeza: “Nafikiri inabidi watu waendelee kujiunga na mbio hizi mwakani kwa wale wasiokuja leo waje mwakani kwa wingi wajionee, hali inavyokuwa hasa unapokuwa katika vituo vya kuwapa wakimbiaji maji, vipozeo hisia unayoipata unapokuwa hapa uwanjani wakimbiaji wanapoanza na kumalizia mbio, uwanja wa hapa Moshi ukiwa umefurika watu Kama Hivi leo….kukutana na watu wengi kiasi hicho kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, hawatajutia kushiriki, na pengine wakajutia kwa nini miaka yote hiyo wamekuwa wakijikosesha burudani kama hii”. 

Meneja huyo alisifia mbio za Kilimarathon, ambazo mwaka huu zinaadhimisha mwaka wa 20 tangu kuanzaishwa kwake, na kuonyesha matumaini kuwa shamrashamra za mwaka huu wa 20 zitasaidia kunogesha mbio za mwakani, ambazo ni mara ya 19 kwa Tanga Cement Kushirikki.

“Kili Marathon limekuwa ni jukwaa bora ambapo inatuwezesha kuwasiliana ana kwa ana na wateja wetu na wadau wengine. Unapata fursa ya kusikia yale ambayo huwezi kuyasikia katika mikutano ya bodi, tumekutana na wateja kuanzia wadogo hadi wale wakubwa. Kwa hiyo haya maadhimisho ya miaka 20, nina amini, yataboresha zaidi raha ya Kili Marathon,” aliongeza.

Kwa upande wa biashara kwa wenyeji wa Moshi, Brits alisema kuwa Kili Marathon imekuwa ni mtambo madhubuti wa kuzalisha kipato kwa mji huo, na kuwa mbio hizo zimekuwa zikitunisha mikoba ya wenyeji kuanzia wenye mahoteli, huduma za malazi, watoaji wa huduma za chakula wadogo na wakubwa, wauzaji vinywaji baridi na vileo na wengineo.”

Aliongeza Brits: “Si hao tu, bali pia wapo wale wanaofanya biashara pembezoni mwa barabara wameuza matunda, mbogamboga kwa wasafiri wanaoingia na kutoka mjini Moshi.. Tusisahau vilevile wageni wanaokuja Tanzania kwa ajili ya mbio hizo. Hao wote mwisho wa siku wamechangia katika pato kuu la taifa kwa miaka 20 mfululizo.

Alisema Tanga Cement ni kati ya wadhamini wakongwe kabisa wa Killimanjaro Marathon, na kuongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishirikikisha wafanyakazi wake, na kuwa mwaka huu imepeleka timu ya wakimbiaji 25, na zaidi ya 30 wamekuwa wakojitolea kugawa maji kwa wakimbiaji. Alisema Brits : “Tunajivunia kuwa sehemu ya tukio maarufu kama hili la kimichezo nchini na tumefurahi kuwa ni sehemu ya historia ya Kilimarathon.

Sisi tunajiona kuwa tunakua sambasamba na Kili Marathon. Wakati mbio hizi zinatimiza miaka 20, sisi tunatimiza miaka 42. Jopo letu la wakimbiaji ni sehemu ya wakimbiaji ambao wamekuwa wakishiriki kila wakati wa mashindano. Kwa ufupi, tumewaleta wakimbiaji kuja kushindana mbali ya kujiweka vizuri kiafya.

Kuhusiana na kilichoivutia kampuni hiyo kubwa ya simenti kujiunga na mbio hizo nakutumia zaidi ya milioni 36 kwaajili ya kudhamini maji vipozeo kwaajili ya wakimbiaji, Brits alisema:” Tunapenda michezo, na hasa tunapenda mbio za Kilimarathon, kwa kuwa huu ndiyo mchezo pekee ambao unashirikisha wafanyakazi wetu wengi kwa mpigo, kutoka wakimbiaji hadi wasio wakimbiaji. Ninaposema wasio wakimbiaji nina maana ya wale waliojitolea leo hapa katika vituo vya kugawia maji na kazi za uwanjani. Kwa hiyo tunapoongelea Kilimarathon, tunaongelea Timu Simba kutoka Tanga Cement ikishiriki kwa ukamilifu
Share:

Tuesday, March 1, 2022

Wafanyakazi wa Absa Tanzania wajitolea damu kusaidia wodi ya wazazi ya CCBRT

 
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria (kushoto) akijitolea damu katika zoezi lililoandaliwa na wafanyakazi wa benki hiyo kutoa damu kwa ajili ya kusaidia wodi mpya ya wazazi katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kulia ni Muuguzi Mkunga wa hospitali ya CCBRT, Emiliana Tibilikirwa na Fundi Sanifu wa Maabara ya Hospitali hiyo, Athumani Daffa.
Meneja Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Linda Lance (kulia) akipata vipimo kabla ya kujitolea damu katika zoezi lililoandaliwa na wafanyakazi wa benki hiyo kutoa damu kwa ajili ya kusaidia wodi mpya ya wazazi katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaomhudumia kutoka kushoto ni Afisa Muuguzi wa Hospitali ya CCBRT, Christina Baluhya na Fundi Sanifu wa Maabara ya Hospitali hiyo, Athumani Daffa.
Product Implementation Analyst, Ridhiwan Ibrahim (kulia) na Meneja Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Linda Lance (wa pili kulia) wakijitolea damu katika zoezi lililoandaliwa na wafanyakazi wa benki hiyo kutoa damu kwa ajili ya kusaidia wodi mpya ya wazazi katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam hivi karibuni. kutoka kushoto ni Afisa Muuguzi wa Hospitali ya CCBRT, Christina Baluhya na Fundi Sanifu wa Maabara ya Hospitali hiyo, Athumani Daffa.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive