A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, April 22, 2022

WANANCHI IKUNGI WAHIMIZWA KUTUNZA CHAKULA ILI KUJIKIGA NA BAA LA NJAA

 Mwenyekiti  wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mwisi Kata ya Lighwa katika mkutano wa hadhara wa kuzungumzia maendeleo na kupokea kero za wananchi ili zifanyiwe kazi ulioandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Gabriel Mukhandi na kuhudhuriwa na umati wa watu uliofanyika jana mkoani Singida.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Stamili Dendego akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Lighwa Gabriel Mukhandi akijibu maswali ya wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mwenezi wa CCM  Wilaya ya IKungi, Pius Sanka akizungumzia Wana CCM wa kijijiji hicho wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM  Wilaya ya Ikungi, Asha Mjema akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi Shabani Mhimbani akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ikungi, Hawa Gidabudayi akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkazi wa Kijiji cha Mwisi Jeremiah Ntandu akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Ramadhani Hamisi akiuliza swali.
Zabron Mgghwai akiuliza swali.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Regina Mjungu akielezea kero ya kukithiri kwa wizi katika kijiji hicho.
Ester Paulina akiuliza swali.
Mkazi wa Kata hiyo Emmanuel Majani akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Lighwa, Gabriel Mukhandi akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa katika mkutano huo.
Katibu wa Mbunge Jimbo la Singida Mashariki, Ally Rehani akizungumzia kazi mbalimbali na michango iliyotolewa na mbunge wa jimbo hilo Miraji Mtaturu katika kata hiyo ambapo zaidi ya Sh.Milioni 3.5 amezitoa kutekeleza baadhi ya miradi katika kata hiyo.
Taswira ya mkutano huo.
Patrick Suna kutoka Chadema akipeana mkono na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa baada ya kuhamia chama hicho.
Swalehe Hamadi kutoka chama cha TLP akitema nyongo baada ya kuhamia CCM.
Mkutano ukiendelea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Ally Rehani, Emmanuel Majani na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ikungi, Shabani Mhimbani.
Anisia Marco kutoka TLP akikabidhi kadi kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa.
Hawa ndio viongozi waliohamia CCM kutoka vyama vingine. Kutoka kushoto ni Anisia Marco, Thomas Misanga, Patrick Suna na Swalehe Hamad "Maarufu Daktari wa Viatu"
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa na timu yake akikagua boma la nyumba ya walimu katika Sekondari ya Lighwa ambao ujenzi wake haujakamilika kwa zaidi ya miaka tisa.
Ukaguzi wa mradi wa ufugaji wa nguruwe katika kata hiyo ukifanyika. Mradi huo wa vijana unatokana na fedha asilimia 10 zinazotolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambapo kikundi cha vijana wa kata hiyo wanaofanya mradi huo wamekuwa wa mfano katika Halmashauri yaWilaya ya Ikungi. 


Na Dotto Mwaibale, Ikungi


WANANCHI  wa  Kijiji cha Mwisi Kata  ya  Lighwa Wilaya  ya Ikungi mkoani Singida  wametakiwa  kutunza   chakula  ili kujikinga na baa la njaa litakaloweza kutokea siku za usoni.  

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti  wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa wakati akiwahutubia Wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara wa kuzungumzia maendeleo na kupokea kero za wananchi ili zifanyiwe kazi ulioandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Gabriel Mukhandi na kuhudhuriwa na umati wa watu.

"Ndugu zangu mwaka huu haukuwa na mvua za kutosha na kusababisha mazao shambani kuwa machache hivyo nawaombeni tunzeni chakula kwani kutakuwa na upungufu mkubwa wa chakula" alisema Likapakapa.

Akijibu baadhi ya kero zilizoibuliwa na wananchi katika mkutano huo kama kukosekana kwa jengo la Mama na Mtoto alisema wananchi wanapaswa kuanzisha ujenzi hadi ngazi ya boma na Serikali isasaidia kulimalizia.

Akizungumzia Bwawa lililokuwa la TASAF ambalo hivi sasa limeharibika alisema litafanyiwa ukarabati ili lirudi katika hali yake ya kawaida na wananchi wawezekunufaika nalo lakini akaomba baada ya ukarabati huo iundwe kamati maalumu itakayokuwa ikisimamia bwawa hilo ambalo lilikuwa likitumika kwa kilimo cha umwagiliaji na uvugaji wa samaki.

Pia Likapakapa aliwaomba wananchi wa kata hiyo kutenga maeneo kutoka kwenye mashamba yao kwa ajili ya miundombinu ya barabara zitakazoweza kuwasaidia panapotokea matukio ya dharura kama magonjwa, moto na wajawazito waweze kufikiwa kwa urahisi na vyombo vya usafiri.

Halikadharika Likapakapa akizungumzia masuala ya kutumia muda mwingi katika maziko baada ya mtu kufariki ambapo alisema suala hilo ni la kijamii zaidi wenye maamuzi ni mfiwa hama viongozi wa dini wanaoongoza ibada za mazishi na Serikali haiwezi kuingilia jambo hilo kwani ni la kiimani zaidi.

"Hatuwezi kuingilia suala ili kwani wenye maamuzi ni ndugu wa mfiwa husika kwani wengine wanakuwa wanawasubiri ndugu zao wanaoishi mbali na viongozi wa dini hawezi kupangiwa muda wa kufanya ibada za mazishi" alisema Likapakapa.

Likapakapa aliyasema hayo kufuatia swali lililouklizwa na mmoja wa wananchi akiomba Serikali kupanga muda wakati wa shughuli za mazishi baada ya kuonekana yanatumia muda mwingi hadi kufikia wananchi wengine kuondoka katika misiba kwa kuchoka kutokana na kuwepo kwa mlolongo wa mambo mengi.

Diwani wa Kata hiyo Gabriel Mukhandi alisema lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuzungumzia ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati ya Kijiji cha Mwisi ambalo ni muhimu sana na kuwa litakuwa likiwahudumia wananchi kutoka kata za Ntuntu, Misughaa, Makiungu na Munghaa.

Alitaja lengo lingine kuwa ni kuzungumzia ukarabati wa Bwawa la TASAF ambalo lilisombwa na mafuriko, umaliziaji wa nyumba ya walimu katika Sekondari ya Lighwa ambao boma lake limedumu kwa zaidi ya miaka tisa pasipo kukamilika na pia walizungumzia zoezi la kitaifa la Anwani za makazi na postikodi.

Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Stamili Dendego alisema mikutano ya namna hiyo ni ya muhimu sana wananchi kushiriki ili waweze kutoa kero zao na kuchukuliwa na wahusika ziweze kutafutiwa ufumbuzi ambapo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kwenye mkutano huo.

Katibu Mwenezi wa CCM wa Wilaya hiyo Pius Sanka aliwaomba wananchi wa kijiji hicho na kata hiyo kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ambazo tayari zipo kwenye maeneo yao kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa ndani ambao mchakato wake  umeanza.

Katika mkutano huo  viongozi wanne kutoka vyama vya Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na TLP wa kijiji hicho walivihama vyama vyao na kujiunga CCM viongozi hao ambao walikabidhi kadi zao ni Patrick Suna, Swalehe Hamadi, Anisia Kisiu na Thomas Misanga.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive