A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, April 21, 2022

AKIBA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE DAR ES SALAM

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank  Plc Silvest Arumas akizungumza wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali wateja wake 

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Akiba Commercial Bank ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali na kuwa karibu  na wateja wao.


Wateja na wageni waalikwa wa Akiba Commercial Bank wakichukua mlo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali wateja wake

Akiba Commercial Bank tunatambua nakuheshimu imani za wateja na wadau wetu
 Akizungumza katika halfla ya futari iliyoandaliwa na ACB Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank  Plc Bw. Silvest Arumas  alisema benki hiyo imeweka mipango mikakati kwaajili ya wateja wake hasa katika kipindi hiki cha Ramadhan

Tunaupa umuhimu wa kipekee sana mwezi mtukufu wa Ramadhan sio tu kwa wateja na wadau bali ni kwa waislamu wote kwani kama benki tunadhamini nakujali kila dini hivyo hivyo tumejikita kikamilifu katika mwezi huu wa Ramadhan kwaajili ya kuwashika mkono ndugu zetu waislam.

Akiba Commercial Bank, umekuwa ni utaratibu wetu kama benki yenye kujali na kutambua umuhimu wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan tumekuwa tukiwaruhusu wafanyakazi kutoka kazini mapema kwaajili ya ibada na matayarisho ya futari.

Pia Akiba Commercial Bank, umekuwa pia ni utaratibu wetu kufanya hafla yakuandaa futari kwa wateja wetu kila mwaka kwaajili ya kuwaunga mkono ndugu zetu waislamu katika funga yao pia kudumisha mahusiano kati ya wateja na benki yao pendwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive