A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Sunday, March 27, 2022

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA USIMAMIZI WA FEDHA YANAYOTOLEWA NA DCB FOUNDATION KUENDELEA KUWANUFAISHA WATANZANIA

  
Ofisa Mikopo Vikundi vidogo vidogo wa Benki ya Biashara ya DCB, Leticia Nyato akizungumza na wajasiriamali jijini Dar es Salaam jana wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation.
Ofisa Mikopo ya Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, Odilia Johnson akizungumza na wajasiriamali jijini Dar es Salaam jana wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation.
Ofisa Masoko na Huduma kwa Wateja Benki ya Biashara ya DCB, Elizabeth Ntulu (kulia) akikabidhi cheti kwa Shafii Njayo wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Masoko na Huduma kwa Wateja Benki ya Biashara ya DCB, Elizabeth Ntulu (kulia) akikabidhi cheti kwa Amina Ally wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Masoko na Huduma kwa Wateja Benki ya Biashara ya DCB, Elizabeth Ntulu (kulia) akikabidhi cheti kwa Baraka Jeremia wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali wakati wa mahafali ya kwanza ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha yaliyotolewa na benki hiyo kupitia asasi yake ya DCB Foundation jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Wednesday, March 23, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK DEBUTS POPOTE VISA CARD, VOWS TO SUPPORT DIGITAL TANZANIA AGENDA




VISA Card East Africa Vice President Corine Nana (right), and Tanzania Commercial Bank Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi press a button to mark the official launch of the Popote Visa Card launched by Tanzania Commercial Bank to facilitate the Bank's customers access to any services and wherever they are in and out of the country the launch event took place today in Dar es Salaam






VISA card East Africa Vice President Corine Nana (center) with Tanzania Commercial Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi second left showing the POPOTE VISA CARD model during the official launch of the card launched by Tanzania Commercial Bank. and Tanzania Commercial Bank Telecommunications and Operations Director Jema Mssuya, CEO of UBX Tanzania LTD, Seronga Wangwe and TCB Internet Banking Senior Manager Allen Manzi at the event held today in Dar es Saam.





Tanzania Commercial Bank Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi, speaking during the official launch of the Popote Visa Card launched by Tanzania Commercial Bank to facilitate the Bank's customers accessing any services and anywhere in the country and abroad. today in Dar es Salaam


Vice President of VISA card East Africa Corine Nana (right), presenting the POPOTE VISA CARD card to one of the customers who attended the official launch of the Popote Visa Card launched by Tanzania Commercial Bank to facilitate the Bank's customers accessing any services and In any part of the country and abroad, the launch took place today in Dar es Salaam (center) by Tanzania Commercial Bank Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi.


Tanzania Commercial Bank customer showing the VISA CARD card of Tanzania Commercial Bank launched today




The government’s aspiration for a less cash economy got yet another vital digital finance shot in the arm yesterday following the official debut of an internationally accepted electronic payments card in the market by Tanzania Commercial Bank (TCB).

The bank has partnered with Visa International to introduce the new service that elevates its commercial clout in international trade finance circles and enables its customers to transact anywhere any time in the world.

Speaking at the launching ceremony of the Popote Visa Card, the Chief Executive Officer of TCB, Mr Sabasaba Moshingi, said the debit card has all it takes to make universal financial services to be within reach in Tanzania.

The Popote debt card partners vowed to support efforts for a less cash national economy by championing and promoting responsible and innovative digital payment solutions that are more convenient, safe and offer better money management options.

“Any efforts like the international debit card that we have launched today and our partnership with Visa are mportant to the government’s digital economy and cashless society ambitions,” Mr Moshingi noted.

He said the bank opted for the Visa partnership because the American multinational was the giant of digital payments in the world with an unmatched network of 61 million merchants.

Speaking at yesterday’s event in Dar es Salam, Visa East Africa officials said the company is committed to expand digital payments not only in Tanzania but across the world by working closely with partners like TCB to also bring the benefits of digital finance to consumers and government partners.

The Visa Vice President and Managing Director for East Africa, Ms Corine Mbiaketcha Nana, said Tanzania has all the ingredients for a cashless society.

The official was upbeat of the benefits the partnership with TCB will deliver and the added values that will be accrued from it, including cost savings through greater payments efficiency and speed.

“Like all innovative digital payment solutions, adoption and use of the Popote Visa Card offers significant benefits to individuals, business entities and the government,” Ms Nana pointed out emphatically noting that the impactful advancement of financial inclusion will make the most difference in the lives of many people.

The launch of TCB Popote Visa Card comes a week after the government revealed its plans and the investments to create a digitally empowered national economy.

The ICT minister Nape Mnauye said that already a US$150 million World Bank soft loan has been secured to advance the Digital Tanzania Project, whose ultimate goal is to stir the national digital transformation efforts.

He said already a blueprint is being drawn to chart out the roadmap for executing the grand digital economy venture.

Speaking yesterday at Hyatt Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam, TCB customers and other sectoral stakeholders said the Popote debit card rollout augurs well with ongoing local initiatives to accelerate digital payments.

The debut of TCB Popote Visa Card, they emphasised, was also a boon for supporting the government and national efforts to make Tanzania a digitally supported cashless society.

“The strategic partnership between TCB and Visa international does not only expand benefit the two organisations but will also greatly help to expand the local digital payments space and enhance commercial fortunes across the national payments value chain,” the General Manager of dt card Tanzania told this reporter.







Share:

BENKI YA CRDB YAJA NA MUAROBAINI KWA WAJASILIAMARI

 
Maafisa wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa wakitoa elimu ya utunzaji wa fedha na kuwafungulia akaunti wanakijiji wa Naunambe wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi.

Na Mwandishi Wetu, Ruangwa | Benki ya CRDB katika kuendeleza juhudi za Serikali katika kuhakikisha wajasiriamali wanafanikiwa katika biashara zao.

Hivi karibuni CRDB imezindua huduma ya utunzaji wa Fedha za wajasiriamali kupitia Akaunti iitwayo Hodari ambayo ni mahususi kwa wafanyabiashara wenye mitaji isiyozidi Milioni 300.

Akiongea na mwandishi wetu Kiongozi wa Mauzo na Huduma za Kibenki wa CRDB Tawi la Ruangwa, Lilian Makawa amesema Akaunti hiyo haina makato ya utunzaji wa fedha wala makato wakati wa kutoa pesa kutoka kwenye Akaunti hiyo.

"Hodari Akaunti ni akaunti sahihi kwa Wajasiriamali kwani ni akaunti rahisi kutumia kwasababu ni akaunti isiyo na makato iwe ni wakati wa kutoa hela au makato ya kila mwisho wa mwezi"

"Mteja wa Akaunti hii ana uwezo wa kutoa pesa zake wakati wowote kwenye ATM, Wakala au ndani ya Benki dirishani," aliongeza Bi Lilian.

Musa Mpue mmoja wa waendesha Bodaboda katika Kituo cha Mabasi Ruangwa anasema kupitia Akaunti ya Hodari ameweza kuhifadhi makusanyo yake ya kila siku anayoyapata kutokana na biashara yake ya usafirishaji kwa kutumia Bodaboda.

Akaunti ya hodari imenisaidia kuhifadhi makusanyo yangu ya kila siku yatokanayo na biashara yangu ya Bodaboda, na fedha hizo nazipata kwa wakati pale ninapozihitaji kufanya marejesho ya mkopo wangu wa Bodaboda,” alisema Musa.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa na wakati mgumu wanapozitunza pesa zao Benki, pale wanapozihitaji huhitajika kutumia taratibu kadhaa ambazo husababisha kutoweza kufanya miamala ya kibiashara kwa wakati. Benki ya CRDB imeondoa kikwazo hicho kupitia Akaunti hii ya Hodari kwani inawawezesha wafanyabiashara hawa kufanya miamala ya kipesa muda wowote kupitia CRDB Wakala.
Share:

Sunday, March 20, 2022

JUKWAA LA "Getpaid" KUTOA FURSA KWA VIJANA WA KITANZANIA

 

Mkuu wa Kitengo cha Biashara-GetPaid, Bw. Justine Mahinyila, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa la GetPaid, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Mpiga Picha Wetu

Washiriki wakifuatia  mijadala jinsi ya kutumia la Jukwaa la GetPaid, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa hili jijini Dar es Salaam jana. (Mpiga Picha Wetu)


Jukwaa la “GeitPaid” kutoa fursa kwa watanzania

 

Na Mwandishi Wetu

 
Jukwaa la Kijidital, “GetPaid” lenye lengo la kutoa fursa za Ajira na nyinginezo limezinduliwa jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mchango wa sekta binafsi kusaidia mikakati ya serikali inayolenga kupanua wigo wa fursa kwa vijana na watanzania kwa ujumla.

 
Mbali na mambo megine Jukwaa la GetPaid,  litasaidia Tanzania kupunguza wimbi kubwa la ukosefu wa ajira—kwa vijana na watanzania wote (wasomi na wasio soma,  amesema Bw. Richard Lema, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania DLT CP iliyobuni  na kutengeneza Mtandao wa GetPaid—wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa hilo jijini Dar es Salaam jana.

 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Lema, GetPaid ni jukwaa la kimkakati la kidijitali ambalo lengo lake kuu ni kuwaunganisha watanzania, ikiwa nia pamoja na vijana,  wafanyabiashara, wasomi, wasio soma, wajasiriamali, wanaofanyakazi binafsi na fursa mbalimbali duniani.

 
"Kwa kweli, hili ni jukwaa la kidijitali la pekee, ambalo linawaunganisha watu—wasaka fursa na watoa fursa, " ameongeza Bw. Lema

 
Alielezea GetPaid kama ni teknolojia ya kisasa, ambayo itawaunganisha watu na fursa mbalimbali kitaifa, kikanda na kidunia.   

 
Kwa njia ya jukwaa la GetPaid, watu wa aina mbalimbali – wazalishaji,  wafanyabiashara, wanaofanya kazi binafsi, watu wazima, vijana, wenye weledi na wasio na weledi - watawezeshwa kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo Afrika na nje ya Afrika.

 
"Jukwaa la GetPaid linawafanya waweze kunufaika na fursa mbalimbali duniani, elimu ya kidijitali na uvumbuzi. Hili linafanyika kupitia kikundi cha jumuiya, utumiaji rahisi na elimu," alisema Bw. Lema na kuongeza kwamba "bidhaa ya GetPaid ina vitu vitatu na inawapa watumiaji (waanzilishi, wafanyabiashara na wafanyakazi binafsi vifaa na elimu wanayohitaji kuishi, kufanyakazi na kupata ujira."

 
Akizungumza wakati wa uzinduzi, mtaalamu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari (ICT) Baraka Mafore alisema ingawa kuna ukuaji wa kasi wa uchumi wa kidijitali, bado kuna pengo kubwa linalotakiwa lijazwe, kwa vile mamilioni ya vijana katika nchi nyingi za Afrika hawana ajira.

 
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba pamoja na kwamba vijana wanaomaliza chuo na kuingia kwenye soko la kazi Tanzania wanaanzia 800,000 hadi 1,000,000 kila mwaka (NBS-2015), kwa wastani uchumi unatengeneza ajira zipatazo 250,000 tu kwa mwaka na asilimia 75 ya hawa vijana wanabaki bila ajira.

 
"Hata hivyo, kutumia njia na vifaa sahihi, kama jukwaa la GetPid, nchi za Afrika zinaweza kushuhudia idadi kubwa ya vijana wakijiunga na kuingia kwenye uchumi wa kidijitali," alisema mhitimu mmoja kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Asha Mkwezu wakati wa uzinduzi wa GetPaid APP.

 
DLT CP-Tanzania ni kampuni iliyosajiliwa na inamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania wenye vipaji ambao wameingia kwenye "huu uchumi wa kidijitali."
Share:

Wednesday, March 16, 2022

KONNECT TANZANIA YAFANYA UZINDUZI RASMI WA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI NCHINI

 Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi rasmi wa mtandao wenye kasi zaidi nchini Konnect utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.Meneja Mkuu wa Konnect Tanzania Bw. Philippe Baudrier akizungumza na wadau mbalimbali pamoja na maofisa kutoka Konnect wakati wa ghafla maalumu ya uzinduzi rasmi wa mtandao mpya wa satelaiti nchini utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.


Mshereheshaji wa shughuli ya uzinduzi rasmi wa mtandao wa Konnect Bernice Fernandez akizungumza na wadau mbalkimbali pamoja na maofisa wa Mtandao wenye kasi zaidi Konnect wakati wa shughuli ya uzinduzi wa Mtandao huo utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.


Baadhi ya wageni waalikwa na wana habari wakiwa katika majukumu yao kusikiliza na kufatilia uzinduzi rasmi wa mtandao wenye kasi zaidi konnect utakaowawezesha watanzania kupata huduma ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi kwa sababu mtandao wa Konnect ni mtandao wa kwanza nchini wenye kasi kuliko mitandao mengine.





Konnect Tanzania yajenga daraja la usawa wa kidigitali Tanzania

Dar Es Salaam, Tanzania, Machi 16, 2022 – Konnect Tanzania, iliyosajiliwa kama: “Konnect
Broadband Tanzania Limited” ni kampuni tanzu ya Eutelsat iliyojitolea kutoa huduma za kasi
zaidi za satelaiti. Kampuni imetangaza kuzindua ofa mpya ya mtandao wa satelaiti nchini
Tanzania yenye kasi ya hadi 100Mbps. Pamoja na leseni zote na kibali cha kiserikali, Konnect
Tanzania ina vibali vyote vinavyohitajika ili kuweza kutoa huduma za kimtandao wa bei nafuu
nchini.


Kulingana na Utafiti wa Uchumi wa Simu wa GSMA wa 2021, chini ya 28% ya watu katika Afrika
Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaweza kupata mtandao wa simu. Hii inashiria kuwa kuna
sehemu nyingine ulimwenguni ufikiaji wake ni wachini kama vile Europe na zaidi ya 80% ya
watu wameunganishwa. Uchumi wa intaneti barani Afrika una uwezo wa kufikia dola bilioni 180
ifikapo 2025, ambayo ingewakilisha 5.2% ya Pato la Taifa la bara kupitia kupanua matumizi ya
kidijitali, ukuaji wa miji na kupenya kwa simu mahiri.


Utoaji wa huduma za uhakika na haraka kote Tanzania ni muhimu kwa kuzingatia upenyezaji
mdogo wa intaneti nchini, iliyo chini ya 20%. Huku muunganisho ukiwa juu zaidi, huduma za
mtandao wa Konnect Tanzania, zilizoundwa na kupangwa kwa mahitaji ya ndani, sasa
zinapatikana kwa watumiaji wa aina zote nchini kote, kuanzia majumbani na biashara hadi
mamlaka za umma.


Meneja Mkuu wa Konnect Bw. Philippe Baudrier alieleza kuwa: “Huduma za mtandao wa
Konnect zimeundwa kukidhi mahitaji ya makazi na SMBs (wafanyabiashara wadogo na wa kati)
lakini pia zinaweza kusaidia katika maendeleo ya sekta mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo,
utalii, madini, elimu na afya.

Mtandao wa satelaiti ya kasi ya juu na uboreshaji wa sekta ya kilimo Tanzania
Mtandao wa kasi wa juu ni ufunguo wa kuboresha shughuli za kilimo ambazo zinawakilisha
26,74% ya pato la taifa la Tanzania. Kuongeza tija katika sekta ya kilimo sio tu kukuza Pato la
Taifa,bali kutaongeza maendeleo ya taifa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kitaifa wa Kikundi cha Wakulima nchini Tanzania Bw
Stephen A. Ruvuga alisema kuwa: “Mashamba mengi ya kilimo nchini Tanzania yapo katika
maeneo yaliyotengwa na hakuna mtandao wa intaneti. Kuunganisha mashamba haya kwa
mtandao wa satelaiti kutawawezesha wakulima kukusanya data muhimu kama vile unyevu wa
udongo na viwango vya mabwawa, pamoja na ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuboresha ufanisi
kwa kasi.


Kusaidia Sekta ya Utalii ya Tanzania katika ufufuaji wake baada ya Janga
Uwepo wa mtandao wa Kasi katika nyumba za kulala wageni utaongeza usalama na mvuto
katika sehemu za kitalii Tanzania, ambao umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na janga la
kimataifa na mchango katika Pato la Taifa kushuka kutoka 10.7% mwaka 2019 hadi 5.3% mwaka
2020. .


Bw. Kennedy Edward, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Hoteli za HAT Tanzania aliangazia:
“Wajasiriamali wa utalii wa Tanzania wanahitaji mtandao wa uhakika ili kutoa huduma bora,
kukuza ujuzi, na kufungua masoko mapya. Kwa vile tovuti nyingi nzuri zaidi za Tanzania ziko
katika maeneo ya mbali, Broadband ya satelaiti ya Konnect inaweza kusaidia sekta ya utalii kwa
kutoa muunganisho wa intaneti kwa wageni na wafanyakazi katika nyumba za kulala wageni,
zisizoweza kufikiwa na mitandao ya kitamaduni.”


Kuongeza usalama na tija katika sekta nzima ya madini
Janga la Covid-19 limeharakisha kwa kiasi kikubwa sekta ya madini kufahamu faida za mtandao
wa kasi wa juu. Idadi kubwa ya tovuti za uchimbaji madini za Tanzania ziko katika maeneo
yaliyotengwa bila muunganisho wa Wi-Fi au 4G.


Bw. Peter Kabepela, Naibu Mkurugenzi wa chama ya wachimbaji madini Tanzania: “Kuunganisha
migodi ya mbali ya Tanzania kwenye mtandao wa satelaiti kutaongeza tija na kuchangia katika
kulinda eneo lao. Pia itaboresha hali ya maisha ya mafundi wanaofanya kazi kwenye maeneo ya
uchimbaji madini yaliyo mbali na makazi yao.” Shukrani kwa muunganisho wake wa kasi wa
satelaiti, mtandao wa satelaiti wa Konnect ni nyenzo dhabiti katika kusaidia ukuaji wa mchango
wa Pato la Taifa wa sekta ya madini kutoka 3,5% hadi 10% ifikapo 2025.


Kujibu hitaji muhimu la mtandao wa bei nafuu wa kutegemewa wa kasi ya juu kote Tanzania
kutatoa manufaa mengi ya kijamii na kiuchumi. Kuongeza usawa wa kidijitali nchini Tanzania
kwa hakika kutakuwa na manufaa kwa maendeleo ya kiuchumi na kibinadamu na riziki; kusaidia
kuifanya nchi kuvutia na kustahimili.

Hatua rahisi za kusakinisha mtandao mpana wa satelaiti wa kasi zaidi wa Konnect
Kufikia mtandao mpana wa satilaiti ya kasi ya juu sana wa Konnect kunahitaji hatua kadhaa
rahisi. Wateja wanaweza kutembelea tovuti ya Konnect (www.konnect.com), kuzungumza moja
kwa moja na huduma kwa wateja kwa kupiga nambari +255 768 132 829 kuanzia saa 3.00
asubuhi mpaka saa 12.00 jioni au kwenda kwenye duka la washirika lenye leseni ili kukutana
moja kwa moja na mshiriki wa timu ya Konnect. Wafanyakazi waliojitolea watasaidia wateja
kuchagua kifurushi sahihi na kupanga usakinishaji wa haraka. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya
kujisajili kama mshirika tafadhali tembelea Konnect.com

About Konnect
Konnect is the Eutelsat Group entity in charge of retail marketing for a new generation of superfast
satellite broadband services. As its implementation accelerates, Konnect is redefining the connectivity
expectations of people who live and/or work outside the geographical boundaries of fibre, enabling
them to access an immediately available service with ultra-fast, unlimited and competitive offers of up
to 100Mbps. To find out more about Konnect's offers, visit www.konnect.com.

Contact

Name: Obafemi AGBANRIN
Tel: +255 767 256 405
Email: oagbanrin@eutelsat.com

Share:

Sunday, March 13, 2022

WANAWAKE KKKT BOKO WAFANYA MATEMBEZI YA SHUKURANI

 

.com/img/a/
Mwenyekiti wa Wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Sylvia Lupembe, akizungumza wakati wa matembezi ya shukrani 2022 yaliyowashirikisha wanawaka wa kanisa hilo..com/img/a/

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boko, Ambakisye Lusekelo (wa pili kulia) akiongoza matembezi ya Shukrani ya kilometa 5 yaliyoanzia Kanisa la KKKT - Boko na kuishia katika ufukwe wa Ndege Beach Mbweni jijini Dar es Salaam leo Machi 12, 2022. Matembezi hayo yakiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia ambapo Umoja wa Wanawake wa Usharika huo wametumia fursa hiyo kuhamasishana katika kuwachangia watoto waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambao wakisumbuliwa na ugonjwa wa saratani.

.com/img/a/
.com/img/a/
.com/img/a/
.com/img/a/
.com/img/a/
.com/img/a/
Share:

Friday, March 11, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAMFURAHISHA RC MONGELLA


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati), akikata utepe  kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha kushoto ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, pamoja na  Meneja wa Tawi la Tanzania Commercial Bank  Usa river, Speratus Kamala.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la benki hiyo jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi,wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha kulia ni Meneja wa Tawi hilo Speratus Kamala. 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi,wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha

 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (kushoto), pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi wakifungua pazia kwenye jiwe la msingi  kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Usariver lililofunguliwa leo wilaya ya Arumeru,Mkoani Arusha.

 
 
 
Tanzania Commercial Bank (TCB) yazidi kuchanja mbuga kutanua huduma zake imeendelea kuongeza jitihada kuwafikia Watanzania nchi nzima
Tanzania Commercial Bank imeendelea na juhudi zake za kuendelea kutanua huduma zake kwa kufungua matawi katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha kila mtanzania anaitumia Tanzania Commercial Bank.


Benki hiyo imetimiza haja yake hiyo kupitia huduma zake mbalimbali katika kuigusa jamii kwa kufungua tawi jipya katika mkoa wa Arusha wilaya ya Arumeru USA river katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali.


Tawi la USA River lilianzishwa mwaka 2007 kwenye ofisi za posta, Usariver ikiwa ni benki ya kwanza kufika na kutoa huduma za kifedha katika wilaya ya Arumeru Katika mkoa wa Arusha, Benki ya Biashara Tanzania ina matawi sita (6) Arusha Meru,Usariver, Rombo, Mto mbu,Sokoine na Tanzanite.
 

Tawi la Usariver lina jumla ya mawakala 60 ambao wamesambaa katika wilaya ya Arumeru pamoja na kusogeza huduma za kibenki kwa wananchi, Tanzania Commercial Bank pia inategemewa kufungua na kuendeleza fursa mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kuinua uchumi katika mkoa huo


Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, alisema wateja wa benki hiyo wapo katika mikono salama na kuwaomba wananchi waitumie benki hiyo kwani imekuwa ikifanya mambo mengi yanayolenga jamii.


“Benki imepata mafanikio makubwa, kwa sasa Tawi la Usariver lina jumla ya wateja 5,916 wanaofurahia huduma mbalimbali za kibenki hususani mikopo yenye riba nafuu kama ya kilimo, biashara, watumishi na wastaafu pamoja na kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ndani na nje ya nchi.

Lakini vilevile, Tanzania Commercial Bank ni wabunifu kwenye upande wa kidigitali tumeanzisha huduma ya kuweka akiba kwenye vikundi ambayo tumeshirikiana naVodacom na tumeshakusanya zaidi ya Tshs bilioni 27 lakini pia sisi ni wamiliki wa huduma ya Songesha ni huduma inayomuwezesha mteja kukamilisha miamala pale anapokua hanasalio. 


Lakini kikubwa zaidi, Benki yetu imefanikiwa kutoa kadi za Visa, hivyo basi wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla karibuni sana mjipatie Visa ATM card kwa kufanikisha miamala yeyote popote mlipo Kwa kipindi cha mwaka 2020 mpaka February 2021 tawi limeweza kutoa mikopo ya kiasi cha Tshs 5.78 Billioni  kwa wadau mbalimbali.


 Kuna jumla ya mawakala 60 wanaotoa huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha. Kukua kwa biashara kumefanikisha benki kuhama kutoka katika ofisi ndogo za TPC na kuhamia katika jengo Jipya tunalolizinduliwa leo lenye nafasi kubwa na kuwezesha kutoa huduma kwa ubora na umahiri zaidi.


 Kwa sasa tawi lina wafanyakazi 12 waliobobea katika mambo ya fedha na benki wakitoa huduma bora na kwa weledi wa hali juu.


“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo ya huduma za jamii; Tumefanikiwa kutoa misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa bweni la Shule ya sekondari ya wasichana Nduruma.”
Ni matarajio yetu kuwa biashara itaendelea kukua na kutuwezesha kufungua matawi katika kila wilaya ili kuwezesha bidhaa na huduma zetu kuwafikia watanzania wote kwa ukaribu zaidi .”


Benki imechangamkia fursa ya kukua katika wilaya ya USA river, huku pia ikipanua uwepo wetu nchini.
Tawi linapatikana kwa urahisi, huduma zote za kibenki zipo, pamoja na timu ya wataalam wenye ujuzi. Tunatazamia kukutana na wakazi wa USA river, wafanya biashara na fursa zinazoifanya Benki ya Biashara ya Tanzania kuwa mahali pazuri pa kufanya kazi.


Tanzania Commercial Bank pia inatoa huduma za Kibenki Mtandaoni kama vile Internet Banking, Mobile App & Mobile Banking. Lakini Benki pia iko karibu na wateja wake kupitia vituo vyetu vya Huduma kwa Wateja.


Mkuu wa Mkoa Arusha, alitoa shukrani kwa Benki kuweza kuwafikia wananchi wa Usariver na alitoa wito kwa wananchi ili kuweza kuchangamkia fursa hususani makundi ya kina mama kwasababu Tanzania Commercial Bank, ina akaunti maalum kwa ajili ya wanawake.


Aliongeza kwa kuishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kuendelea kuwekeza katika mkoa huo na kuwataka waendelee kuwekeza katika wilaya zote za mkoa huo.


Mongella amewasisitiza wananchi wa Arusha wajitokezea kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Tanzania Commercial Bank kwani imekuwa benki ya kwanza kuwajali na kuwasogezea huduma wananchi wa mkoa huo.


Kuhusu Tanzania Commercial Bank

Tanzania Commercial Bank Plc ni taasisi ya fedha iliyoundwa kisheria kutoka iliyokuwa
Benki ya Posta Tanzania (Tanzania Post Bank). Mtandao wa Tawi la Tanzania Commercial
Bank una jumla ya matawi 82 Tanzania nzima ikijumuisha bara na visiwani yenye makao
yake makuu jijini Dar es Salaam. TCB inatoa bidhaa na huduma ili kukidhi mahitaji ya
benki ya kibinafsi na ya biashara ya wateja. Tembelea tovuti yetu kujifunza zaidi
www.tcbbank.co.tz
Share:

Wednesday, March 9, 2022

ABSA TANZANIA KUDUMISHA HAKI NA USAWA WA MAENDELEO KWA WAFANYAKAZI WAKE

 
Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick Foya (wa sita kushoto), akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake jijini Dar es Salaam Jana. Absa iliandaa hafla hiyo kwa ajili ya Wanawake wateja wao, watoa Huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Pamoja naye ni baadhi ya viongozi wa Absa wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed (wa nane kushoto).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro (wa pili kulia) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume (kushoto) huku Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdi Mohamed akiangalia katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa kwa ajili ya baadhi ya wateja wake wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (kulia) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya baadhi ya wateja wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (katikati) akipokea tuzo ya shukrani kuwa mgeni rasmi kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya baadhi ya wateja wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- (Redskirts), Irene Sengati- Giattas.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro (wa pili kulia) akipokea tuzo ya shukrani kuwa mtoa mada kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Benki ya Absa Africa, Elizabeth Willilo katika hafla ya Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas na Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa benki hiyo, Esther Maruma.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume (wa pili kulia) akipokea tuzo ya shukrani kuwa mtoa mada kutoka kwa Mkuu wa wateja Wadogo wa benki hiyo, Ndabu Swere wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na benki ya Absa jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas na Mkuu wa Vipaji, Mafunzo na Uongozi wa Absa, Veronica Muumba.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa pili kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Ndabu Swere katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa baadhi ya wateja wake wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wa Absa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Benki ya Absa Tanzania, Eveline Kamara wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa Absa. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (katikati) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji uliotukuka Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Mauzo ya Masoko ya Nje, Irene Rwegalulira wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wanawake watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa Absa. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Ofisa katika kitengo cha wateja binafsi, Irene Msungu wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake benki hiyo. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Vipaji, Mafunzo na Uongozi wa Absa, Veronica Muumba, katika wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dkt. Ellen Mkondya Senkoro.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rex Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa utendaji bora Mkuu wa Kitengo cha Malipo wa Benki ya Absa Tanzania, Jane Mbwilo katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa Absa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania- Redskirts, Irene Sengati- Giattas, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (wa tatu kushoto) akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo huku wakionyesha alama ya usawa wa kijinsia ambayo ni kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya baadhi ya wateja wao wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam Jana.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Red Advocates, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wa pili kulia) na Mjumbe wa Bodi ya Benki ya Absa Tanzania, Fatma Amani Karume, wakikata keki katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na benki Absa kwa ajili ya baadhi ya wateja wake wanawake, watoa huduma wanawake na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro.
Share:

Tuesday, March 8, 2022

TUME YA PAMOJA YA FEDHA (JFC) YASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA MWANAMKE DUNIANI.

 

 

.com/img/a/
 Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika maandamano walipoungana na wanawake wengine  duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake duniani katika viwanja vya Uhuru jiji Dar es Salaam ambapo maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Visiwani Zanzibar ikiwa mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani

 
.com/img/a/

.com/img/a/

.com/img/a/
Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika picha za matukio mbalimbali

 

 Watumishi wanawake wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  ambayo hufanyika kila Machi 8 ambapo wanawake hao wameonyesha kujiamini katika kutenda kazi kwa maendeleo ya Taifa kama kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani Kizazi cha Haki na Usawa katika Maendeleo Endelevu,wafanyakazi hao walikuwa na shamlashala za za namna yake katika katika viwanja vya uhuru jijini Dar es Salaam.


KATIKA Maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani  Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) imetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu hassan kwa jitihada za kuwawezesha Wanawake katika sekta mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo na mwakilishi wa Tume ya pamoja ya Fedha (JFC)   alieleza kuwa katika  Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) imezingatia  kuwapa kipaumbele wanawake  na kutoa majukumu sawa na wanaume ili kutekeleza kauli mbiu ya Siku ya wanawake duniani.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive