Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa (wa tatu kulia), akikabidhi baadhi ya misaada kwa Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Child in the Sun, Padri Paul Raj kinachoendeshwa chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Sullivan Provost, Fanuel Nashon, Meneja wa shule hiyo, Richard Samwel Mkami pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost, Fanuel Nashon, akikabidhi baadhi ya misaada kwa mmoja ya watoto wanaoelelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto wenye Mahitaji cha Child in the Sun kinachoendeshwa na kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kusaidia jamii yenye mahitajii. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine kutoka kulia ni msimamizi wa kituo hicho, Padri Paul Raj, Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa pamoja na vijana wanaolelewa kituoni hapo.
Meneja wa shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost , Richard Samwel Mkami (kulia), akikabidhi baadhi ya misaada kwa Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Child in the Sun, Padri Paul Raj kinachoendeshwa chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine pichani ni vijana wanaolelewa katika kituo hicho.Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kuoka mikate cha Sands Bakery kilichopo Bunju, Sarah Makumbati (kushoto) akitoa mkono wa pongezi kwa mmoja ya wafanyakazi wa kituo cha kulelea watoto wenye Mahitaji cha Child in the Sun kinachoendeshwa na kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango maalumu wa shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kusaidia jamii yenye mahitajii. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu.
Baba wa Kiroho wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Mch: Tusimsahau Manoza akiendesha ibada fupi wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami.






0 comments:
Post a Comment