Sunday, June 27, 2021
Yara kushirikiana na serikali kuhamasisha matumizi bora ya mbolea na ukulima wa kisasa
Thursday, June 24, 2021
Wanafunzi wa Sekondari ya Sullivan wawakumbuka wenye mahitaji
Sunday, June 20, 2021
Benki ya TPB Yapata faida ya Bilioni 21
BENKI ya TPB imepata faida ya Shilingi bilioni 21 kabla ya kodi kwa mwaka 2020. Kiasi hicho ambacho kimepatikani kabla ya kodi, kinatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kikubwa ukizingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza mwaka jana, hasa janga la Corona lililoathiri dunia nzima.
Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa wanahisa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo, Dkt. Edmund B. Mndolwa alisema benki hiyo inaendelea kufanya vizuri kwa kupata faida hiyo kabla ya kodi.
Utendaji kazi uliotukuka, ufanisi na umakini wa menejimeti ya benki huku wakisimamiwa kwa karibu na Bodi tumeweza kupata faida kubwa ambalo ni jambo la kujivunia sana kwa kufanya kazi kubwa kwa tija,’’ alisema Dkt. Mndolwa.
Alisema kwamba pamoja na kwamba benki hiyo ina mtaji mdogo, ikilinganishwa na benki nyingine, imeendelea kufanya vizuri katika nyanja zote kwa miaka takriban kumi.
Dkt. Mndolwa alisema kwamba benki hiyo itaendelea kujipanga na kupanua shughuli zake za kibenki nchini na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa sasa katika sekta ya fedha nchini.
Benki ya TPB ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 11 ya mwaka 1991, kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 1992. Mwaka 2016 jina la Benki lilibadilishwa na kuwa Benki ya TPB badala ya Benki ya Posta Tanzania.
Katika kuendelea kuelezea matukio makubwa Kwa mwaka 2020, Dkt. Mndolwa alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
iliziunganisha Benki ya TPB na Benki ya Biashara ya TIB. Lengo likiwa kuunda benki kubwa ya serikali itakayo boresha huduma, kupanua wigo wa mtandao na kutengeneza faida kubwa.
Benki ya TPB itaendelea kuboresha huduma zake na kubuni huduma mpya zinazokidhi matarajio ya wateja na kuwafikia wateja wengi zaidi wa kipato cha chini.
Miongoni mwa huduma kama hizo ni SONGESHA na M-KOBA ambazo zinatolewa na Benki ya TPB kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Vodacom.
Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Edmund Mndolwa akimalizia taarifa yake amesema Benki ya TPB inafanya vizuri katika soko la mabenki na hivyo kutoa wito kwa wateja kuendelea kuiunga mkono Benki yao. Mwelekeo ni mzuri na ndiyo maana benki imeendelea kukua na hadi kufikisha thamani ya Mali za Shilingi trioni moja mwisho mwa mwaka 2020 ikishika nafasi ya Saba kati ya benki zaidi ya 50 kote nchini.
Tuesday, June 15, 2021
RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA SGR MWANZA-ISAKA KM 341
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko ziarani mkoani Mwanza akikagua miradi ya maendeleo. Katika ziara hiyo Rais Samia amezindua rasmi ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga
Uzinduzi wa ujenzi wa kipande hicho cha reli ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa kipande hicho cha tano kinachojengwa ndani ya miezi 36 sawa na miaka mitatu.
Kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa nchini Tanzania kutasaidia kutatua kero ya usafiri kwa kusafirisha mizigo na abiria kwa uharaka zaidi katika nchi za ukanda wa maziwa makuu.
Rais Samia amezindua kipande hicho cha reli kutoka Mwanza hadi Shinyanga chenye urefu wa kilometa 341, ambapo kilometa 219 zitatumika kama njia kuu huku kilomita 122 zitatumika kama njia za kupishana na vituo vya kushuka na kupanda abiria ni 9, huku idadi ya vivuko vya chini vitakavyojengwa ni 44 na vya juu vitakuwa ni 23.
Mapema mwezi Januari mwaka huu, serikali za Tanzania na china zilitiliana saini za makubaliano ya ujenzi wa reli ya kisasa ambao utagharimu jumla ya shilingi za kitanzania trilioni 3.1 sawa na zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.326.
Kuanza kwa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa nchini Tanzania, kunatajwa kuwa na tija hasa kwa wananchi wa mikoa hiyo kwani zaidi ya ajira elfu 75 zinatajariwa kupatikana kwa miaka yote mitatu ya ujenzi wa reli hiyo.
Kuwekwa kwa jiwe la msingi ni kiashiria cha kuanza kujengwa kwa kipande cha tano, ambapo kipande cha kwanza ni kutoka dar es salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Makutupora, Makutoporakwenda Tabora, Tabora mpaka Isaka na Isaka hadi jijini Mwanza.
Akizungumza mkoani mwanza baada ya raisi kuzindua awamu ya tano ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka mwanza hadi isaka Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Michael Zhang alisema kwasasa kampuni hiyo inashirikiana kwa ukaribu zaidi na Shirika la Reli Tanzania TRC kwa kutoa vifaa vya mawasiliano na huduma kwenye miradi ya SGR ikiwemo Mfumo wa wa Teknolojia ya Mawasiliano-Reli (GSM-R) ambayo baadae itabadilika na kuwa mfumo wa LTE-R.
Niimani yetu kwamba chini ya uongozi mpya wa Rais Mama Samia Suluhu, Huawei itaendelea kujenga Miundombinu ya TEHAMA kulingana na Dira ya maemdeleo ya Tanzania 2025" aliahidi
Friday, June 11, 2021
Benki ya Akiba yashiriki katika zoezi la kutoa na kuchangia damu
Kama sehemu ya jamii pamoja na kutambua umuhimu wa kuokoa maisha, Benki ya Akiba imeshiriki kikamilifu katika zoezi muhimu la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya siku ya maadhimisho ya siku ya kuchangia damu ambapo kilele cha maadhimisho yake ni June 14, 2021.
BENKI YA NBC YASOGEA KARIBU ZAIDI KWA WAFANYABIASHARA WANAOCHIPUKIA
Mkurugenzi wa Wateja wa Rejareja na Binafsi wa NBC, Nd Elibariki Masuke (Kulia) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Bi Neemarose Singo (Kushoto), wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Twende Sawa na NBC inayolenga kuwafikia wafanyabiashara wanaochipukia nchi nzima na kuwasogezea akaunti ya Kua Nasi mahususi kwa wajasiriamali isiyo na gharama za uendeshaji pamoja na kuwapa elimu ya biashara wakiwa kwenye biashara zao.
Benki ya Taifa ya Biashara leo imezindua kampeni yake ya Twende Sawa na NBC yenye lengo la kuwafuata na kuwapa elimu wafanyabiashara wanaochipukia katika maeneo yao ya kazi na biashara. Kampeni hiyo imezinduliwa leo katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo wafanyakazi na baadhi ya wateja wa benki hiyo
Saturday, June 5, 2021
KAMPUNI YA UNILEVER TANZANIA YATOA MKONO WA SHUKRANI KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI DAR ES SALAAM
Thursday, June 3, 2021
SULLIVAN PROVOST BOYS’ SECONDARY SCHOOL COME WITH 'GIVEAWAY DAY TO THE NEEDY'
Tuesday, June 1, 2021
Russia and Tanzania to create joint environmental projects
Russia and Tanzania to create joint environmental projects
Dar es Salaam, June 2nd, 2021 – The Russian Society of Friendship that was formed in Russia by public figures and entrepreneurs will join forces with Tanzania to promote environmental and humanitarian projects at the international level.
The head of the Organisation, a member of the Russian Geographical Society Yuri Korobov said "Firstly, we plan to work on environmental projects. This is in both Russia and Tanzania, the problem of mass deforestation is the most acute. Because of the low cost, Tanzania is deforesting widespread rainforests, which are already few on the planet.
Tanzania is faced with a number of environmental problems. Resources are being
depleted, with major developmental and environmental implications. The major
environmental problems facing Tanzania are land degradation, lack of accessible, good
quality water for urban and rural inhabitants, environmental pollution, loss of wildlife
habitats and biological diversity, deterioration of aquatic systems and deforestation.
The Russian Society of Friendship plans on working with organisations in Tanzania such as The National Environmental Management Council (NEMC) which has the responsibility of advising the government on all matters related to the environment.
Korobov looked at other problems that are affecting the environment of which the society also plans on addressing in Tanzania.
· Looking at abandoned mines, which are not properly preserved after mining, releasing harmful chemical gases that lead to soil degradation,
· Mass deforestation
· Environmental pollution
“All of the above problems can be leveled at the expense of existing technologies in Russia. That's why we plan to conduct mutual training and exchange of specialists - environmentalists, engineers, chemists and volunteers," Korobov said.
The Russian Friendship Society and Tanzania are expected to sign their first agreement with the Tanzanian Friendship Society at the end of June 2021. As part of the agreement, the parties will create a business council, which will include members of the public and entrepreneurs.
"Together we will work together and implement an understanding of how projects should be implemented on the ground, so that everywhere, even in commercial projects, in which we will participate as consultants and give information support, there is an environmental focus," Korobov said.
In addition, the organization plans to implement a number of other projects. Among them are the creation of a platform of economic cooperation between the business of Tanzania and Russia, the holding of an economic forum with the theme of mutual investment attractiveness, the preparation of educational programs for students and young people of Russia and Tanzania, cooperation in the development of the agricultural sector of both countries, as well as the implementation of safe cognitive tourism programs, cultural exchange.
The Society of Friendship with Tanzania was established in Russia in April 2021 by an initiative group of public figures and entrepreneurs to promote environmental and humanitarian projects at the international level.
In 2019, Sochi hosted the first Russia-Africa economic summit, which resulted in a declaration containing the goals and objectives of further development of Russian-African cooperation in the fields of politics, security, economy, scientific, technical and cultural and humanitarian spheres. The second Russia-Africa summit is scheduled for 2022.
We look forward to a fruitful friendship between Russia and Tanzania towards an environmentally friendly country and continued partnership.