Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni iliyozinduliwa na NBC kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka, Meneja Masoko wa Sanlam, Marco Yambi na Mkurugenzi wa Mauzo wa Total, Marieme Sow.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Mauzo wa Total, Marieme Sow (kushoto kwake), wakionyesha kadi ya kuwekea mafuta ya Total wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayofanyika kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka, Meneja Masoko wa Sanlam, Marco Yambi, Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total, Marsha Msuya na Meneja Mahusiano Kitengo cha Bima cha NBC, Kuruthum Mwaluwinga.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (kushoto), akikabidhi kadi ya kujazia mafuta ya Total kwa mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Danford Robert Buguru wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoangalia ni wawakilishi kutoka NBC, Sanlam na Total.
Mkuu wa Kitengo cha Bima cha Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kushoto), akikabidhi zawadi mbaimbali kwa mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Robert Danford Buguru, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoangalia ni wawakilishi kutoka NBC, Sanlam na Total.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (katikati), akisaidia kuweka mafuta ya ofa katika gari la mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Robert Danford Buguru (kulia), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Nyuma yake ni Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC, David Raymond (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ambapo NBC ilizindua kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Sanlam imezindua kampeni ya bima ya magari itakayojulikana kama “Ifurahishe gari yako”.
Kampeni hiyo inayoanza Desemba mwaka huu hadi Januari mwakani ni sehemu ya malengo ya benki kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja kwa kuwapa mahitaji muhimu kupitia huduma bora zilizoandaliwa mahsusi kwa ajili yao.
Kwa kutambua umuhimu wa usalama kwa wasafiri na watumiaji wote wa vyombo vya moto kwa ujumla, katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, NBC imemrahisishia mteja kupata kifurushi kizuri cha bima kwa ajili ya magari kikiambatana na nyongeza kadhaa za kuvutia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Kituo cha Mafuta cha Total, Mbezi jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa NBC, Benjamin Nkaka alisema kampeni hiyo imezinduliwa katika kipindi sahihi cha mwaka ambapo kwa kawaida huwa na idadi kubwa ya wasafiri.
NBC imedhamiria kuboresha huduma za bima na kufanya kasi ya matumizi ya bima nchini kuongezeka, kwa kupitia kampeni hii, wateja watakaonunua bima katika matawi ya NBC watapata ofa kadha wa kadha zikiwemo huduma ya bure ya mafuta ya kilainishi cha injini na mafuta ya bure kutoka vituo vya mafuta vya Total pamoja na bima ya bure ya ajali ulemavu wa kudumu na gharama za matibabu kutokana na ajali.
Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo, Meneja Mahusiano wa Bima kutoka NBC Bi. Kuruthum Mwaluwinga alisema, wamiliki wa magari yenye thamani ya TZS 50,000,000 na zaidi watanufaika na mafuta bure pamoja na bima ya bure ya ajali, ulemavu wa kudumu na gharama za matibabu kutokana na ajali.
Aliongeza kuwa kwa wateja wenye magari yenye thamani ya kuanzia TZS 15,000,000 hadi 49,900,000, watapata lita 10 za mafuta bure katika kituo chochote cha Total nchi nzima, bima ya ajali ama ulemavu wa kudumu na gharama za matibabu.
Mwisho, kwa wateja wenye magari yenye thamani ya kuanzia TZS 7,000,000 hadi 14,900,000, watapata lita tano za bure za mafuta katika kituo chochote cha Total nchini, bima ya ajali ya bure ama ulemavu wa kudumu na gharma za matibabu. Wateja wote kwenye vipengele tajwa watapata kadi ya Total kwa ajili ya kujazia mafuta.
Alimaliza kwa kusema: "NBC kupitia Sanlam na kampuni nyingine za bima hutoa huduma bora za bima za aina mbalimbali kwa wateja wetu zikijumuisha bima za maisha na za kawaida. Huduma hizi tayari zipo katika matawi yetu yote yanayopatikana kote nchini.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke, alisema kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ni ishara wazi ya dhamira NBC kutoa huduma bora za kifedha kwa wateja wake hapa Tanzania.
"Pamoja na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 ya kutoa huduma za kuvutia, siku zote NBC inajivunia kuzindua huduma zenye viwango vya juu kwa manufaa ya wateja wetu. Tunawakaribisha wote kutumia na kufurahia huduma hizo za kibenki.”
NBC imeendelea kuwa kinara katika ubunifu ambapo kwa mwaka huu pekee imefanikiwa kuzindua huduma na bidhaa kadhaa za kufurahisha, kama Klabu ya Biashara ya NBC inayolenga kuwapa maarifa muhimu ya biashara wafanyabiashara wa kati na wadogowadogo ili waweze kuendeleza biashara zao kwa ufanisi; NBC Kiganjani ambayo ni suluhisho rahisi kwa watumiaji kwani ni huduma za kidijitali zinazotembea. Bidhaa nyingine mpya ni Akaunti ya Fasta inayowezesha kufunguliwa kwa akaunti haraka na mteja kupewa kadi ya Visa papo hapo.
Kwa muktadha huo huo, NBC imeendelea kukuza mtandao wa mawakala wa huduma zake (NBC Wakala) nchini. Zaidi ya mawakala 2,200 wanawezesha huduma za kibenki kupatikana kwa urahisi hata katika maeneo pasipokuwa na matawi ya benki.