Mshambuliaji machachali wa timu ya Magereza, Franki William, akijaribu kumtoka beki wa kushoto wa timu ya Azam Poly sacks Iddi Ramadhani, wakati wa mchezo wa ligi inayokwenda kwa jina la PROPHET SUGUYE CUP iliyoendelea jana tarehe 28.5.2019 katika viwanja vya Misitu Kivule nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo timu ya Magereza imeibuka kidedea kwakuinyuka timu ya Azam bao 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Magereza Moses Godfrey (katikati), akiwania mpira wakati wa mchezo na timu ya Azam Poly sacks, wakati wa mchezo wa ligi inayokwenda kwa jina la PROPHET SUGUYE CUP iliyoendelea jana tarehe 28.5.2019 katika viwanja vya misitu kivule nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo timu ya Magereza imeibuka kidedea kwakuinyuka timu ya Azam bao 1-0.
Beki wa timu ya Home Boys ya kitunda, Daniel Moses (wa pili kulia), akiokoa moja ya mpira uliopigwa na mshambuliaji wa timu ya Kitunda FC wakati wa mchezo wa ligi ya PROPHRET SUGUYE CUP, inayoendelea katika viwanja vya Misitu Kivule nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam katika mchezo huo Kitunda FC iliibuka kidedea kwakuichabanga Home Boys bao 2-1 ambapo timu itakayoweza kufanya vizuri siku ya fainali itajinyakulia kitita cha shilingi milioni mbili.
Baadhi ya watoto wakiwa juu ya mti wakishuhudia mtanange huo
Kikosi cha timu ya Home Boys wakiwa katika picha ya pamoja kabla yakuanza kwa mchezo wao dhidi ya Kitunda FC.
Kikosi cha timu ya Magereza Dar wakiwa katika picha ya pamoja kabla yakuanza kwa mchezo wao dhidi ya Azam Poly Sacks.
Kikosi cha timu ya Kitunda FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla yakuanza kwa mchezo wao dhidi ya Home Boys.
Mshambuliaji wa timu ya Magereza Christopher Msikwe, alieruka juu akiipatia ushindi timu yake baada ya kupika mpira kwakichwa na ukaenda moja kwa moja nakutinga wavuni.
Mshambuliaji wa wa timu ya Azam Poly Sacks Selemani Aguero akimtoka beki wa timu ya Magereza wakati wa mchezo, wakati wa mchezo wa ligi inayokwenda kwa jina la PROPHET SUGUYE CUP iliyoendelea jana tarehe 28.5.2019 katika viwanja vya misitu kivule nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo timu ya Magereza imeibuka kidedea kwakuinyuka timu ya Azam Poly Sacks 1-0.
Kikosi cha timu ya Azam Poly Sacks wakiwa katika picha ya pamoja kabla yakuanza kwa mchezo wao dhidi ya Magereza Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa ligi inayokwenda kwa jina la PROPHET SUGUYE CUP iliyoendelea jana tarehe 28.5.2019 katika viwanja vya misitu kivule nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo timu ya Magereza imeibuka kidedea kwakuinyuka timu ya Azam bao 1-0.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Prophet Suguye Cup, Robert Mujuni akijadiliana jambo na baadhi ya viongozi wa Kamati hiyo.
0 comments:
Post a Comment